Nape: CCM kuwarejesha kwenye ukweli vijana waliopotoshwa na wapinzani

issenye

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
3,781
5,205
[h=3][/h]
NA MWANDISHI WETU

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kitahakikisha katika mabadiliko yake ya sasa kinawarejesha katika kuujua ukweli vijana waliopotoshwa na wapinzani hadi kufikia hatua ya kudhani hakuna mazuri yaliyofanywa tangu uhuru.

Mikakati hiyo ilisemwa jana na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye wakati akizungumza na baadhi ya viongozi na watangazaji wa Clouds Media Group, Mikocheni Dar es Salaam, alipofanya ziara ya kujitambulisha katika wadhifa wake huo na kueleza mabadiliko yaliyofanywa na Chama, mapema Aprili mwaka huu.
Alisema, wakati wapo vijana ambao hawakuipigia kura CCM katika uchaguzi mkuu uliopita kwa sababu zinazoonekana kuwa za msingi, lakini ipo idadi kubwa ya vijana ambao walifanya hivyo kutokana na chuki tu kutokana na kushibishwa na uongo na baadhi ya vyama vya upinzani.
Nape alisema katika miaka ya karibuni hasa baada ya kupevuka kwa kiwango kikubwa mawasiliano kwa njia ya mitandao kwenye kompyuta, baadhi ya vyama hivyo vimetumia na vinaendelea kutumia mawasiliano hayo kueneza uongo kwa njia hiyo na kufanikiwa kuwanasa vijana wengi kwa kuwa ndio wanaopendelea zaidi kutumia mawasiliano hayo ya mtandao.
"Baada ya vyama vya upinzani kujua kwamba vijana wengi wanapenda zaidi upashanaji habari kwa njia ya mitandao kwenye kompyuta, kuliko mikutano ya hadhara na njia nyingine za kawaida, baadhi ya vyama hivi vimetumia sana njia hii kuwajaza uongo vijana", alisema Nape.
"Na kwa sababu uongo ukizidi kuenezwa bila kupingwa huweza kuonekana ndiyo ukweli, baadhi ya vijana wameamini uongo huo, na matokeo yake wamejenga chuki kiasi cha kutoyaamini hata mambo ya maana na ya msingi wanayoambiwa na CCM na serikali yake jambo ambalo ni hatari kwa hatma ya taifa", alisema Nape.
Alisema katika mikakati yake ya sasa CCM itahakikisha inawapa ukweli kupitia njia hiyo ya mawasiliano ya mitandao ya kwenye kompyuta kama 'face book' na kueleza matumaini yake kwamba hatua hiyo itazaa mafanikio kwa kuwa yameanza kuonekana katika hatua za awali ambazo CCM imeanza kufanya.
Nape alisema, CCM inafanya hivyo kwa kuwa bado kina uwezo wa kuongoza huku kukiwa hakuna chama cha upinzani ambacho kinaweza kujitapa kuwa kinaweza kuongoza nchi kwa uhakika ikilinganishwa na hali inayojionyesha katika vyama hivyo hadi sasa.
Alisema, mbali ya kuyaendea makundi ya vijana, CCM pia imejipanga kuyafikia kwa ufanisi zaidi makundi yote, kwa kutumia njia mbadala, ikiwemo kufuatilia kwa karibu maoni ya vyombo vya habari hasa vile vinavyoonekana kuwa makini zaidi katika kutoa habari zake.
Nape aliahidi CCM kutoa ushirikiano mkubwa kwa vyombo vya habari katika kuhakikisha vinapata habari za ukweli, sahihi na kwa wakati kuhusu chama na hata za ndani ya serikali.
"Tunaamini sisi CCM tukifungua masikio yetu vilivyo kwa vyombo vya habari tuyaweza kuongoza nchi kwa usahihi zaidi, kwa sababu ninyi vyombo vya habari ndiyo mliopo mitaani wakati mwingi, hivyo mnaweza kuwa mnayajua mengi kuliko sisi, ni vizuri tukawa tunawasikiliza na kufanyia kazi mnayosema", alisema Nape.
Katika ziara hiyo, Nape alizungumzia kwa kina dhana ya mabadiliko ndani ya Chama na utekelezwaji wake unavyoendelea na baadaye waandishi wa Clouds Media Group walipata fursa ya kuzungumza na kumuuliza maswali yaliyoona yanafaa.
Baadaye Nape akiongozwa na Mkurugenzi Mwendeshaji wa kampuni hiyo ambayo ni walimiki wa vituo vya Clouds FM, Choice FM na Clouds TV, Ruge Mutahaba alipata fursa ya kutembelea baadhi ya vituo hivyo kuona kazi zinavyofanyika.

Source: fullshangwe.blogspot.com
 
Du hao jamaa wa clouds kwenye picha mbona mdebwedo hivyo.

Nape nae anahangaika, hebu maliza kuvua magamba halafu uanze na issue nyingine unatuchanganya bana
 
hakuna kijana aliyeshibishwa uongo ila hali halisi ya maisha inatosha kukufanya uichukie ccm(chukulia mfano yanayoendelea bungeni sasa kwa wabunge wa ccm)
 
Nape asidhani vijana ni mazoba!!
watu wameelimika na wanatumia vichwa vyao kufikiri...
 
Nape, umevaa vizuri and god damn you those clothes are designe'rs lebel, wenzio angalau wawe hivyo, hawahitaji V8 yako.
 
Hakuna uongo wowote waliolishwa vijana maana unaoitwa uongo wote umedhihirika ukweli hadi hii leo mnavuana ngozi sorry magamba!
 
siungi hoja mkono, kwanza maisha ni magumu sana nape, huna jipya wewe..maliza kwanza kuvua hayo magamba then uturudishie mabilion yetu ya EPA, richmond, mengine unajua wewe bwana mzee wa ccj...
 
vijana wanahitaji ajira,gharama za maisha kuwa chini,wanapenda elimu iwe bure au ya gharama nafuu,wanapenda kuona watanzania wananufaika na madini,mbuga za wanyama,hawapendi mikataba ya kifisadi,hawapendi kuona viongozi wanaishi maisha ya kifahali kuliko hata viongozi wa nchi zinazotupatia misaada,mfano safari za nje za Rais.Nape akiweza kutatua hayo machache ndani ya serikali na chama chake ndio aanze kutafuta urafiki na vijana vinginevyo anapoteza muda bure hata akifungua blogs zaidi ya mia haitasaidia
 
CCM bana aliye waroga anaishi mtoni mtongani ndiyo maana akili za nape zimekaa kama nepi ya mtoto mdogo .Tanzania ya leo labda hao clouds anadhani wana influence na vijana wa kitanzania wasiopenda rushwa .Pole sana Nape na ukilaza wako
 
Tunataka udhahiri (certainity) wa maisha kwa vijana na sio porojo na chombo cha habari (clouds) ambacho kinahusika kuwagawa vijana pia. Kama kijana naamka asubuhi sina ajira alafu watoto wa vigogo (akiwemo nape) wanapata ajira kwa kupiga simu tu unategemea nn. CCM ur done wapisheni wengine
 
............................Alisema, wakati wapo vijana ambao hawakuipigia kura CCM katika uchaguzi mkuu uliopita kwa sababu zinazoonekana kuwa za msingi, lakini ipo idadi kubwa ya vijana ambao walifanya hivyo kutokana na chuki tu kutokana na kushibishwa na uongo na baadhi ya vyama vya upinzani..........

hhahahahahha hi kaluli sijui niseme inajicontraidct au haieleweki

Nape eneleeni kuvuana magamba usiwafanye vijana wajinga....eti kuhsibishwa uwongo. Kama uwongo CCM ndio imewasibisha uwongo vijana kwa muda mrefu EPA ni mfano mdogo tu..........
 
Madharau mengine toka CCM, kwamba vijana hawana uwezo au utashi wa kufikiri na kuchagua! Kwa kutumia neno 'kuwarejesha' Nape anasema kuwa vijana hawa walikuwa ccm lakini sasa wako upinzani kwa sababu 'walipotoshwa'. Je, nani aliwapotosha wakawa huko CCM in the first place?
 
Kwahiyo Nape anaposema kwamba na wao watatumia mitandao kutuelimisha sisi tusio na akili mpaka tuamini shule zote Tandahimba kila mwanafunzi ana laptop, Obama anaionea gere Tanzania kwa Maendeleo tuliofikia au Tanzania yaisaidia Japan?
Internet yenyewe anayoitegemea Nape ndio hii ya kuwatemea akina Rejao, Ritz, Jeykey,Aporycalpto & co? kwangu hawa ni Top crapiest in JF sasa wana msaada gani kwa ccm macrapiest hawa.
 
Madharau mengine toka CCM, kwamba vijana hawana uwezo au utashi wa kufikiri na kuchagua! Kwa kutumia neno 'kuwarejesha' Nape anasema kuwa vijana hawa walikuwa ccm lakini sasa wako upinzani kwa sababu 'walipotoshwa'. Je, nani aliwapotosha wakawa huko CCM in the first place?
Hapa nadhani Nape anapaswa kuwaomba radhi vijana, kwamba kwa nilivyomuelewa mimi nakubaliana na Dr Didas Masaburi kwamba hawa wanatumiwa makalio kufikiri, wala sio utani Nape anazidi kuzishushia hadhi degree za India. siwezi kupeleka mtoto wangu India kama hizi ndio product zenyewe.
 
Tunamsubiri tu aingie humu ndo atajua kumbe watu wana uchungu na hii nchi.. Anafikiri kila mtu nyanya kama yeye.. Anadhan UDA,EPA,RICHMOND,MELEMETA,TANESCO haya yote yameletwa na wazungu au ccm??
 
Back
Top Bottom