Nape: CHADEMA iwajibike matukio ya mauaji

KAUMZA

JF-Expert Member
Aug 31, 2010
699
237
Katibu wa itikadi na uenezi wa CCM, Nape Nauye, leo atazungumzia mauaji ya Mwangosi katika Star tv.

Ninatafakari, atakuwa na jipya gani? Kama tuliilaani serikali ya makaburu kwa mauaji ya Sharpville na yale ya Soweto(hatukulaani polisi wa Afrika kusini) ambayo yote yalifanywa na polisi wa Afrika kusini, vipi mauaji ya Mwangosi(Iringa), Morogoro na Arusha, tusiilaani Serikali ya CCM?

Polisi ni agents tu. CCM ndo wakulaaniwa na kubebesha mzigo.

Angalia: mazuri yote yanayofanywa na serikali, wanasema ni ya kwao. Vipi wajitenge na mabaya yanayofanywa na serikali?

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) imekitaka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuwajibika kutokana na kuwepo kwa matukio ya watu kupoteza maisha yanayosababishwa na maandamano ambayo yamekuwa yakifanywa na wafuasi wake.

Kauli hiyo imetolewa jana mjini hapa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, wakati akizungumza na waandishi wa habari.

"Chadema wana kila sababu ya kuwajibika, kwa sababu matukio haya ya mauaji yamekuwa yakitokea kwenye operesheni za mikutano yao na matukio ya aina hii kutokea katika kazi za chama cha siasa ni aibu, hivyo viongozi wa kisiasa wanaokutwa na matukio hayo ni lazima wawajibike kwa umma, lakini matukio haya yamekuwa yakitokea bila wao kuwajibika," alisema Nape na kuongeza:

"Inapotokea shughuli za chama chako zinasababisha kupotea kwa maisha ya watu kila unapozifanya na bado usitake kuwajibika, inahitaji roho ngumu na ujasiri wa aina yake."

Alisema CCM inaungana na wanaCCM na wananchi wote kulaani mauaji ya aliyekuwa Mwandishi wa Channel Ten mkoani Iringa, Daudi Mwangosi aliyeuawa Septemba 2, mwaka huu.

"Chama Cha Mapinduzi kimepokea kwa masikitiko makubwa sana taarifa za kifo hicho na kujeruhiwa kwa askari hao.CCM inachukua nafasi hii kutoa pole kwa wafiwa, wanahabari nchini na wote walioguswa na msiba huu kwa namna moja au nyingine," alisema Nape.

Katibu huyo wa Itikadi na Uenezi alisema CCM imetoa mwito kwa vyombo na tume mbalimbali zilizoundwa kuchunguza kwa umakini na weledi mauaji ya Mwangosi ili kubaini chanzo cha mauaji hayo pamoja na chanzo cha vurugu zilizotokea na mazingira ya kifo cha mwandishi huyo wa habari.

"Pamoja na mwito wetu wa kuchunguzwa suala hili kwa umakini na weledi mkubwa, pia tunatoa rai kwamba uchunguzi huu ufanyike kwa kutumia muda mfupi ili ukweli uweze kubainika mapema na hatua zinazostahili ziweze kuchukuliwa haraka iwezekanavyo," alisema Nape na kuongeza:

"Vilevile CCM inasikitishwa sana na mfululizo wa matukio ya watu kupoteza maisha au kujeruhiwa katika mikutano na operesheni mbalimbali zinazoendeshwa na Chadema nchini hasa zile zilizofanyika kwa kukaidi amri halali za vyombovya ulinzi na usalama."

Aliyataja baadhi ya matukio hayo kuwa ni la kuuawa kwa kada wa CCM mkoani Singida, kuuawa kwa Ali Hassan mjini Morogoro, kuuawa kwa Mwangosi, kujeruhiwa kwa askari polisi Iringa na matukio mengine yalitokea wakati viongozi wa Chadema wakiendesha operesheni zao mbalimbali nchini.

Nape alisema matukio hayo si mazuri kutokea kwenye shughuli za chama cha siasa kwa madai ni aibu kwa wanachama wake na wananchi kwa ujumla na hivyo kupoteza sifa ya kuitwa chama chema cha siasa.

(Source: Habari Leo 6th september 2012)
 
Nape is one of the people who can not even differentiate between his left eye and right eye so expect nothing from him he has no brain at all his reasoning is to some extent ruled by his stomach so better not listen to what he will come up with
 
CCM inatakiwa kubeba lawama zote kwa kifo cha kikatili cha Mwanahabari Mwangosi,,,,,NAPE hana akili nzuri maana kwake mabaya ya Serikali yanafanywa na CHADEMA lakini mazuri CCM ndo inafanya......Ajabu kwelikweli
 
Kwa mtu kama Nape usitegemee kuongelea chochote tofauti na haya.
1. kuhusu sms ya Dr. Slaa kwa IGP na kuitaka Polisi ichukue hatua, kama vile na yeye ana mamlaka ya kuiamuru polisi na watendaji wengine wa serikali (rejea ziara zake Rukwa na Iringa mwezi July 2012) alivyokuwa anatoa maelekezo kwa watendaji wa serikali kama vile ana mamlaka juu yao.
2. Kwamba wao kama CCM ambayo ni chama tawala wanaiagiza polisi ifanye uchunguzi na kuwafikisha wote watakaobainika kuhusika katika kifo hicho kwenye vyombo vya dola na kujibu tuhuma, zaidi akielekeza mashambulizi zaidi kwa CHADEMA kama alivyofanya msajili John Tendwa muda mfupi uliopita.

Mutayakumbuka haya maneno yangu hasa wakati Nape anaongea, kwani hana jipya.
 
Anazungumza nape as Nape or kwa niaba ya CCM. Asitake kuifanya tume iliyoundwa haina maana. Yeye akiongea kwa niaba ya chama tawala ambacho kinaunda serikali ni sawa na kauli hiyo kutolewa na JK itabidi tume ivunjwe. Kama anasema yeye mwenyewe as Nnape na si kwa niaba ya chama aongee tu. Ila atakachokisema then tume ikaja na maelezo tofauti atakuwa kajidhalilisha. Vilevile maneno yake yakifanana na ya tume tutajua tume imekaririshwa. Sometimes bora kunyamaza. Nape kama ansoma hapa ajipime.
 
Anazungumza nape as Nape or kwa niaba ya CCM. Asitake kuifanya tume iliyoundwa haina maana. Yeye akiongea kwa niaba ya chama tawala ambacho kinaunda serikali ni sawa na kauli hiyo kutolewa na JK itabidi tume ivunjwe. Kama anasema yeye mwenyewe as Nnape na si kwa niaba ya chama aongee tu. Ila atakachokisema then tume ikaja na maelezo tofauti atakuwa kajidhalilisha. Vilevile maneno yake yakifanana na ya tume tutajua tume imekaririshwa. Sometimes bora kunyamaza. Nape kama ansoma hapa ajipime.

Kumbuka vyama vikubwa vya upinzani vimekwisha laani mauaji haya, CCM bado na huenda ndio zamu yake. Lakini kwa wadadisi hii itakuwa karata nzito kuicheza kulaani au kukana kurudisha imani ya watz kwenye chama
 
nashangaa waandishi wa habari hawakitosi hicho chama wakati wakijua wao ndio wanaelekeza polisi kuua. Nilitegemea gazeti lije na kichhwa CCM Waua Mwandishi kwa kutumia Polisi. Nafikiri ingewaogopesha zaidi ili waache ukatili wao.
 
Hivi Rejao yuko wapi siku hizi?

By the way, Nape atasema anaunga mkono kauli ya Tendwa maana walipanga pamoja jana usiku nini cha kusema kwenye media leo
 
Back
Top Bottom