FortJeasus
JF-Expert Member
- Jan 19, 2012
- 603
- 397
Ndugu mchambuzi,kwa kuzingatia mfululizo wa mabandiko yako hapa jamvini umeonyesha dhahiri unaamini kuwa CCM kama taasisi ya kisiasa imekamilika.Kukamilika huko kunatokana na kuwa hazina ya nyenzo muhimu kama vile Katiba,Miongozo , Kanuni na Taratibu za Chama.Sote tunaelewa kuwa ,CCM, imerithi nyenzo hizo kutoka kutoka kwa mtangulizi wake,TANU.Katiaka maandishi yako, unaamini vile vile, kuwa, taasisi hiyo ina tatizo watu wenye matatizo ya kimaadili katika nafasi na ngazi tofauti .Sasa nini kimetokea kiasi kwamba mienendo ya wanachama imeshindikana kudhibitiwa licha ya uwepo wa katiba,miongozo na kanuni za chama?Je,hii si ashirio la wazi kuwa wanachama wake wa sasa wameshindwa kurithi tabia,silka na hulka za wana TANU wa wakati huo.Katika taaluma za oganaizesheni, tunafahamu kuwa taasisi ama oganaizesheni yoyote hulazimika kupitia hatua tano (5) muhimu katika makuzi yake :huzaliwa ,huanza ukuaji ,kisha hukua kwa kasi (exponential growth),halafu hubaki katika mkuo sawa kwa muda (constant growth) kabla haijalazimika ''kuchagua'' ama kufa kama itakosa nyenzo za kujiokoa, ama kujiumba upya ikipata nyenzo hizo ili kuepuka kutoweka.Kwa sasa,baadhi yetu tunaamini CCM ipo katika hatua za mwisho wa kifo maama haikui tena kiidadi na kimaadili.Baada ya CCM kufa,halafu sasa nyie mnaoamini katika misingi ya TANU mje mpate nafasi ya kukifufua chama chenu huku mkichukua hadhari ya kutenda makosa ya waandamizi wa sasa.Kwa sasa ,hakuna namna CCM inaweza kujiepusha katika kuuendea mwisho wake.Haiyumkini kuamini vinginevyo.