Nape na Miaka 35 ya kupinga rushwa CCM

KIM KARDASH

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
5,139
1,139
[h=3]ccm kuadhimisha miaka 35 ya kupinga rushwa kwenye chaguzi zake[/h] on Monday, January 16, 2012
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema maadhimisho ya kuzaliwa kwake ya mwaka huu pamoja na mambo mengine kitayatumia kupiga vita wagombea wote wanaotoa na kupokea rushwa wakati wake mkuu.

Pia kitatumia maadhimisho hayo kuhamasisha wananchama wake waadilifu na waaminifu kujitokeza kugombea katika uchaguzi huo utakaofanyika mwaka huu, kuanzia ngazi za mashina hadi taifa.

Hayo yalisemwa leo na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape na Nnauye wakati akizungumza na waandishi wa habari, kwenye Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba mjini Dar es Salaam.

Nape alisema, Chama kitatumia fursa hiyo pia kuwaelimisha wanachama wake na wananchi kwa jumla kuhusu mabadiliko ya Katiba ya nchi yanayokusudiwa kufanyika, ikiwa ni pamoja na msimamo wa kuilinda nchi, amani, na kupatikana kwa Katiba bora itakayokuwa na manufaa kwa watu wote.

Alisema, maadhimisho hayo yataanza Februari mosi na kufikia kilele chake Februari 5, 2012 yakiambatana na shughuli mbalimbali yakiwemo matembezi ya mshikamano yatakayofanyika kila mkoa wakati Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete atakuwa mgeni rasmi katika kilele cha matembezi hayo kitakachofanyika Mwanza.

"Maadhimisho haya ni kumbukumbu muhimu kwa Chama Cha Mapinduzi kufikisha miaka 35 ya uhai wake yangu vyama vya TANU na ASP vilipovunjwa na kuundwa chama kipya cha CCM chenye nguvu, Februari 5, 1977",lisema Nape na kuongeza.

"Sherehe hizo huadhimishwa kwa Chama na Jumuia zake kufanya shughuli mbalimbali za kisiasa na kijamii. Aidha, Kitaifa Chama huteua mkoa mwenyeji wa sherehe hizi ambazo huambatana na matembezi ya mshikamano".

Alisema kwa kuwa mwaka huu ni wa Uchaguzi Mkuu wa Chama kimependekeza kaulimbiu mahsusi itakayotumika katika sherehe hizo kuwa ni "CCM Imara na Madhubuti inaanza na mimi; naimarisha Chama Changu kwa kuchagua viongozi bora na waadilifu".

Nape alisema uzinduzi wa sherehe hizo utafanyika kila mkoa Januari 30, mwaka huu na kufuatiwa na wiki ya shughuli za Jumuia, ambazo kila Jumuia itapanga ratiba ya mikutano ya ndani na shughuli za kijamii kama kupanda miti.

CCM imewataka wajumbe wa Kamati ya Siasa na Halmashauri Kuu ya mikoa kutumia wiki hiyo kufanya ziara katika matawi kuimarisha uhai wa Chama.

Kutoka Nkoromoblog
 
"CCM Imara na Madhubuti inaanza na mimi; naimarisha Chama Changu kwa kuchagua viongozi bora na waadilifu".

Yetu macho na masikio....!!
 
Hadithi hadithi......hadithi njoo utamu kolea!!hizo ni ngonjera,namkumbusha nape kuwa maadhimisho ya mwaka jana ndiyo yalizua gamba ni vizuri kwanza wakamalizana na hilo kuliko kurukia lingine,pia aelewe kuwa ccm bila rushwa haiwezi kushinda hivyo hilo ni tatizo lingine anataka kuanzisha na atapata upinzani zaidi ya gamba kwani hapa ni ccm wengi mno kama si wote hawatakuwa naye pamoja,kuwa makini utazeeka kabla ya wakati wako ndugu yangu,kuisemea ccm ni lazima uwe kama kachizi fulani hivi.
 
Nakumbuka enzi zile tarehe 5 Februari kila mwaka tunapumzika kiserikali eti ni sikukuu ya ccm!!!!?
 
Yaleyale ya siku 90 zikapita kimya na hili litapita kimyakimya bila impact yoyote.
 
Nape kaza buti mwanangu mwenyewe achana na hawa jamaa waliojazana humu,kazi yao kukejeli kejeli tu kila jambo...........
 
Kweli ccm na nape wao ni kichwa cha mwendawazimu, yani maadhimisho ya rushwa. Kwani kwa mfano wanafanya kutimua ccm wote wanaotoa na kupokea rushwa sidhani kama ccm itabakiwa na mtu
 
Haya tusubiri tuone jinsi wagombea watakavyowajibu wale wapiga kura wanaowauliza "UNATUACHAJE SASA" mara baada ya kumaliza kuomba kura.
 
Nape kaza buti mwanangu mwenyewe achana na hawa jamaa waliojazana humu,kazi yao kukejeli kejeli tu kila jambo...........

Ndugu kama mtu huwezi kufanya jambo usijigambe mbele za watu. Nani aliyemwabia atangaze "siku 90 wajivue gamba la sivyo tutawang'oa". Watu walisema "hawawezi" na ni kweli mpaka sasa wameshindwa sasa kwa nini wasikejeliwe?

Mpaka watakapowang'oa ndio watapewa heshima yao, until then tutaendelea kuwaita wachovu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom