Nape kadhihirisha uongo wake Dodoma leo

Waliopinga kwamba Nape hakuongea hayo, hapa ni ushahidi zaidi kutoka gazeti la Haari leo, pamoja na kuchakachua habari lakini ukweli umebaki kama mada hii ilivyo

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimewataka wanachama wake na wananchi kuondoa wasiwasi kuhusu vikao vyake vya juu vinavyofanyika Dodoma.

Chama hicho kimesisitiza kuwa, dhana ya ‘kujivua gamba' ambayo inaendelea, haihusu watu watatu tu, ni pana, iliyosheheni mageuzi kuanzia chini hadi juu.

Chama hicho mbali na kukiri kuwa vikao hivyo vilivyoanza Jumamosi na kutarajiwa kumalizika Alhamisi vimesababisha hisia kali kwa wanachama, kimeonya kuwa hakitavumilia upotoshwaji wa habari kuwa ‘kujivua gamba' kunahusu watu watatu, wakati kuna mengi zaidi ya hilo.

Akizungumza jana na waandishi wa habari katika ofisi za makao makuu ya CCM mjini hapa, Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM, Nape Nnauye, alisema habari zinazotolewa zimekuwa zikipotosha kuwa vikao hivyo vinashughulikia watu watatu kwa maslahi aliyosema hajui ni ya nani.
 
natamani nigekua hapo karibu kama alivyo kaa huyo mwenye t shirt ya kaki, ningemchapa kelbu ndo akome kuongea uongo wake mara kibao alikua anawataja kwa majina leo waandishi ndo waongo waandishi ikifika mahali muwe mnawapiga kelbu viongoz wanoaongopa wanakera sana hawa
 
Kwa tabia anayoonyesha Nape sijapata picha Kikwete alimpa cheo cha Mkuu wa wilaya kwa vigezo vipi, maana mapungufu ni mengi mno.
 
wakisimama katika uhalisia na kuzingatia uboreshaji wa maisha ya MTZ wa hali ya chini, wangeweza kurudisha imani kwa wananchi, imani iliyopotea 2010.
 
Pamoja na kwamba kakana ID, tunajua ni ya kwake.
Mwenye link ya jinsi alivyokua akisisitiza hapa atuwekee please!!
 
kama ndo hivi, kweli nimeamini Lowasa nomaaa... Kweli nchi hii mafisadi wananguvu
 
Kibaya zaidi ni pale anaposahau kuwa kuna sauti kawa recorded akitamba kuwa hayo yalikuwa ni maamuzi ya chama. Ni bora angeomba samahani kuwa alikosea na si waandishi wa habari waliokosea. Na hata hivi karibuni alikuwa recorded akimsema Lowassa, sasa leo anakuja kuvilaumu vyombo vya habari.....shame on him.

Wenye vyombo vya habari nao wangemtaka awaombe samahani, tofauti na hapo wachunie stori za magamba. Tatizo la magamba wanaona tabu kuomba samahani pale wanapokosea. Kazi ipo kweli kweli.....na yeye anasubiri kuvuliwa gamba...watch.

Tanzania hakuna vyombo huru vya habari. Wamiliki wote wa vyombo vya habari ni makada wa ccm na hawana ujasiri wa kusimamia ukweli kwa gharama yeyote. Kwa ufupi ni wachumia tumbo.

Ingekuwa nchi zingine, mjadala wa kauli yake hii ungemfanya kuachia ngazi. Wangeweka clips za kauli zake zote alizowahi kutoa kuhusu mapacha watatu na upuuzi anaozungumza sasa.
 
n1.jpg
nape mnauye wakati akiongea na vyombo vya habari mjini dodoma leo ambako vikao vya chama cha ccm vikiendelea amebadilisha kuali mbiu ya awali aliyokuwa akizunguka nchi nzima kutangaza majina ya wanaotakiwa kuachia ngazi . Leo kaja na mpya kwamba vyombo vya habari vilipotosha ukweli wa maana ya kuvua magamba kwa maana ya kubadilika na wala si kuwafukuza watu. Hii imekaaje?waliopinga kwamba nape hakuongea hayo, hapa ni ushahidi zaidi kutoka gazeti la habari leo, pamoja na kuchakachua habari lakini ukweli umebaki kama mada hii ilivyogazeti la habari leo limeandika habari hii kama ifuatavyo
kichwa cha habari: kujivua gamba si lowassa, chenge, rostam pekee
chama cha mapinduzi (ccm), kimewataka wanachama wake na wananchi kuondoa wasiwasi kuhusu vikao vyake vya juu vinavyofanyika dodoma. Chama hicho kimesisitiza kuwa, dhana ya ‘kujivua gamba’ ambayo inaendelea, haihusu watu watatu tu, ni pana, iliyosheheni mageuzi kuanzia chini hadi juu. Chama hicho mbali na kukiri kuwa vikao hivyo vilivyoanza jumamosi na kutarajiwa kumalizika alhamisi vimesababisha hisia kali kwa wanachama, kimeonya kuwa hakitavumilia upotoshwaji wa habari kuwa ‘kujivua gamba’ kunahusu watu watatu, wakati kuna mengi zaidi ya hilo. Akizungumza jana na waandishi wa habari katika ofisi za makao makuu ya ccm mjini hapa, katibu wa halmashauri kuu (nec) ya ccm, nape nnauye,alisema habari zinazotolewa zimekuwa zikipotosha kuwa vikao hivyo vinashughulikia watu watatu kwa maslahi aliyosema hajui ni ya nani.mpaka sasa watu wanaolengwa na habari hizo kuwa 'watavuliwa gamba' alizosema zinapotoshwa, ni mbunge wa monduli, edward lowassa, mbunge wa bariadi magharibi, andrew chenge na aliyekuwa mbunge wa igunga, rostam aziz.
hili si msukule mwingine wa ccm majini yakimzidi anakimbizwa hospital
 
Back
Top Bottom