Nape kupanda kizimbani Arusha kwa kutoa hukumu kabla ya jaji

Lokissa

JF-Expert Member
Nov 20, 2010
7,446
2,490
012nape.jpg

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye

Nnauye anadaiwa kutoa kauli kwamba wana uhakika wa ushindi wa Lema unaopingwa na wapiga kura watatu, wote wanachama wa CCM, utatenguliwa na mahakama na hivyo, kuwataka vijana wa chama hicho kujiandaa kwa uchaguzi mdogo utakaoitishwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Maneno hayo yanadaiwa kutamkwa na kukaririwa na Gazeti la Nipashe toleo la Oktoba 9, mwaka huu, ambalo pamoja na Nnauye, Jaji Aloyce Mjuluzi anayesikiliza shauri hilo pia alimwamuru mhariri wa gazeti hilo kufika mahakamani leo kuthibitisha iwapo kweli maneno yaliyoandikwa yalitamkwa na kiongozi huyo wa CCM.

Uamuzi wa Jaji kuwaamuru Nnauye na mhariri wa gazeti hilo kufika mahakamani ulitokana na hoja ya Wakili wa utetezi, Method Kimomogoro aliyeomba kesi hiyo isikilizwe na majaji watatu au watano kutokana na mteja wake kuhisi kuwa hatatendewa haki kwa sababu tayari CCM kimetamba kunyakua jimbo hilo kwenye uchaguzi mdogo hata kabla ya kesi kusikilizwa.

Kimomogoro alihoji kwa nini CCM iliyofungua kesi 14 za kupinga uchaguzi kati ya mashauri 44 ya uchaguzi yaliyofunguliwa na vyama vingine nchini kote, watangaze kujiandaa kunyakua Jimbo la Arusha iwapo hawajahakikishiwa ushindi mahakamani?

Wapiga kura watatu wanachama na wafuasi wa CCM, wanaoiomba mahakama itengue ushindi wa Lema kwa madai kuwa alitoa maneno ya kashfa dhidi ya aliyekuwa mgombea wa chama hicho, Dk Batilda Burian wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu uliopita ni Mussa Mkanga, Agnes Mollel na Happy Kivuyo ambao wanawakilishwa na Mawakili, Alute Mughwai na Modest Akida.

Katika kuhakikisha haki inatendeka, wakili huyo wa Lema alipomuomba Jaji Mkuu, Othman Chande kuteua majaji watatu au zaidi kusikiliza shauri hilo. Hoja hiyo ilimfanya Jaji Mjuluzi kumhoji wakili huyo iwapo kauli yake ina lenga kumwomba ajitoe kusikiliza shauri hilo linalovuta umati wa watu kila inaposikilizwa.

Hata hivyo, Wakili Kimomogoro alisema kilichomsukuma kufikia hatua hiyo ni mwenendo wa kesi hiyo na kwamba endapo wangekuwapo majaji zaidi ya wawili, anaamini kwamba haki ingetendeka pasi na kutiliwa shaka.Umati wa watu umekuwa ukifurika mahakamani hapo kila kesi hiyo inapotajwa kiasi cha wengine kulazimika kubaki nje kutokana na ufinyu wa chumba cha mahakama.

Hata hivyo, habari njema kwa wale watakaokosa fursa ya kuingia ndani ya chumba kitakachotumika kuendeshea kesi hiyo ni kwamba watapata fursa ya kusikiliza mwenendo wake kupitia vipaza sauti ambavyo Jaji Mjuluzi aliagiza vifungwe.

Source: Mwananchi
 
Nape anawapatia kweli chadema nimeamini,maana kwa jinsi anavyowashughulisha mpaka mnatia huruma;ndio maana mimi sina chama naangalia sera zipi zinanivutia kutokana na wakati uliopo ndio napiga kura!ndio maana niko huru kusema chochote na kumgonga yeyote kutoka chama chochote nikihisi anachemka....
 
Anawapatia kivipi sasa?
 
Uvuvuzela umemponza! Alitoa matokeo ya Igunga kabla ya Nec, alipoulizwa akaikana hadi id yake. Naomba wataalamu watuwekee hata ka kipande cha U tube tumwone alipotoa hiyo kauli.
 
Nape anawapatia kweli chadema nimeamini,maana kwa jinsi anavyowashughulisha mpaka mnatia huruma;ndio maana mimi sina chama naangalia sera zipi zinanivutia kutokana na wakati uliopo ndio napiga kura!ndio maana niko huru kusema chochote na kumgonga yeyote kutoka chama chochote nikihisi anachemka....

Habari yako mwana magamba mkereketwa
 
Nape amesema anacho kifahamu mumesahau maelekezo ya makamba kuagiza wb wote walio shidwa kwenye uchaguzi kwenda mahakamani ccm, polis, mahakama, tume ya uchaguzi, ni pacha sema mahakama wamechukiya nape kutowa sil mapema
 
Si tetesi sinasema amelazwa hosptal huyu??

Mkuu naona unachanganya kati ya orange and apple!alielazwa ni naibu katibu mkuu wa chadema,nape ni katibu muenezi wa ccm!hajalazwa juzi alikua na ugeni wa katibu mwenzake wa uenezi kutoka chama cha kikomunisti cha watu wa china,nilimuona kule kwa michuzi akimtembeza mgeni wake huyo kuanzia tazara mpaka majohe gongo la mbali kwenye makaburi ya wataalam wa kichina waliofia bongo!zitto ndio sijapata taarifa zake za jinsi anavyoendelea huko india!
 
Nape anawapatia kweli chadema nimeamini,maana kwa jinsi anavyowashughulisha mpaka mnatia huruma;ndio maana mimi sina chama naangalia sera zipi zinanivutia kutokana na wakati uliopo ndio napiga kura!ndio maana niko huru kusema chochote na kumgonga yeyote kutoka chama chochote nikihisi anachemka....
Mbona unasomeka! Maana sasa hivi hakuna aibu kubwa kama mtu kujitangaza kwamba ni MwanaCCM, unless uwe kiongozi ndio unajikuta huwezi kujificha, sisi wenye akili zetu tumekuelewa Mkuu hatutamwambia mtu kwamba wewe ni Gamba.
 
Anafanya kazi aliotumwa na wakubwa zake, kama hatumwi kwani tangu alivyoanza kuropoka kuna hatua zipi walizomchukulia zaidi ya kumsifia kijana anafanya kazi vizuri.
Waendelee hivyohivyo wanasema usimwamshe aliolala........! sasa waacheni wakizinduka tayari kumekucha
 
Back
Top Bottom