Wile GAMBA
JF-Expert Member
- Sep 13, 2011
- 1,809
- 595
Chezeni michezo yenu yote wananchi tunasubiri 2015. ndiyo hapo Nape atajua ushindi wa kishindo ni kitu gani, wakichakachua kama kawaida yao tunawachakachua pia
Wapi nimejiita Great Thinker? Mie muuza kahawa tu.
Tunapambana kuiondoa rushwa wewe unashangilia ushindi wa rushwa, hivi Tanzanaia tutafika kweli??????Mbona mnakuwa wakali Pro-Chadema JF.
CDM ni maafa kanda ya ziwa, pongezi zipokeeni wana Nyamagana kwa kugundua udhaifu wa chama kilijichokita kwenye misingi ya ukanda na ubabe
Ndugu yangu Nape ujiulize ushindi huo una maana gani kwako hasa ukiangalia cahama chako kilivyokuwa na mikashfa ya kukumbatia mafisadi, ningeona unafanya furaha nzuri kaama falsafa yenu ya kuvua gamba ingefanikiwa walau hata kwa asilimia 0.5. Hapo hatuchezi ligi ili bingwa apate kombe bali ni vipi tunaweza kuwahudumia wananchi kwa fursa za kiuongozi tunazopewa.
Friday, September 28, 2012
*Asema Dk. Slaa ameikimbia Mwanza mapema baada ya kunusa Chadema kugaragazwa
*Awapongeza madiwani wa CCM wa Nyamagana kwa kuwezesha ushindi wa Menya na Naibu Meya Nyamagana
NA MWANDISHI WETU, MWANZA
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, amesema dalili za kubwagwa kwa CHADEMA ndizo zilizomkimbiza mapema jijini Mwanza, Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Willbroard Slaa.
Amesema kushindwa kwa Chadema katika kinyang'anyiro cha Meya na Naibu Meya, ni mavuno ya ubabe wa viongozi wa chama hicho ambao baadhi wanazeeka vibaya.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa, Nape (pichani) alisema kwamba, Slaa alikimbia baada ya kuona maji yamezidi unga.
Nape aliyetumia fursa hiyo pia kuwapongeza Madiwani wa CCM wa wilaya ya Nyamagana na Chama kwa ushindi wa Viti vya Meya na Naibu wake, alisema Dk. Slaa anazeeka viba ndiyo maana naongoza chama hicho kwa ubabe na maandamano ya kila mara.
"Babu (akiwa na maana ya Dk Slaa) alisema CCM Mwanza itaondoka madarakani, imejidhihirisha wazi katika uchaguzi wa leo kuwa CCM bado ina nguvu na ni Chama kikongwe kisiasa, vingine vinaiga."
"Chadema wameona mavuno ya ubabe wao japo kura za CCM ni ndogo…., Babu ajiulize kwa nini ameshindwa kwenye uchaguzi huo wa Meya na Naibu Meya." Alisem Nape na kuongeza kwamba, kutokana na dalili za kushindwa zilizoonekana mapema, ndiyo maana Dk Slaa alikimbia Mwanza mapema.
Akiwapongeza madiwani hao kwa ushindi alisema kwamba wamefanya kazi kubwa na ya ziada kuhakikisha CCM inarejesha Halmashauri ya jiji hilo mikononi mwake baada ya kushikwa na Chadema kwa kipindi kifupi na hivyo kuwataka wana Mwanza wawe na mshikamano na kuwapa ushirikiano viuongozi wao.
"Nawasihi wananchi wa Mwanza wawe na mshikamano na kuacha maandamano yasiyokuwa na msingi, badala yake wafanye maandeleo, waimamini CCM sasa inachokuja kufanya ni cha uhakika." Alieleza Nape.
POSTED BY: BASHIR NKOROMO AT FRIDAY, SEPTEMBER 28,
Nbimependa comment yako, I feel the same wayIdadi ya madiwani iko wazi, Hapa pongezi wape wale madiwani waliosaliti chadema na kufukuzwa na kufanya idadi ya ccm na cuf kuongoza.Ila cha msingi ni kwamba cdm ni chama pekee kinachofanya maamuzi magumu, tuko tayari kupoteza hata jimbo zima kuliko kuwa na viongozi mamluki ndani ya chama chetu makini.Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
Mkuu wa MKOA wa MWANZA ndie alieyeanza kuwapa hongo MADIWANI WA CHADEMA wa Kuchaguliwa ili
Wabadilishe kura zao kuchagua Mwana CCM as MAYOR... na tatizo walilonalo CHADEMA Mwanza na ILEMELA
Idadi ya madiwani iko wazi,
Hapa pongezi wape wale madiwani waliosaliti chadema na kufukuzwa na kufanya idadi ya ccm na cuf kuongoza.
Ila cha msingi ni kwamba cdm ni chama pekee kinachofanya maamuzi magumu, tuko tayari kupoteza hata jimbo zima kuliko kuwa na viongozi mamluki ndani ya chama chetu makini.
Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
CDM ni maafa kanda ya ziwa, pongezi zipokeeni wana Nyamagana kwa kugundua udhaifu wa chama kilijichokita kwenye misingi ya ukanda na ubabe
porojo zingine sasa kama mlikuwa mnayajua hayo kwa nini dr slaa alienda mwanza.
Mkuu wa MKOA wa MWANZA ndie alieyeanza kuwapa hongo MADIWANI WA CHADEMA wa Kuchaguliwa ili
Wabadilishe kura zao kuchagua Mwana CCM as MAYOR... na tatizo walilonalo CHADEMA Mwanza na ILEMELA
cdm isiwavumilie mamluki hata kama, itamaanisha kushindwa 2015, bora tushindwe kuliko kushinda tukiwa na watu wenye akili za ki-ccm ccm
ninazo kumbukumbu kuwa nccr likumbwa na kundi kubwa la mamluki mpaka kikasambaratika;kwamba karibu asilimia kubwa walikuwa wanachama wakutengenezwa na ccm na usalama wa taifa ambao walipandikizwa nccr kupanga na kutekeleza migogoro ili kisilete upinzani wa dhati kuipumulia ccm karibu.hayohayo yamefanyika kwa cuf mpaka sasa haielewiki kule visiwani zanzibar na pemba kama bado chama cha upinzani .haya pia yalitegemewa kwa cdm yatokee,sikweli kabisa kundi kubwa linaloshabikia cdm ni wahafidhina wa upinzani, wengine mamluki na wachumia tumbo.weamekuwpo lutekeleza mipango ya ccm na usalama wa taifa kuidhofisha cdm, ili ccm iendelee kutawala milele.hapa nape hana cha kujivunia, chaguzi kama za meya si kioo cha kuonyesha imara wa ccm, bali mbinu chafu kuionyesha jamii kuwa bado kinapendwa na umma.swali jamii itarudisha imani ya kutumikia wanyonge kwa kushinda umeya huku ukirubuni madiwani wa cuf na baadhi ya mamluki wa chadema?kwa sasa nape angejitahidi kuwatumikia wanyoge waliopoteza imani na serikali yao badala ya kujidaganya na viuchaguzi vya hila kama ngao kwa umma, wakati ukweli hali si nzuri.serikali hiyohiyo ndo imesababisha chama cha ushirika kufirisika kwa kumtumia dalali ambaye alikuwa mbunge wa ccm kuhujumu ushirika huo kwa kuuza mali za ushirika, hivyo kuwafanya wakulima kwa sasa kupata bei duni .huyohuyo mbunge wa ccm magu dr.limbu amekuwa msitari wa mble kuwakejeri wakulima wa zao hilo bila kkuishauri serikali itie mkono kuwasaidia wapate bei nzuri.kwa hiyo nape kujiridhisha kwa uchaguzi wa meya kama msingi wa maisha ya wana mwanza ni kukumbatia utoto.