Nape, CCM: Unyanyasaji huu ndo utawasadia kupendwa?

RUV ACTVIST.

JF-Expert Member
Jan 14, 2012
472
110
Naomba niwashirikishe hii wana JF,

Hospitali ya wilaya Mafinga iliyoko mjini mafinga (IRINGA) amabako jana NAPE alitolea kauli yake ya kukalipia watumishi ndo kiini cha yeye kutoa ile kauli.

Tayari Mganga mkuu wa wilaya na Mganga mkuu wa kitengo cha Meno wamehamishwa kwa visa vya kisiasa, mbaya zaidi Mganga wa meno hakuna mwingine, hivyo wananchi wanakosa huduma kisa mganga wao yupo CHADEMA hivyo hastahili kufanya kazi MUFINDI (mafinga).

SWALI: Mufindi ni mali ya CCM? wanastahili kufanya kazi mufindi ni wanaCCM tu? Watumishi wote wanaonekana kuwa na uhusiano na waliohama wanayanyasika kwa maneno ya vitisho, Hali hii mpaka lini?

Kabla ya mkutano wa hadhara, Nape alikuwa na mkutano na walimu wa ndani (Naufatilia nijue aliwaambia nini) tena muda wa kazi,na walimu hao walidanganywa eti kuna mgeni toka wizarani amekuja kusikiliza kero za walimu, kuingia ukumbini wakakuta wali na soda na mzungumzaji ni NAPE, ni haki hii?
 
Huyu Nape ameanza kuchanganyikiwa. Amesahau kuwa yeye ni kiongozi wa Magamba na si wa Serikali. MAra kwa mara amekuwa akitoa matamko na maagizo as if yeye ni Minister au Mkuu wa Mkoa/wilaya.

Lakini ni kawaida ya mfa maji, sasa watamalizana wenyewe kwa wenyewe
 
Haya ni maswala mazito sana na ni unyanyashaji mkubwa kinyume change sheria/katiba. Nashauri huyo mganga na hao waalimu wachukulie hatua maswala haya. Hata kama hawatapata haki yao, basi yataingizwa kwenye kumbukumbu na yatafanyiwa kazi mara serikari huru &haki ya watanzania itakapopatikana karibuni.
 
Hamasisheni wananchi wafanye maandamano hapo mafinga ili Dr wao arudi huyu nepi kwani siku hizi ukosefu wa akili (UWAKI) ndio unao msumbua.
 
Back
Top Bottom