NAPE, MBOWE NA Dr SLAA KATIKA MAZISHI YA MPIGANAJI BOB MAKANI

Hapana Elizabeth Dominic nafikili hii picha uliyoitumia ndio imenifanya nitake kukufahamu zaidi, Nafikili sio kosa, ni muhimu member kufahamiana!

Sio "nafikili" ni "nafikiri".

Umenikumbusha kijana handsome aliyekuwa anatongoza lakini hana habari ana gaga la kamasi limeganda kwenye sharubu, demu anacheka, yeye anafikiria kapenda nyimbo zake kumbe anamcheka lile gaga.
 
kwenye msiba hakuna uadui ,wote ni kitu kimoja,maana pale ndipo tunakumbuka kuwa sisi wote ni marehemu watarajiwa!
 
Kwenye mazishi ya kanumba kulikuwa na picha Ridhwani anacheka na kina Steve Nyerere na Ray. Watu walichonga saaaaana, oooh watachekaje kwenye msiba na maneno mengine meeeeeengi. Leo naona watu wako kimya kuhusu kucheka!!! Zis is vere interestingi!
 
Nimekumbuka enzi za Mwalimu ambapo wagombea wa ubunge walipanda gari moja na wote walihutubia pamoja. Unafiki huu wa Nape Tusingeuona inaelekea Nape anawasema viongozi wa CDM vibaya huku anawapenda coz wako mbali nae! Mh Mbowe utafikiri anamshangaa Nape na kusema si ndo huyu katutukana Jumamosi CHADEMA SQUARE?

We kwa kuangalia umeongozwa na ushabiki...kuona mnafikki ni Nape tu na sio magwanda hao wawili..? Duuu....what a shame
 
Mchezo wa Siasa ni zaidi ya watu wa kawaida tujuavyo!!.
(Picha kutoka Michuzi blog)

We bwana weee. Siasa ndivyo zilivyo. Mashabiki watatoana roho lakini wahusika wenyewe wanakorogeana vikombe vya kahawa wanapokutana. Achana na wanasiasa, ujijali wewe na maisha yako. Wakipata hawageuki nyuma ila kuwawekea uzio msije mkawafuata mkawa kama wao kupeleka ushindani mwingine. Wanapingana na wala hawapigani. Sio maadui ila ni ni competitors for the rivalry. Maneno ya kwenye majukwaa ndiyo sehemu yao ya kuishi, wataishi kwa maneno hayo lakini hawatatenda kamwe wayasemayo. Wale wote wtendao kile wanachokisema hawadumu katika siasa.
 
Maisha Yanaendelea.JPG
Maisha Yanaendelea...Mkuu wa nchi na mkuu wa nchi kivuli...Protocali Ikafuatwa....
 
View attachment 56153
Maisha Yanaendelea...Mkuu wa nchi na mkuu wa nchi kivuli...Protocali Ikafuatwa....

Kwa hapa inabidi tutofautiane kidogo. Katiba ya nchi haina kipengele kama hiki bali inatambua kiongozi kivuli mkuu wa sughuli za bunge na katika vyama vya siasa, Mheshimiwa Freeman Mbowe ndiye anawadhifa kama wa Mwenyekiti ya CCM.
Ingekuwa vizuri ukaifafanua sentesi yako kwa sababu hata katika protokali, anayekuwa kulia huwa ndiyo anayefuata baada ya mkuu. Angalia hata jinsi walivyokuwa wamekaa katika msiba.
 
Siasa siyo uadui. waungwana ,jaribuni kufuatilia siasa za Ulaya Magharibi na Marekani
muone Wanasiasa wanavyozungumza na kufurahi pamoja bila kujali Itikadi zao za kisiasa.

Umesema kweli mtemiwaWandamba. Unajua wabongo wengi wanafikiri siasa ni uadui. Siasa ni sera, hivyo kutofautiana sera na itikadi haifanyi kuwa maadui. Ni sawa na wapenzi wa Simba na Yanga. Haina maana viongozi wa timu hizo ni maadui bali wanatofautiana kwa sababu tu itikadi za timu zao na kwamba kila mmoja anataka yeye ashinde na mwenzake ashindwe. Jambo hili haliwafanyi watu hawa wasisaidiane katika shida au kushiriki katika mambo ya kijamii pamoja. Hivi si vita hizi ni siasa tu wapendwa.
 
Misibani ata maadui huwa kitu kimoja!
Kuna ile picha JK anampa pole Slaa nkasema Dah hii kali
 
Back
Top Bottom