Nape: Dr. Slaa anaiua CHADEMA

Kageuka

JF-Expert Member
Jun 22, 2012
241
59
DR. SLAA AMECHANGANYIKIWA: Nape
Adai amekubuhu kwa utapeli wa kisiasa
Amtuhumu kuiua Chadema
Asema si M4C tena bali ni M4D

Tarehe 28/10/2012 kumefanyika uchaguzi mdogo katika kata 29 kwenye mikoa mbalimbali nchini. Kata hizi zilikuwa wazi kwa sababu mbalimbali, hivyo kwa mujibu wa sheria ililazimika kufanya uchaguzi mdogo kujaza nafasi wazi.

Ukiacha matukio kadhaa ya vurugu, maeneo mengi uchaguzi umeenda kwa utulivu. Chama Cha Mapinduzi kinawapongeza wote waliofanya uchaguzi kwa amani na utulivu, huo ndio utamaduni wa watanzania, kushindana bila kupigana.

Muhutasari wa matokeo ya jumla unaonyesha kuwa TLP wameshinda kata moja(1), CUF wameshinda kata moja(1), CHADEMA wameshinda kata 5 na CCM imeshinda kata ishirini na mbili(22).

Kwa matokeo haya ambayo kwakweli yanatafisiri pana sana hasa ikizingatiwa kuwa mgawanyo wa kata ulikuwa nchi nzima basi matokeo haya yanatoa ujumbe wa jinsi CCM inavyokubalika nchini kwasasa.

Na pia ni uthibitisho wa kile kilichoitwa M4C(movement for change) kwa Chadema kuwa ni *kiini macho kisichokuwa na matunda chanya bali ni M4D ( movement for dealth). Na hii inatokana na aina ya siasa za hovyo *zinazoambatana na operesheni hii. Bila shaka sauti ya Watanzania kwa aina hii ya siasa imesikika bila kumumunya maneno.

Aidha kwa upande mwingine siasa za uongo,uzushi na ulaghai zilizotumiwa na vyama vya upinzani hasa Dr. Slaa kwenye kampeni hizo imekidhalilisha chama hicho na kudhalilisha utu uzima wa Katibu Mkuu huyo wa Chadema.

Mfano mzuri ni pale ambapo Dr. Slaa bila ya soni alipoamua kumzushia Rais na Mwenyekiti wa CCM kuwa kasafiri mpaka China eti kwenda kumuokoa mwanae ambaye kwa madai ya Dk. Slaa alikamatwa na madawa ya kulevya nchini humo.

Bila aibu Dr. Slaa alizusha uongo huo Tabora kwa wapiga kura huku akijua kuwa ni uongo, lakini hata hivyo uongo huo hauna sehemu kwenye kampeni hizo za udiwani. Wananchi walitegemea kusikia namna ya kutatua kero zao badala yake wakashuhudia mtu mzima akizusha ujinga wa ajabu.

Uongo huu na mwingine mwingi unathibitisha kuwa Dr. Slaa anazeeka vibaya kwani kila anavyoongeza siku hamu na tamaa yake ya kusema uongo ili kujiongezea umaarufu na kujenga chuki kati ya watanzania inaongezeka sana. Hakika TAPELI HUYU WA KISIASA, LICHA YA KUZEEKA VIBAYA SASA ANACHANGANYIKIWA.

Naamini mzigo aliotwishwa na wenzake unamlemea sana, hivyo namshauri awaachie vijana wajaribu kukiokoa chama hicho kinachoporomoka kwa kasi, vinginevyo wana Chadema waanze kuandaa matanga kwa chama chao.

Ukitazama mgawanyo wa ushindi huu utagundua kuwa, pamoja na Katibu Mkuu wa Chadema Dr. Slaa kwenda na kupiga kambi kanda ya ziwa ameambulia kata sifuri(0). Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kwa kutumia gari ya serikali alijikita kusini nako katoka kapa.

Nguvu iliyotumika kutoka kwa vyama vya upinzani hasa Chadema hailingani na ushindi walioupata. Wakati CCM ikiwa busy na chaguzi za ndani ya Chama wao wamezungusha viongozi wa kitaifa nchi nzima na matokeo ndio hayo.

Tunawashukuru sana Watanzania kokote nchini walioendelea kutuamini na kutupa dhamana ya kuendelea kuwaongoza na kutekeleza ilani yetu. Tunawaahidi utumishi uliotukuka.

Nape Moses Nnauye
 
Tarehe 28/10/2012 kumefanyika uchaguzi mdogo katika kata 29 kwenye mikoa mbalimbali nchini. Kata hizi zilikuwa wazi kwa sababu mbalimbali, hivyo kwa mujibu wa sheria ililazimika kufanya uchaguzi mdogo kujaza nafasi wazi.

Ukiacha matukio kadhaa ya vurugu, maeneo mengi uchaguzi umeenda kwa utulivu. Chama Cha Mapinduzi kinawapongeza wote waliofanya uchaguzi kwa amani na utulivu, huo ndio utamaduni wa watanzania, kushindana bila kupigana.

Muhutasari wa matokeo ya jumla unaonyesha kuwa TLP wameshinda kata moja(1), CUF wameshinda kata moja(1), CHADEMA wameshinda kata 5 na CCM imeshinda kata ishirini na mbili(22).

Kwa matokeo haya ambayo kwakweli yanatafisiri pana sana hasa ikizingatiwa kuwa mgawanyo wa kata ulikuwa nchi nzima basi matokeo haya yanatoa ujumbe wa jinsi CCM inavyokubalika nchini kwasasa.

Na pia ni uthibitisho wa kile kilichoitwa M4C(movement for change) kwa Chadema kuwa ni kiini macho kisichokuwa na matunda chanya bali ni M4D ( movement for dealth). Na hii inatokana na aina ya siasa za hovyo zinazoambatana na operesheni hii. Bila shaka sauti ya Watanzania kwa aina hii ya siasa imesikika bila kumumunya maneno.

Aidha kwa upande mwingine siasa za uongo,uzushi na ulaghai zilizotumiwa na vyama vya upinzani hasa Dr. Slaa kwenye kampeni hizo imekidhalilisha chama hicho na kudhalilisha utu uzima wa Katibu Mkuu huyo wa Chadema.

Mfano mzuri ni pale ambapo Dr. Slaa bila ya soni alipoamua kumzushia Rais na Mwenyekiti wa CCM kuwa kasafiri mpaka China eti kwenda kumuokoa mwanae ambaye kwa madai ya Dk. Slaa alikamatwa na madawa ya kulevya nchini humo.

Bila aibu Dr. Slaa alizusha uongo huo Tabora kwa wapiga kura huku akijua kuwa ni uongo, lakini hata hivyo uongo huo hauna sehemu kwenye kampeni hizo za udiwani. Wananchi walitegemea kusikia namna ya kutatua kero zao badala yake wakashuhudia mtu mzima akizusha ujinga wa ajabu.

Uongo huu na mwingine mwingi unathibitisha kuwa Dr. Slaa anazeeka vibaya kwani kila anavyoongeza siku hamu na tamaa yake ya kusema uongo ili kujiongezea umaarufu na kujenga chuki kati ya watanzania inaongezeka sana. Hakika TAPELI HUYU WA KISIASA, LICHA YA KUZEEKA VIBAYA SASA ANACHANGANYIKIWA.

Naamini mzigo aliotwishwa na wenzake unamlemea sana, hivyo namshauri awaachie vijana wajaribu kukiokoa chama hicho kinachoporomoka kwa kasi, vinginevyo wana Chadema waanze kuandaa matanga kwa chama chao.

Ukitazama mgawanyo wa ushindi huu utagundua kuwa, pamoja na Katibu Mkuu wa Chadema Dr. Slaa kwenda na kupiga kambi kanda ya ziwa ameambulia kata sifuri(0). Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kwa kutumia gari ya serikali alijikita kusini nako katoka kapa.

Nguvu iliyotumika kutoka kwa vyama vya upinzani hasa Chadema hailingani na ushindi walioupata. Wakati CCM ikiwa busy na chaguzi za ndani ya Chama wao wamezungusha viongozi wa kitaifa nchi nzima na matokeo ndio hayo.

Tunawashukuru sana Watanzania kokote nchini walioendelea kutuamini na kutupa dhamana ya kuendelea kuwaongoza na kutekeleza ilani yetu. Tunawaahidi utumishi uliotukuka.
 
Siasa ina utamu wake bana, hawa jamaa (Nape & Slaa) wakikutana bar, hutaamini. Kama baba na mwana vile.
 
Ni upuuzi mtupu, chadema inapaswa kiteue msemaji wa kuwajibu wapuuzi kama hawa kwa haraka mnyika yupo busy mno.
 
only83;

japo waliongea ni wala rushwa na mafisadi lakini kama kuna uhalisia flani ivi
ni lini chadema wataacha siasa za ukanda??
Hii ni fedheha sanaa..
 
Last edited by a moderator:
Kati ya Kata 26 zilizokuwa chini ya CCM, wamepata kata ngapi? Nape acha hesabu za ngumbaru. Pamoja na tume mbovu ya uchaguzi na kutumia green guard na jeshi la polisi na tiss bado kata zimepungua toka 26 mwaka 2010 mpaka 22 mwaka 2012! Na mume wenu Mamvi ndio anapiga jaramba hivyo mwaka huu waropokaji chu.pi zitawabana! Mliomwita Gamba sijui mtakimbia nchi!
 
Tangu lini Bwana Pampasi akawaa Katibu Mwenezi wa Chadema? Kushindwa au kufaulu kwa CDM kunamhusu nini? Angekuwa na akili angepingana na Mkiti wake? Mwenyekiti analalamikia rushwa yeye anasema ipo kwa kiwango cha chini sana!!"" I can not argue with this ........
 
Ukjipa moyo kutamu sana... Nepi anasahau kwamba, viti 2 tu ndio CDM ilitaka kuvilinda/kuviudisha (Romba na Mtibwa-Mvomero), nayo imeweza kuvitetea. CCM imepoteza viti 3 (ambavyo CDM imevipokonya kutoka kwa CCM). Sasa kimahesabu unapata nini? 3/5 x 100 = 60% (CDM imepanda) wakati CCM imeshuka (2/27 x 100 = 7.4%).
 
CORRECTION:
Ukijipa moyo kutamu sana... Nepi anasahau kwamba, viti 2 tu ndio CDM ilitaka kuvilinda/kuviudisha (Romba na Mtibwa-Mvomero), nayo imeweza kuvitetea. CCM imepoteza viti 3 (ambavyo CDM imevipokonya kutoka kwa CCM). Sasa kimahesabu unapata nini? 3/5 x 100 = 60% (CDM imepanda) wakati CCM imeshuka (3/27 x 100 = 11.1%).
 
Kageuka I THINK ITS TIME NOW FOR SLAA TO RETIRE,,
KWA CHADEMA TUITAKAYO YAMPASA AWE KAMA YULE MKWE WAKE MBOWE
YULE MUASISI WA CHAMA HIKI KITAKATIFU i.e MZEE MTEI
:smile: :smile:
 
Last edited by a moderator:
Nape ni wa kuhulumia kwa ushindi wa kununua ndo amtukane dr. Kama chaguzi zao za ndani tu wananunuana kiasi hicho je? Nnje ya uchaguzi unao washilikisha watu wa vyama tofauti hali ikoje?
We nape acha upuuzi wa kumtuka mzee mwenye umri sawa na babako, subili kiama chenu, tume huru ya uchaguzi, daftari huru ya uchaguzi,
We kalia kupaka calo right 2 na siku el akichukua nnchi tafuta pa kijificha utakunywa maji kwa kalai hafu kumbe na we ni mbulula tu.
 
Nape kwanini hizo kata zilizokuwa chini ya himaya yenu zimeenda upinzani?nilidhani ungekuja na sababu za msingi kwann kata zenu zimepungua badala ya kuja na propaganda
 
Nape mbona uelezei rushwa iliyokithiri wewe kila siku uko na Dr Slaa waswahili wanasema mfa maji haachi kutapatapa hivi wewe Nape mbona huongelei wale vijana wa CCm waliowavamia viongozi na wanachama wa Chadema kule Songea na baada ya mapambano makamanda walikamata gari lenye mapanga,marungu,mishale,Mundu na fimbo kibao hivi wale jamaa wa CCM walikuwa wanakwenda vitani au kupiga kura hebu tiririka Nape acha kutoa mapovu.

Ati uchaguzi umefanyika pasipo vurugu wakati mlisaidiwa na Usalama wa taifa,Polisi,Green Gard kupiga na kutishia watu pia unatakiwa upige mahesabu katika uchaguzi huu CCm Magamba mmepoteza kwani kumbuka Chadema ndio washindi kwa 60% na nyie Magamba mko na 11.1% kama hujakimbia hisabati hebu kaa chini then kokotoa nani mshindi.
 
I THINK ITS TIME NOW FOR SLAA TO RETIRE,,
KWA CHADEMA TUITAKAYO YAMPASA AWE KAMA YULE MKWE WAKE MBOWE
YULE MUASISI WA CHAMA HIKI KITAKATIFU i.e MZEE MTEI
:smile: :smile:
Kwa kosa lipi au kwa sababu ya mpuuzi 1 nape?achana unafiki chama si Dr Slaa bali wanachama.
 
Hizi za Nape ni propaganda za kizamani sana!CCM imepoteza kata 5 kwenye uchaguzi huu kwa wapinzani(27-5=22)LKN BADO NAPE ANAJIPA moyo kama wamefanya vyema zaidi ya CHADEMA?

Upinzani ingieni mitaani kushangilia ushindi wenu maana mmeongeza kata 5 zaidi!CCM wameshindwa vibaya kwenye uchaguzi huu na kama CCM wangekuwa chama madhubuti basi NAPE and his CO mnapaswa MUACHIE MADARAKA!
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom