Halfcaste
JF-Expert Member
- Nov 28, 2010
- 972
- 215
Nimekusoma mkuu ila isije kuwa 'msumeno' sie walala wima tutashindwa kufanya kaziMimi mara nyingine ninaachwa mdomo wazi na uelewa wa watu wengine? Labda ni kupotoshaji wa makusudi. Zitto hajasema POSHO zote zifutwe. Anachopendekezwa kufutwa ni sitting allowance, kwa kiswahili posho za vikao na hili sio kwa wabunge tu bali pia viongozi wengine wakubwa serikalini na taasisi zake. Kitu gani kigumu kueleweka hapa hata kama umemaliza STD VII??
Wabunge wakiwa Dodoma hulipwa posho za aina mbili 1. subsistance allowance (posho ya kujikimu). Hii Zitto anasema iendelee kuwepo. 2. Lakini wakati huo huo hulipwa sitting allowance simply kwa kuhudhulia vikaovya bunge ambavyo kimsingi ni majukumu yao. Hii ndiyo Zitto anapendekeza ifutwe. Lakini watu wameanza kupotesha mantiki ya suala hili wakidai eti Zitto anapendekeza Posho zote zifutwe kama anavyoseme Nape Nnaye kwa mapolisi eti wakihamishwa wasipewa posho!
Halafu wanadai suala la posho ni la kisera na lipo kwa mjibu wa sheria, kwamba CDM hawapaswi kulipinga wafuate utaratibu kama wanataka kuzitoa wakati wanafahamu kwamba Wabunge wa Magamba wako wengi na ni wachumia tumbo wata vote against! Sasa Anne Makinda amesema atawalipa kwa nguvu hizo posho CDM na NCCR. Kama mlifikiri wana beep wameshaandika barua ya kuzikataa kwanini mnawashinikiza, si mchukue nyinyi mafisadi (CCM) tu.