Nape: Mleteni Slaa Arumeru, Asema CCM wanakesha wakiomba aruhusiwe

TONGINDI

Senior Member
Nov 23, 2011
174
32
Nape: Mleteni Slaa Arumeru
• Asema CCM wanakesha wakiomba aruhusiwe

na Mwandishi wetu


amka2.gif
SIKU moja baada ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, kusema ni ruksa kwa Katibu Mkuu wao, Dk. Willibrod Slaa, kugombea ubunge katika jimbo la Arumeru Mashariki, Chama cha Mapinduzi (CCM), kimejibodoa kuwa kinamsubiri kwa hamu.
Akizungumza na Tanzania Daima jana, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Nape Nnauye, alisema kuwa CCM wanaomba usiku na mchana Dk. Slaa agombee katika jimbo hilo ili wamalize kazi ya uchaguzi mkuu 2015.
Kwa kujiamini, Nape alisema kuwa Dk. Slaa akitia mguu Arumeru Mashariki, haponi, hivyo utakuwa mwisho wake kisiasa na umaarufu wa CHADEMA.
“Dk. Slaa ndiye jembe la CHADEMA, akija Arumeru Mashariki, tutahakikisaha tunalikata makali na tukishafanya hivyo hawezi tena kuwa maarufu mwaka 2015 na chama kizima hakitakuwa na nguvu, hapo kazi yetu ni nyepesi kama kumsukuma mlevi,” alisema Nape.
Alipoulizwa endapo kauli hiyo ni ya woga dhidi ya Dk. Slaa ili kiongozi huyo asiende Arumeru, Nape alijibu kwa kujiamini kuwa CHADEMA ikitaka kuthibitisha hilo, imlete kigogo huyo katika jimbo hilo.
Aliongeza kuwa umaarufu wa CHADEMA unatokana na mtu mmojammoja kama Dk. Slaa na kutamba kuwa kiongozi huyo ni maarufu awapo bungeni, hivyo watahakikisha anashindwa ili uwe mwisho wake kisiasa na chama chake.
Hata hivyo, pamoja na kauli hizo za majigambo ya Nape, Dk. Slaa amekwishatoa msimamo wake kwamba hakakuwa tayari kuwani ubunge katika jimbo lolote kwa wakati huu.
Tangu kuanza kwa harakati za kuwania ubunge katika jimbo hilo, Dk. Slaa amegusa hisia za wasomi wanaharakati na makundi mbalimbali ya kijamii wakiwemo wafuasi wa chama chake, wakimtaka agombee kiti hicho.
Matakwa hayo ya kumtaka Dk. Slaa agombee, yanatokana na imani kwamba kulingana na umaarufu aliojijengea na rekodi yake ya utendaji wenye audilifu, CHADEMA haitapata ushindani mkubwa toka kwa CCM.
Itakumbukwa kuwa Dk. Slaa aligombea urais katika uchaguzi mkuu uliopita na kukonga nyoyo za Watanzania wengi ambao hadi sasa wanaamini kuwa aliibuka mshindi ila kura zake zilichakachuliwa.
Hisia za wanaotaka Dk. Slaa agombee ubunge katika jimbo hilo, zimechochewa zaidi na kauli ya Mbowe, aliyekaririwa na gazeti moja akisema kama kiongozi ataamua kuwania kiti hicho, CHADEMA itaheshimu uamuzi wake.
Mbowe pia alisema kama Dk. Slaa hatakuwa tayari, chama vilevile hakiwezi kumlazimisha kugombea. Akitamba kuwa hana shaka ya kukubalika kwake na imani aliyojijengea mwanasiasa huyo kwa Watanzania.
Mwenyekiti huyo alifafanua kuwa katika kuteua mgombea, CHADEMA inazingatia vigezo na si suala la uteule.
Na wakati akisema hivyo, aliyekuwa mgombea ubunge katika jimbo hilo katika uchagzu mkuu uliyopita, Joshua Nasari, alisema endapo Dk. Slaa ataamua kugombea na chama kikampitisha, ataridhia.
Uchaguzi huo unaotarajia kufanyika Aprili mosi mwaka huu, umetokana na kifo cha aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Jermiah Sumari (CCM).
Tayari harakati za kuchukua fomu zimeanza ndani ya vyama vya siasa huku kila kimoja kikitamba kulinyakua hasa mchuano mkali uko kwa CCM na CHADEMA vinavyopewa nafasi kubwa ya ushindi.


 
Mmh nape hamna k2 apo..izo ni dalili waza anajua Slaa akigombea anapita so anatanguliza vitisho jembe lisigombee...
 
Nnauye Nape!gambaz vp wahusika washavuliwa gambaz,au ulimaanisha wamepewa miaka 90 na si siku 90?
 
Mnamuongelea nnauye yupi?

Kama ni yule mtoto wake wa singida hana kitu ila kama ana mwingine tuanze kujadili.
 
Mie sipo nilikuwa napita, HATAHIVYO DR Slaa alishasema hawezi kurudi nyuma, HIVI Leo anapokea m,ilioni 12 pasipo kodi, ubunge atapokea hizo na kodi juu
 
Ndg yangu Nape chunga kauli zako za kuropoka, unajishushia heshima. Hii inakuongezea nini kwenye kazi yako ya itikadi na uenezi wa CCM? Watch it out brother!
 
Nape amesema ukweli kabisa, na Slaa alishaona hii lasivyo angejitokeza kugombea hicho kiti.
 
Nape ajui kuwa Slaa ana kisimat umaarufu wake hauwezi kushuka kwa ubunge wa Arumeru, anaogopa kiama cha si si em iwapo Dr. atagombea 2015. Tayari homa ya uchaguzi 2015 ishampanda na anajua kitakachotokea ktk chama chake ndio maana anajihadhari mapema.
 
Nape anafanya kazi yake ya kichama tuache dharau na matusi....hata SIMBA na YANGA huwa wanatambishiana hivyo hivyo .Binafsi sipendi matusi na dharau kwa bwana NAPE. NAPE amethubutu kupambana na LOWASA wazi wazi ,huku wengine tukiishia kusema MAFISADI.Je Mafisadi hawana majina? Pia NAPE ameweka ID yake humu JF bila kificho huku wengine tukijificha nyuma ya PAZIA,je hapa nani MNAFIKI ?????????????????

NAPE anaweza kujenga chama akipewa rungu bila kuhofia usalama wake...BRAVO NAPE
 
Nape amepinda kweli. Hebu aende yeye na sisi tumpeleke slaa aone moto wake.kumbe nnape sio katibu mwenezi wa sera ma itikadi tu. Pia ni mwenezi wa uzush na propaganda ccm mhh amekwisha.
 
Back
Top Bottom