Nape: Hatutakabidhi nchi kwa wahuni

mwajua NAPE nikijana mwenzetu,sijui huwaanatumwa kama JINII.Kwa kujitoa muhanga ndiyo mwenyewe.najua huyu wetu tu,keshoutasikia naomba kujiunga na wapambanaji.
 
Kama kweli amesema hivyo itakuwa yeye ndio muhuni zaidi ,,,
alizunguka nchi nzima kuhusu kujivua gamba na siku 90 zake zimeisha mambo yako vilevile au zaidi ya alivyoyakuta yaani sasa ccm sio mafisadi ni majambazi hebu fikiria wale faru kule serengeti wameuwawa lakini hakuna hatua yeyote
 
Muda mfupi uliopita Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Nape Nnauye amefungua Baraza la UVCCM Wilaya ya Missenyi na kusema kuwa CCM haitakubali kukabidhi nchi kwa wahuni waliojificha katika makundi ya wanaharakati.

Nape kaongea point
 
Mfa maji haachi kutapatapa, wahenga walisema.
 
Muda mfupi uliopita Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Nape Nnauye amefungua Baraza la UVCCM Wilaya ya Missenyi na kusema kuwa CCM haitakubali kukabidhi nchi kwa wahuni waliojificha katika makundi ya wanaharakati.

Tatizo huyo bwana mdogo hajui hata anachokifanya. Ni takataka hii. Ni kauli za mfa maji. Zinalenga kufurahisha mabwana zake - Kikwete na mwanawe Ridhiwani.

Hata Salmin Amour aliwaita CUF wahuni. Akasema siyo kuingia Ikulu, hata kukaribia jengo la Ikulu ni haramu. Akamtaka Seif akitaka Ikulu akajenge yake Mtambwe, Pemba. Akawabambiza kesi ya uhaini washindani wake.

Akajiapiza kuwa akiona CUF wanakaribia Ikulu atakwenda kwa miguu yake kuwazuia wasifike. Haya ni maneno aliyoyazungumza mara kadhaa na akayarudia tena kwa mara ya mwisho mwaka 2002 mjini Dodoma. Leo CUF wako Ikulu, tena Salmin akiwa bado hai.

Hata Robert Mugabe alimwita Shingirai mhuni. Akasema anatumiwa na mabeberu wa Uingerea. Akasema hawezi kukaa naye meza moja. Lakini leo hii, ndiyo PM wa Zimbabwe.

Gadafi alitoa kauli kama hizo pia. Rais Satta alipokuwa kiongozi wa upinzani mtawala wa taifa lake, alimwita Mhaini. Leo yuko madarakani.

Ni vema Nape kabla ya kutumikia mabwana zake angetafakari kwanza haya. Lakini kwa kuwa anafikiri KIMASABURI hataki hata kuangalia nyuma. NAMHURUMIA.
 
Lakini niulize swali la kizushi! Hivi ukiwa unaoga mtoni akija mwendawazimu aka chapa lapa na nguo zako na wewe ukatoka nae baru huku uko uchi nani mwendawazimu?
Jamani tumuache Nape na maneno yake ya kujifariji kama amefiwa namkwe wake. Anataka kutuambia atashika vidole vya Watanzania siku ya kura?asubiri aone kati ya Ccm na watanzania wapenda maendeleo ni nani wahuni. Kwa taarifa aende Jangwani kesho akaone nomi itakayo kwenda kwa hiari na gharama zao bila kubebwa na malori na kupewa shilingi 5000 zinazotutesa kwa miaka 50
 
Nyie hajui nape ni kada wa chadema angalia tokea ameiongoza ccm amekuwa akiwasemea magamba indirect bila nape m4c haitafanikiwa namwomba Nape aendelee kumaliza ccm
 
Nilifikiri ugonjwa wa 'kulewa madaraka na kujisahau' hautampata, maana wengi chini ya utawala wa magamba wameathiriwa na ugonjwa huo ila ni dhahiri kuwa sasa naye ni muathirika maana dalili zote anazo..
 
Maneno yake kama ni kweli yawekwa kwenye kumbukumbu na yatatumika vema kule ICC siku ikifika.
 
Mie niliisha waambia humu ndani nchi haikabidhiwi kwa vikaratasi vinavyo tumbukizwa kwenye masanduku, ni zaidi ya hapo. Hicho ndicho wengi wenu hamjui na hamta kaa mjue hata siku moja

Mkuu hebu tujuze kwa Faida ya Taifa letu!!
 
Muda mfupi uliopita Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Nape Nnauye amefungua Baraza la UVCCM Wilaya ya Missenyi na kusema kuwa CCM haitakubali kukabidhi nchi kwa wahuni waliojificha katika makundi ya wanaharakati.

Hii nchi haihitaji kukabidhiwa na mtu au chama chochote bali ITACHUKULIWA na CHADEMA . Nchi si faili wala kapu la machungwa bali ni watu kwa maana ya waTZ ndiyo watakao ikabidhi kwa CHADEMA ; Nape ni ENTITY he can hardly count on anything ni sawa na sisimizi mmoja kujaribu kuzui kundi la nyuki ku- occupy mzinga.
 
Muda mfupi uliopita Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Nape Nnauye amefungua Baraza la UVCCM Wilaya ya Missenyi na kusema kuwa CCM haitakubali kukabidhi nchi kwa wahuni waliojificha katika makundi ya wanaharakati.
The simple truth!
 
Kwahiyo hata wahuni wakishinda uchaguzi ccm watakataa kukabidhi nchi kwa washindi?
 
Naamini kabisa kuwa Nape hawezi kuita watanzania wenzake wahuni

Usiusemee moyo mkuu! Aje hapa akanushe mwenyewe! Alishasema pia yeye si
mchagga hawezi kujiunga na CHADEMA. Ni huyu huyu ninayeona hashindwi kuita watanzania wengine wahuni. Ina maana vyama vyote vya siasa ni vya kihuni. Huyu kijana anapotoka kwa hili
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom