Nimependa sana ndugu yangu Mwigulu ulivomjibu mwana JF inaonekana unajua kuna shida ya watendaji serikalini na siyo sera wala mipango ya serikali ya chama cha mapinduzi. Ushauri wangu kwako kwa kuwa ni kiongozi wa chama tawala anzieni kwenye hizi halmashauri ndiko kuna shida kubwa, kama kweli mna nia ya dhati kuwapa watanzania maendeleo ya kweli hakuna pa kuanzaia ni kusafisha kabisa watendaji wabovu katika halmashauri kwa kuwa huku ndiko kwenye roho za watanznia maskini. Ni mawazo yangu tu ndugu yangu mwigulu maana nakufahamu toka tukiwa pale mlimani ulikuwa mpambanaji na nina imani kwa vijana kama nyinyi naamini mna mtazamo mpana wa maendeleo ya kisasa. Kila la heri na heri ya pasaka mkuu Mwigulu.