Nape kadhihirisha uongo wake Dodoma leo

[h=2]TUESDAY, JULY 19, 2011
NAPE NNAUYE ASEMA ROSTAM AMEFANYA JAMBO JEMA[/h]





Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, aliyasema hayo wakati akiongea na baadti ya waandishi wa habari wa Mbeya katika ukumbi wa Hotel ya Paradise amesema Chama hakina la kusema, lakini kikubwa ni kuwa amefanya jambo jema, kwa kuitikia wito wa Chama, uamuzi ambao ni mzuri na wa busara," alisema Nape. Kuhusu mkutano wa hadhara wa mjini Mbeya, Nape alisema unalenga kuwaelezea wanachama wa CCM na wananchi kwa jumla, juu ya mabadiliko ya uongozi ndani ya Chama, msingi wake ili waweze kuelewa, CCM imetoka wapi, ipo wapi na inakwenda wapi,



 
Wenye Chama chao wapo huyo si mpiga ramli tu! keleleleeee! Oooh lazima mtu aondoke tumewapa mda wafikirie!!!
Shame on you! With your blabber mouth!
 
Pale unapoamua kusimulia mambo ambayo yametoka kwa mtu kigeugeu, lazima kujiandaa kuyameza maneno yako...!
Bahati mbaya Nape aliingia nalo mzima mzima kwa kuwa aliamini sifa yote itakuwa kwake atakapofanikiwa! Alitaka kukubalika tena kwa gharama nyepesi kama hiyo!
Nadhani kwa kipindi alichokaa CCM alipaswa kujua kuwa ulikuwa mtego kwake, coz kila mmoja wao alikuwa makini sana katika kuliongelea hili la magamba, ila yeye kwa kupumbazwa na kupenda sifa, akajua amekuwa jiwe kuu la pembeni, akazunguka nchi nzima akilihubiri,ona sasa hivi anameza matapishi yake mwenyewe... Binafsi namsikitikia sana:embarassed2:, ila naamini anastahili alichovuna na wahenga walisema "the lesson learnt in pain is best remembered!" so hatasahau kwa urahisi tena!
Ni aibu kwake, na amejidhihirisha kuwa hafai kuwa kiongozi kwa kuwa hafikirii kabla ya kutenda(kusema) na muhimu zaidi kwa kuwa hawezi kusimamia kile anachokiamini!
 
Watanzania sasa muone Kiongozi kama Nape anadhubutu kukana maneno aliyoyatamka yeye mwenyewe na Kuwasingizia Waandishi wa Habari kuwa walimkariri sivyo, hii ni dharau kwa Watanzania na Waandishi wa habari kwa upande Mwingine.
 
Kumekuwepo na juhudi za muda mrefu sasa kutaka kupotosha au hata kushawishi kubadili kabisa maamuzi ya Chama juu ya dhana nzima ya kufanya mageuzi ndani ya Chama (KUJIVUA GAMBA).

Juhudi hizi zimekuwa zikifanywa na kikundi kidogo sana cha watu wachache ambao kwa namna moja ama nyingine wameathiri wanamageuzi haya tunayoyafanya.

Tatizo kakikundi kenyewe kana nguvu kiasi ya pesa jambo linalofanya kelele zao ziwe kubwa lakini zisizo na mashiko.
Juhudi hizi za kujaribu kuhujumu mageuzi haya ndani ya chama zimekuwepo kwa muda mrefu sasa na tumejitahidi sana kuzipuuza, lakini nadhani umefika wakati wana CCM na Watanzania kujua ukweli walau kwa kiasi ya kinachoendelea.
Wanaofanya juhudi hizi wanadhani hatuzifahamu kwa sababu tu tumekaa kimya wakati wakicheza sarakasi zao za kujaribu kuupotosha umma.

Chama tunafahamu na kufuatilia kwa makini kila kinachoendelea hakuna tusichokijua juu ya juhudi hizi na zingine nyingi zikiwemo jitihada za kutaka kumhujumu hata Mwenyekiti mwenyewe. Nasisitiza tunazifahamu.

Juhudi za hivi karibu ni zilikuwa za kutaka Chama kishindwe Igunga ili kujaribu kuhalalisha hoja ya kwamba mageuzi tuyafanyayo hayana tija kwa Chama. Juhudi hizi zilifanyika bila kificho, tunajua hazikuwa na nia njema kwa Chama ila zilisukumwa na uroho na ubinafsi zikiwa na ujasiri mkubwa wa kifisadi, bila kujali masilahi mapana ya Chama kama taasisi na nchi yetu kwa ujumla. Baada ya kushindwa kwa juhudi hizo Igunga, sasa wanaanza kujaribu kutumia watu mbalimbali kuimba wimbo wao wa zamani kuwa tunapotosha dhana ya kujivua gamba bila kusema usahihi ni upi kama tunachokifanya ni kupotosha.

Ikumbukwe huu sio wimbo mpya uliimbwa sana mara tu baada ya kutangaza maamuzi ya NEC.Bahati nzuri vimeshakaa vikao vya Kamati Kuu karibu mara mbili, ambavyo vyote vimepongeza utekelezaji wa haya mageuzi ndani ya chama.

Mapema mwaka huu Baraza Kuu la UVCCM Taifa chini ya Uenyekiti wa Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa katika taarifa yake kwa vyombo vya habari walipongeza utekelezaji wa maazimio ya NEC. Sasa pengine tujiulize kama wana CCM na Watanzania kwa ujumla hawa wanaodai tunapotosha maamuzi ya NEC ni kina nani na kwa masilahi ya nani?
Naendelea kusisitiza hakuna kilichopotoshwa.

Ushindi wa Igunga kwenye uchaguzi mdogo, pamoja na ule wa chaguzi ndogo za Udiwani kwenye kata kumi na saba kati ya ishirini na mbili zilizofanya uchaguzi ni uthibitisho wa kukubalika kwa mageuzi tuyafanyao.Nachukua nafasi hii kuwashukuru sana wa na CCM na wananchi kwa ujumla kuunga mkono mageuzi tuyafanyayo kwani Mwalimu alishatuasa "BILA CCM MADHUBUTI NCHI YETU ITAYUMBA"

Walikwenda na kauli mbiu Igunga "TUSHINDWE ILI TUHESHIMIANE" wakasahau kuwa Chama ni taasisi si mtu, ushindi ule Igunga na kwenye kata mbalimbali ni Ushindi wa wana CCM na wapenda nchi hii wote! …Hivyo basi "TUMESHINDA ILI TUHESHIMIANE" Bahati mbaya kwao hawa kutegemea kutokea yaliyotokea.
Nawasihi wasiweweseke watulie na kutafakari upya wayafanyayo huku wakikumbuka…HAKUNA TUSICHOKUJUA.

Nichukue nafasi hii kuwaomba wana CCM nchi nzima kutulia na kuzipuuza juhudi hizi kwani tukifanyacho ni kwa masilahi mapana ya Chama chetu na nchi yetu, hakuna sababu ya kutiwa hofu, kila kitu kiko salama.

SABABU YA KUSHINDA TUNAYO, NIA YA KUSHINDA TUNAYO NA UWEZO WA KUSHINDA TUNAO.
Malengo mengine makubwa waliyo kuwa nayo kupitia kushindwa kwa CCM Igunga kama kungetokea ili kuwa kuipa nguvu kampeni yao kubwa na ya muda mrefu ya kujaribu kujenga hoja ya kutenganisha Uenyekiti waTaifa wa CCM na Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Bahati mbaya kwao na wapambe wao mambo yamekwenda kinyume na dua zao. Changa moto ni nayo itoa kwao, kwa nini wasitoke wenyewe kutoa madai wayatoayo hadharani badala yake wanatumia watu?

Hii hoja ya kutenganisha kofia kama ina masilahi kwa chama nasi kwa kikundi kidogo kwa nini wanatumia nguvu ya pesa kutaka kushawishi wajumbe? Anayeamini kwa nini asiilete kikaoni bila kushawishi watu kwa pesa? Mwenendo wa siasa nchini unadhihirisha kuwa upinzani hauna nguvu kiasi hicho ila unapata nguvu ndogo waliyo nayo kutoka kwa kikundi hiki kidogo sana cha Wanaojiita wana CCM lakini kwa kweli ni waasi.

Wengi wao walianza kwa kuasi Imani ya CCM na sasa wana endesha kampeni ya watu kuasi maamuzi halali ya vikao halali vya Chama chetu.

Naomba niwakumbushe TULIAMUA,TUKAAHIDI NA TUTATEKELEZA HAKUNA KINACHOBADILIKA KWA SARAKASI ZA BARABARANI, WANAPOTEZA MUDA.
Yaliyobaki yanayofanywa na wapambe na wanaotaka kutumiwa ya kimaadili tutayashughulikia kwenye vikao.Chama cha siasa makini ni vikao.

Ahsanteni kwa kunisikiliza.
Imetolewa na:-

Nape Nnauye
KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA
ITIKADI NA UENEZI
12/10/2011
.
saini+ya+nape.jpg
 
Taaaanzania tanzaniaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa nakupenda kwa moyo woteeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee nchi yangu tanzaniaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa jina lako ni tamu sanaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa.. nilalapo naota UFISADIIIIIIIIIIIII, Niamkapo ni boranifeeeeeeeeeeee tanzania tanzaniaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa simpendi rais wakeeeeeeeeeeee
 
hata yeye hapo alipo kiroho kinamdunda.kwa sababu wanaotakiwa kuvua gamba hata yeye yumo kwa kashifa ya ccj.mia
 
Inafurahisha kuona kuwa sasa kijana ameanza kuelewa nini maana halisi ya kujivua gamba. Nape, usiogope kuuliza ili ueleweshwe vizur pale ambapo utakuwa hauelewi
 
n1.JPG


Nape Mnauye wakati akiongea na vyombo vya habari mjini Dodoma leo ambako vikao vya Chama cha CCM vikiendelea amebadilisha kuali mbiu ya awali aliyokuwa akizunguka nchi nzima kutangaza majina ya wanaotakiwa kuachia ngazi . Leo kaja na mpya kwamba vyombo vya habari vilipotosha ukweli wa maana ya kuvua magamba kwa maana ya kubadilika na wala si kuwafukuza watu. Hii imekaaje?

hahahahah,
kwenye habariLEO la Leo amesema'suala la kujivua Gamba c la cku 1'
 
hiyo picha imenifanya nicheke sana, inaonyesha huyo mwanahabari anameshanga mpaka anajiuliza niandikeje. wenyewe huwa wanasema ccm ina wenyewe, labda wenyewe wameshamfahamisha.
 
Back
Top Bottom