Nape, 'Kujivua Gamba' ni danganya toto??

"KUSHINDWA KWA DHANA YA KUJIVUA GAMBA"

imekuwa ni ndoto na dua ya mafisadi wengi na walafi wa rasilimali za nchi kwa faida ya matumbo yao kuona swala la wao kuwajibishwa kwa usaliti wao linashindwa! Ndo maana wanadhani wanaweza kujidanganya kwa kuimba tu kuwa limekufa.... HUWEZI DHULUMU HAKI ZA WATU NA UKAIMBA TU TENA KWA SHIBE YA KIFISADI KUWA ETI ZOEZI LIMEKUFA... Kama matamanio yote yangekuwa farasi basi kila masikini angepanda ili awe tajiri bahati mbaya sio!

SASA UAMUZI WA NEC ILIYOKETI APRIL MWAKA JANA ILIYORIDHIA MAGEUZI NDANI YA CHAMA( kujivua gamba).. KUHUSU SWALA LA MAADILI ILIAMUA.... VIONGOZI WOTE WANAOTUHUMIWA NA JAMII KWA UFISADI NA RUSHWA, WAPIME NA WACHUKUE HATUA ZA KUWAJIBIKA WENYEWE KWA KUONDOKA KWENYE VIKAO VYA MAAMUZI VYA CHAMA. WASIPOFANYA HIVYO CHAMA KICHUKUE HATUA YA KUWAONDOA BILA KUCHELEWA.

Wakati wa mjadala watu wakatajwa baadhi ya watu wanaotajwa sana na jamii hasa kwenye ngazi za juu kujihusisha na yanayosemwa kuwa ni ufisadi mkubwa ambao leo ukimwamsha Mtanzania yeyote usingizini ukamuuliza hivi matendo gani ya kifisadi unayoyajua makubwa nchini, bila shaka na bila kigugumizi atakwambia, RICHMOND, DOWANS, EPA, RADA nk. Na ukimuuliza kina nani wanahusika atakutajia majina bila kuuma maneno..

Na tukakubaliana KIKAO KINACHOFUATA TUTAFANYA TATHIMINI YA MWITIKIO WA WITO HUO WA WAO WENYEWE KUWAJIBIKA.... WENGINE WAKATAFISIRI SIKU TISINI, TUKAJARIBU KUFAFANUA LAKINI KWASABABU MAFISADI WANAPESA WASIZO NA UCHUNGU NAZO WAKAENDELEA KUPOTOSHA... SI NENO, TUKAKUTANA NOV. TATHIMINI IKASOMWA IKAONEKANA MWITIKIO SIO MZURI, JAPO TULIKIRI WAPO/ YUPO WALIOITIKIA MWITO HUO.

UAMUZI UKAWA SASA TUCHUKUE HATUA YA PILI YA KUWAONDOA KWANI YA KWANZA YA KUWAPA MUDA KUPIMA, NA NILICHUKUA MUDA MREFU KUPIGA KELELE KUTAKA KILA MMOJA ASIKIE ASIJE MTU KUSEMA SIKUSIKIA( nina hakika kwa wanyonge na wachukia ufisadi kelele zangu zilikuwa za kuamsha matumaini, lakini kwa mafisadi, kelele zangu ilikuwa ni kero kubwa ndo maana wanaziita uvuvuzela, am happy for that kwani lengo ilikuwa ni kuwakera pia mafisadi)..

SASA CHAMA KIPO KWENYE MCHAKATO WA HATUA YA PILI, NA JUZI MKITI WA CCM TAIFA, KASEMA " tuliamua jambo hili kwenye kikao na nila manufaa kwa chama, wanaosema ni la hovyo, wao ndio wa hovyo).

Wanaodhani limekufa wanajidanganya... Mafisadi wanajua hawana chao, sasa kama wanawadanganya ni kwasababu wanataka muendelee kuwasindikiza, kama shetani afanyavyo anajua kabisa mwish wake ni motoni lakini anadanganya watu ili aende nao

Nnauye Jr,
Nimefuatilia kwa makini majibu yako kwa leo.Binafsi nakuona mtu usiye na aibu hata kidogo!.na una mapenzi binafsi na chama ccm kuliko wananchi wa nchi hii wanaoumia kutokana na madhara ya ufisadi uliofanywa,na unaoendelea kufanywa na makada waandamizi ndani ya chama chako ccm.(nina uhakika wewe si mmoja wao).

Kama si mapenzi yako kwa ccm,nina imani kwa akili ya kawaida kabisa ungekwisha ondoka na kujiunga na chama kingine na huko ungeendesha mapambano ya dhati kumkomboa mtanzania kutoka katika haya matatizo ya ufisadi,pamoja na kupambana na mafisadi wenyewe
Kwa wigo mpana zaidi.kuliko hivi sasa ambapo saa nyingine tunashuhudia wengine wakikupiga marufuku hata kukanyaga jimboni kwao ili kufanya kazi za chama.(rejea tukio la igunga).

Nasikitika kuona jasho la kijana mzalendo kama wewe unavyojitambulisha likipotea kwa maneno ambayo hata wewe nafikiri saa nyingine unayasema bila kuwa na uhakika nayo.
Kama ndivyo hasa mkuu anachotaka ukiseme,nasema hivyo kwa sababu sijwahi kusikia kauli ya mwenyekiti wako popote pale katika hotuba zake,akitutaka watanzania tukuunge mkono katika vita hii dhidi ya ufisadi katika chama chako na taifa kwa ujumla.

Ebu jaribu kuwa kama yule kijana mwenzako wa ANC,Julius malema kule afrika kusini.maana wote mnapigana vita vya aina moja na tofauti yenu ni kwamba yeye amepata ujasiri wa kuthubutu ambao wewe umeukosa na hakika umeona jinsi umma wa vijana wa ANC walivyo nyuma yake.

Siasa za nchi hii kwa sasa zinahitaji vitendo zaidi kuliko uenezi majukwaani ukiwa umeshikilia kitambaa cha kufutia jasho.mfano halisi unauona kwa vijana wenzio kama kina Mnyika na wengineo wengi wanavyofanya siasa za kisasa kulingana na mahitaji ya wananchi wakiwa na makabrasha yaliyojaa kero za wananchi.bila shaka hata wewe unawakubali katika nafsi yako kama Nape nnauye,na unaweza kuwakataa pale unapokuwa jukwaani kama katibu mwenezi wa ccm

Kwa sasa unachokifanya watanzania tulio wengi tunakukubali,ila pia tunakuhurumia tunapofikiria aina ya watu unaopambana nao,pamoja na idadi yao ndani ya chama chako.kumbuka wengine waliwahi kutamka kwamba "mwenyekiti wako hawakukutana naye barabarani"..wewe hili ualichukuliaje komredi?.nakupa angalizo usije kuwa kama yule katibu mwenezi wa marehemu Saddam hussen wa Iraq (RIP). aliyekuwa akikanusha kipigo cha wamarekani ,walivyokuwa wakizidi kuikaribia Baghdad na hatimae akakoswa kombora la kichwa mbele ya kamera za television, akiendelea kukanusha,na hatimae akakamatwa wa kwanza kabla ya Saddam.

Watu wanakuita vuvuzela kwa sababu pamoja na kero ya ufisadi,ukiwa kama katibu mwenezi wa chama kikubwa kama ccm,mojawapo ya majukumu yako ni pamoja na kuwaeleza watanzania dira ya serikali ya chama chako,katika kutatua kero za wananchi zinazotukabili kwa sasa kama nitakavyoeleza kwa uchache tu.na si kila ukipanda jukwaani,ukihojiwa na press suala linakuwa moja tuuu!

Si wananchi wote hususan vijijini wanaoweza kuyaelewa madhara ya ufisadi moja kwa moja, hii ni nchi kubwa sana ikiwa na wapiga kura wengi sana ambao hata elimu ya uraia bado ni tatizo hivyo wanataka kuelezwa nini hasa dira ya ccm katika kupambana na kero kama rushwa na Wizi wa madawa katika mahospitali ya serikali (baadhi ya hospitali nchini) na kupelekwa maduka binafsi,jambo linalopelekea madaktari walio wengi kugeuka mawakala wa maduka ya binafsi kwa kutuelekeza wagonjwa maduka wanayopendekeza tukanunuwe dawa wanazotuandikia.

Kuna tatizo kubwa la kushuka kwa morali wa utendaji kazi, kwa walimu wetu nchini na ushahidi ni jinsi kiwango cha ufaulu kinavyozidi kuporomoka nchini mwaka hadi mwaka je unafikiri nini kifanyike ili kuokoa nchi na janga hili nyemelezi,

Tunaambiwa kilimo kwanza, na hata bendera ya chama chako ni jembe na nyundo,(ingawa yule kijana pale mwanza katika kipindi asubuhi alitoa hoja kwamba iongezwe na picha ya noti akikueleza maoni yake live star tv)serikali inaanza kununua zana nyingi za kilimo bila kwanza kufanya utafiti na kuleta wataalamu wa kilimo cha umwagiliaji kwanza,kwani tatizo kubwa la mkulima wa tanzania pamoja na uduni wa zana lakini zaidi ni tatizo la uhaba wa mvua.nafikiri na wewe ni shahidi kwa hilo.

Lakini kubwa zaidi nimalizie kwa kukumbusha kuwa ccm na serikali yenu mnatakiwa kudhibityi mfumko wa bei na kushuka thamani ya shilingi,pia mtueleze kwa nini nchi yetu bado inatumia sarafu mbili?

kwa haya machche niliyoyatoa kwako ninaomba walau unijibu ili wananchi wengi tuendelee kukuombea mungu akupe uzima na ufanikiwe katika vita hii kubwauliyonayo mbele yako.

Kila lakheri.
 
Nape hivi ni kweli mnataka kumpitisha Lowasa we mgombea wa urais 2015? naomba tu unijibu straight kwani lisemwalo lipo na sisi sio watoto wadogo tumeshaona speed ya Lowasa. na je mtatumia mbinu gani kumzuia asigombee au asipite ?
thanks!
 
Kwanza sina kambi, nimewaomba kila mara kusema kambi yangu ipi, kila mara wanababaika tu, mara Sita, Ben, Mwandosya, Mwakyembe, Sumaye, nk. Niambie fisadi gani niliyembagua na kwamba namkumbatia...
Wengine wanadhani msimamo huu nimeanza jana, Mwaka 2008 nilipozungumza na kuokoa mkataba wa hovyo UVCCM nilisema... KWA SWALA LA UBADHIRIFU, UFISADI NA RUSHWA HATA ANGEKUWA BABAANGU MZEE NNAUYE NINGEMSEMA MPAKA AACHE.
Sawa kabisa mkuu Nape¡ hivi kukemia ufisadi bila kuchukua hatua za kisheria ndio njia sahihi ya kukomesha ufisadi naomba ufafanuzi wako .Kimsingi mimi ni ccm mwenzako lakini hapa kwenye issue hii ya mafisadi naona kuna tatizo kubwa ambalo tusipokuwa makini hali ni tete mno
 
Kakaangu Kiungani,

Nashukuru sana, nimekusoma na nimepata muda kurudia tena na tena makala yako, naomba nikushukuru kwa dhati kabisa ya moyo wangu. Ushauri ulioutoa nitaufanyia kazi.

Nina swali moja tu, ungekuwa wewe kwenye nafasi yangu kwa swala lolote chukua mfano wowote wa matumizi mabaya ya rasilimali za nchi KAMA KATIBU MWENEZI WA CHAMA UNGEFANYA NINI CHA ZIADA ZAIDI YA NILICHOFANYA MIMI?
 
Commonmwananchi,

Nakuomba sana sana wewe na mwingine yeyote ambao bado mnaamini hoja kuwa Nape alipigwa marufuku Igunga mnijibu maswali haya mawili;

1. Ni uchaguzi gani mdogo toka tumeanza chaguzi ndogo nchini chini ya mfumo wa vyama vingi ambapo Katibu Mwenezi wa CCM ameenda kwenye kampeni na akakaa huko mwanzo mpaka mwisho??

2. Hivi mbona Igunga ndo inaulizwa ni kwanini juzi hamjauliza Uzini na nahakika hamtauliza Arumeru Mshariki? Bila shaka unaona hoja hii ilitokana na kuanguka kwa mbuyu ulioasisi matumizi ya pesa kwenye chaguzi, yeye na wapambe kutoamini kwamba sasa wanafikia mwisho?
 
Sawa kabisa mkuu Nape¡ hivi kukemia ufisadi bila kuchukua hatua za kisheria ndio njia sahihi ya kukomesha ufisadi naomba ufafanuzi wako .Kimsingi mimi ni ccm mwenzako lakini hapa kwenye issue hii ya mafisadi naona kuna tatizo kubwa ambalo tusipokuwa makini hali ni tete mno

Makupa,
Vaa viatu vya Katibu wa Itikadi na Uenezi kisha nambie ungekuwa wewe ungefanya nini cha ziada kuliko nilochofanya mimi kwa kesi inayoitolea mfano na kuiulizia swali?
 
Commonmwananchi,
Umeuliza maswali ya msingi sana kwa hali ya nchi yetu. Nitayajibu kadri niwezavyo..... Lakini la kwanza si kweli kwamba eti kila nikisimama au kuulizwa swali nazungumzia Ufisadi tu, si kweli! Japo naamini ufisadi( kwa tafisiri ya matumizi mabaya ya rasilimali za nchi kwa faida ya mtu binafsi au kikundi kidogo cha watu) ndio msingi mkuu wa matatizo mengi nchini, kwahiyo badala ya kubaki kukata matawi, bora kuchimbua mzizi kabisa. Hili linawakera wengi ndo maana huniita vuvuzela kwa maana sauti ya vuvuzela inakereketa masikioni.
 
Commonmwananchi,
Umeuliza maswali ya msingi sana kwa hali ya nchi yetu. Nitayajibu kadri niwezavyo..... Lakini la kwanza si kweli kwamba eti kila nikisimama au kuulizwa swali nazungumzia Ufisadi tu, si kweli! Japo naamini ufisadi( kwa tafisiri ya matumizi mabaya ya rasilimali za nchi kwa faida ya mtu binafsi au kikundi kidogo cha watu) ndio msingi mkuu wa matatizo mengi nchini, kwahiyo badala ya kubaki kukata matawi, bora kuchimbua mzizi kabisa. Hili linawakera wengi ndo maana huniita vuvuzela kwa maana sauti ya vuvuzela inakereketa masikioni.

Hujawahi kula 10%?
 
huyu nape aache kutuongopea,tunajua kabisa uko bias kwenye mambo mengi,kuna ushahidi wa sms ambazo ulikuwa unatumiwa na mwenyekiti wako kutukana watu je hapo unatumikia chama au mtu? pia mmekuwa mkimtaja lowassa kama ndiyo fisadi je rais unayemtumkia na usafi gani au kwa kuwa ndi kashika mpini? pia umekuwa ukitukana matusi watu mara kwa mara opale ambapo wamekuwa wakipinga hoja za msingi,ushahidi wa matusi ninayo,mi nafikir bado wewe ni mchanga kwenye siasa usikubali kutumika pia kubali mawazo ya watu hayo ndo yatakujenga kisiasa..
 
Commonmwananchi,
Hivi niambie ukweli bila kujali itikadi ya vyama vyetu, hivi morale ya kazi inatoka wapi kama wafanya kazi wataendelea kuona baadhi ya watu waliopewa dhamana wakijitajirisha kwa kutumia ofisi za umma bila hata kunyooshewa kidole?
Hivi madaktari na wengine wanaoiba dawa za hospitali wataachaje huku wakiona na kushuhudia wajanja wachache wakineemeka wao na watoto wao bila huruma na wao wakiendelea na tumishahara tusitofika mwisho wa mwezi?
 
Hujawahi kula 10%?
Zomba si vizuri kujisemea lakini mwenye ushahidi alete hapa! Unadhani natoa wapi ujasiri kama ningekuwa na doa la kifisadi, mie si mkamilifu lakini si kwa kula rushwa wala kutumia dhamana na ofisi au cheo vibaya
 
huyu nape aache kutuongopea,tunajua kabisa uko bias kwenye mambo mengi,kuna ushahidi wa sms ambazo ulikuwa unatumiwa na mwenyekiti wako kutukana watu je hapo unatumikia chama au mtu? pia mmekuwa mkimtaja lowassa kama ndiyo fisadi je rais unayemtumkia na usafi gani au kwa kuwa ndi kashika mpini? pia umekuwa ukitukana matusi watu mara kwa mara opale ambapo wamekuwa wakipinga hoja za msingi,ushahidi wa matusi ninayo,mi nafikir bado wewe ni mchanga kwenye siasa usikubali kutumika pia kubali mawazo ya watu hayo ndo yatakujenga kisiasa..

Rafikiangu Naninibaraka,
Kwanza kama una msg hata moja hiyo iweke hapa jamvini nami nitawajibika ukitoa ushahidi ni mawasiliano yangu na bwana mkubwa juu ya maelekezo ya kuwatukana watu kama unavyosema.( kukusaidia tu, huu ni uzushi unaosambazwa na kitoto kimoja cha kifisadi kudhani kitachafua image yangu na kuonekana eti sijui nifanyalo).

Hayo matusi unayosema ni yapi nimetukana watu eti kisa sikubaliani na hoja zao! Uchanga huo wa kisiasa ni upi? Kama ukomavu ungekuwa ndio sifa ya busara tunao wangapi watu wazima wakomavu lakini tunashuhudi wanavyokoroga mambo?
 
Matusi kwa kiongozi mwnye dhamana kama wewe hayajengi,wewe ulikuwa rafiki yangu sana tumefanya mambo mengi sn pamoja ingawa kwa sasa kimtazamo haupo na mimi, sikubaliani na style yako ya kazi,tofauti yako na mwenyekiti wako ni kuwa angalau wewe unaongea,lkn kmisingi hoja zenu zenu za kukurupuka,lakini style yenu ya kazi ni zima moto,sera yenu ya kujivua gamba ili fail kabla haijaanza niliwahi kukuonya kwenye hili ukanimwagia matusi ukasema napakatwa na mafisadi,nimehongwa na mafisadi,hii vita ya ufisadi ilipoanza wengine tulifurah na kuunga mkono kuwa angalau raslimali za nchi zitatunufaisha wote,badala yake hoja ikawa ya mtu mmoja[lowssa],lowassa hawezi kuwa fiasadi kikwete akawa salama tuna ushahidi wa pesa ritz 1 alizonazo na hata leo akiulizwa kapataje hawez elezea,sitta,msekwa,membe,ngeleja na wengine wengi ndani ya ccm ni mafisadi ,tatizo lako wewe na kikwete mnapenda sifa hampendi mawazo ya watu wengine,mnabaki mnapiga kelele za hovyo,hela za EPA ndo zilizomwingiza kikwete madarakni alafu leo unasimama jukwani unasema kikwete msafi,kwa taarifa tu ni kwamba kikwete hatokuwa salama baada ya 2015
 
Nape, mimi ninaamini kwa dhati unayo nia njema kabisa tena kutoka moyoni na hayo unayoyasema.
Lakini kutokana na mfumo na chama chako you're doomed to fail. Tofauti na wengine (CCM) wewe
UMEJARIBU.

Ndiyo maana hata hiyo falasa ya kujivua gamba mmebaki kuhamisha post (magoli) kila mnapokuwa confroted.
JK ataendelea kukutumia hivyo hadi atakapopata u-Uenyekiti wa CCM na hiyo falsafa itakufa kama Richmond.
HYPOCRISY ni SERA isiyo rasmi ya CCM, I'm warning, you're fighting a losing battle. Kwasababu Kidole kimoja
hakiwezi kuvunja chawa, very unfortunately you're alone ktk vita hii!
 
Chama chenu kingekuwa sio chama cha mafisadi (na wewe kwasababu upo kati yao) mngekuwa mnachukua hatua badala ya kuwatishia! Kama kweli mna uchungu na hii nchi na ushahidi juu ya hao mafisadi kilichotakiwa ni kuonesha mfano kwa kuwafukuza na kuwapeleka mahakamani!kwa kuwatishia eti wajipime then waondoke wenyewe ni kutupumbaza watanzania.ina maana kuna aina ya wezi ambao hupelekwa mahakamani na kushtakiwa na kuna aina ya wezi wa kujipima kama wana makosa na kuendelea kutamba mitaani?naomba ufafanuzi kwa hili.
 
Nape Naomba nianze kuwasilisha hoja yangu hasa kwa nyie mnaoiita vijana ndani ya CCM na nje kwa maswali.
  • Kwa nini unatumia VX na si vitara au Saloon kwa safari zako za Kiofisi hata uwapo dar?
  • Unaongeleaje juu ya viongozi wa CCM( Na wewe ni mmoja wao) na watendaji walioko serikalini kuonyesha kwa maneno kuguswa na matumzi mabaya ya fedha lakini ki vitendo wao wenywe ndio watumiaji wabaya wa pesa za umma au chama inagawa matumiz yao ni halali kisheria...... hawaoyeshi kuguswa wala kushtuuka wala kutaka kubadilika na ule mfumo wa status quo
  • Je heshima na status yako ya Uongozi kama katibu mwenzi au ya waziri au ya katibu mkuu itahadhirika kama mkipanda Vitara za umma au Saloon kutoka "Masaki"kwenda "Posta".
  • Kwa wiki na/au mwaka Kiongozi mmoja anaweza kuokoa shilingi ngapi kwenye matumizi ya mafuta kama akibadilisha VX yake ya ofisi ya umma kuwa Vitara au saloon ?
  • Unaonaje ukimshauri JK kuwa wewe Nape( katika kujivua gamba) unataka Vitara au Saloon na si VX ili uwe mfano wa viongozi kwa vitendo na anayeonyesh kuguswa na matumizi ?
BInafsi nashanga Chama chenu ambacho kinaongoza serikali Viongzi wake hawaguswi . Wazungumzaji wazuri majukwaani lakini utendaji ni tofauti. Utashangaa wizara inyojiita ya mazgira ina VX kibao kama wizira ya Ujenezi. Hivi wataamu wa wizara hii wanaguswa kweli na mazingira na carbon foot prnt achilia mbali matumizi. Jibu ni simple tatizo HAKUNA UBUNIFU. na kuzoea kufanya kazi kwa MAZOEA.

Nape nakushauri tena jaribu kwend mbali zaidi ya maneno jarbu kuishi mabadilio ya CCM unayotaka kama ni kweli. Anza kubadilisha uasfiri wako uwapo dar . Uwe mwalimu wa mawaziri na makatibu waliopo kwenye serikali yenu. Uwe mfano wa kupunguza matumizi yasiyo na Tija.

Nape umeweza kuonyesha mfano kiasi fulani kwani wewe ni mmoja wa wana CCM wachache sana ambaye hata wenye Pubic forum kama hizo upo na unjitahidi kjibu kero na kashfa na sa nyingine kukutaa na matusi. Lakini itapendeza atika falsafaya kjivua gamba na wewe unaweza kuonyesha mfano . Kwenye matumzi niemkupa mfano wa matumizi ya USAFIRI. Sasa ndani ya serikali ya CCM ni kama VX ndio image ya Uongozi.....

Onyesha mfano wa kuvua gamba la VX uwe mfano kwa vingozi wengine serikalini ambao hata safari za Mikoni wanapaa.Sasa VX za nini. Hivi sisi si masikini......

NB
Haya maelezo ni response katika swali lako ulilouliza baadhi ya watu wagekuwa on your shoes wangefanya nini. Onyesha mfano na wewe wa kujivua gambaili watu wakuelewe na tuuelewe vizuri kuwa dhana ya Kujivua gamba ni zaidi ya kuwaondoa baadhi ya WATU bali inaendana pia kurekebsha MFUMO na muundo fulani yasiyooneka kuendana na maadili ya Jamii na umasikini wetu ......

Ngoja niiishie hapa Kazi njema.....
 
Nova,
Waambie mafisadi, tafadhali fikisha salaam hizi kama ulivyozifikisha kwangu kutoka kwao, wao ndio watoke tu wawaombe radhi watanzania kwa unyama waliowafanyia badala ya kudhani hawana akili kiasi cha kutaka eti wanaowatetea wananchi ndio wakaombe radhi... Shame on you fisadis...

Kama unayoyasema hapa ndiyo ndiyo yanayo ujaa moyo wako,hongera sana na sisi watanzania tunahitaji sana vijana kama wewe.
 
Makupa,
Vaa viatu vya Katibu wa Itikadi na Uenezi kisha nambie ungekuwa wewe ungefanya nini cha ziada kuliko nilochofanya mimi kwa kesi inayoitolea mfano na kuiulizia swali?

Mkuu Nape chama ndio kinaunda serikali, na wewe kwa cheo chako ni mmoja wa vigogo kwenye nchi hii,sasa huoni ni muhumu sana nyie kama secretariet ya chama mkamshauri Mwenyekiti wa chama ambae hata katiba yetu inamruhusu kuchukua hatau stahiki kwa wale wote wenye matendo ambayo wewe binafsi tumekushuhudia ukiyakemea hadharani.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom