mfianchi
Platinum Member
- Jul 1, 2009
- 11,842
- 8,230
Hebu tupashe hatujaona Raia Mwema na MwanaHalisi ,bwana mkubwa Nape anasemaje?Wana Jf Nimepata Taarifa ambazo ni za Uhakika ni Kwamba Ziara inayofanywa na Muheshimiwa Nape na Mukama kati Vyombo vya Habari hawatatembelea Kampuni ya Mwananchi,Free media na New Habari kwa Sababu zifuatazo.
1)Mwananchi Communication inaonekana Ni kampuni ya Wakenya lakini Vile Vile ni Magazeti ambayo hayaungi Mkono Chama Cha Mapinduzi,Na kubwa Zaidi ni kwamba MCL ambao huchapisha Magazeti ya Mwananchi na Mwana Spoti,The Citizen Muhariri wake Denis Msacky anaaminika Ni Shabiki wa Chadema,kwahiyo Nape katika ushauri alilimuandikia Katibu Mkuu wa CCM kumshauri Kuwatosa katika ziara ambayo leo walikua Nipashe,kwakuwa Nape anadai Nipashe inakisaidia sana Chama Cha Mapinduzi na wanaunga Mkono Agenda ya Kuvua Gamba.
2)Free Media nayo imetoswa kwa Hoja kwamba chombo Hiki ni cha Chadema na Hakimuungi Mkono Nape katika Harakati zake,kutokana na watu wa Karibu wa Chombo Hiki Nape amedai angelikua Muhariri Mkuu ni Bwana Martin Malela ambae ni swahiba Mkubwa wa Bwana Nape CCM wangelienda kupatembelea lakini Uwepo wa Absolom Kibanda,Hansbert Ngurumo na Kwakuwa Gazeti ni Mali ya CDM wao hawataenda kuyatembelea.
3)New Habari amabao ni magazeti ya Mtanzania ,Rai,nao wametoswa katika ushauri uliotolewa na Nape chombo hiki hakitatembelewa na Vigogo hao wa CCM,kwanza kwasababu Magazeti haya yamebadilika sasa na yamekuwa yakiishambulia CCM na hasa Nape,lakini Gazeti la Mtanzania kwa Sasa Ndani ya Makao makuu ya CCM linaonekana sawa na Tanzania Daima,Mwananchi limekuwa likishambulia serekali na kuibeba CDM hasa limeonekana ni Gazeti linalombeba Zitto kabwe na Kauli ya Nape katika kikao cha sekretariti ya CCM wiki iliyopita alidai Uhusiano wa Hussein Bashe na Zitto kabwe umepelekea mabadiliko ya kimtazamo ya chombo hicho tangu Mwishoni mwa mwaka Jana,na hili la Gamba limepelekea Magazeti hayo kutoibeba Tena CCM
Kwahiyo wana Jf baada ya kuzipata Usiku huu nikiwa Hapa Dom nikaona nizilete hapa Jamvini,Ziara ya Mkuu Nape imedhamiria kujenga Mahusiano na IPP,TSN,UHURUna TBC na kuwatosa MCL,Free Media na New Habari,na CCM wametoa Maelekezo wizara zote Matangazo ya Bajeti yaenda TSN,halafu Uhuru,kama kuna chombo Binafsi basi itakuwa Nipashe na Guardian vingine hawatapata. Naomba kuwasilisha.