Nape: Bajeti Mbadala ya Kambi ya Upinzani inadhihirisha uongo wa CHADEMA

Ushauri wangu ni kwamba from now acheni kumjibu Nape just ignore him na okoa muda wako kwa kusoma mada endelevu na zenye mashiko kuliko kumuongelea huyu dogo si mwelewa . Alisoma India sijui alisoma nini huko .Maana yeye hajui kwamba hata faini zile za mahakamani ni vyanzo vya mapato . Faini za barabarani ni vyanzo vya mapato . Yeyey na CCM wanajua kuomba wazungu tu na si zaidi .
 
Jamani wanaJF Nape ametoa hoja haitaji kushambuliwa bila hoja, mwenye majibu sahihi na afanye hivyo kupitia hutuba yake aliyoitoa. Swali la msingi kwa Nape ikiwa CDM ni waongo kwa ahadi chache walizotoa basi aelewe kuwa CCM watakuwa waongo zaidi kupitia AHADI ZA JK na bajeti iliyowakilishwa majuzi juzi.
Huwezi aminini jinsi ambavyo 96tril zitavyopatika kutimiliza uongo wa JK! Hivi hata viwanja vya machinga complex tano vimeshapatikana? hebu cheki hizo ahadi ni ngapi zimekuwa reflected to and to what extend in budget presented by Hon. Mkulo?
 

Attachments

  • AHADI ZA KIKWETE KWA WAPIGA KURA KATIKA KAMPENI ZA URAIS 2010.docx
    20.2 KB · Views: 86
Ha ha haa Nape bado ana hasira na Dr. W Slaa kweli Slaa ameleta Matatizo Makubwa sana CCM

Nape hawezi kushindana na Dr.Slaa kwa viwango vyovyote,yeye ni mpiga porojo wakati Dr Slaa ni mpambanaji wa kweli.
 
Hebu wekeni Ahadi za JK tuone kama zote ziko kwenye Bajeti ya Mwaka huu au kama zote ziko katika Mpango wa Maendeleo wa 2010/2015
 
Bwana mdogo Nape kwa hoja hizi umepotoka kiasi kwani inaonekana uliziandaa kabla na hazireflect uchambuzi wa bajeti mbadala mimi nilitegemea ungekuja na data kwamba mfano Cdm wanasema watakusanya kiasi kadhaa kwenye kodi ya misitu lakini haiwezekani kwa sababu a,b,c au CDM wanasema wakifuta posho itasave this much wewe ukaja na figure tofauti uliyoifanyia kazi.

Otherwise hapa umepiga politiki ambayo backfiring yake ni kwa mwenyekiti wako, je ile miahadi aliyokuwa akiahidi mwaka jana kwenye kampeni iko reflected kwenye budget hii? Meli mpya ziwa Victoria, Reli mpaka Ngara, Umeme wa uhakika 24 hrs etc. Just one thing Nape na haihitaji fedha za kigeni wala ubunifu wa hali ya juu simamieni na serikali yako kupiga marufuku watu kusimama kwenye daladala. Ukiweza hili ndiyo muanze kuzungumzia mambo makubwa makubwa.
 
Hebu wekeni Ahadi za JK tuone kama zote ziko kwenye Bajeti ya Mwaka huu au kama zote ziko katika Mpango wa Maendeleo wa 2010/2015

[h=2]
icon1.png
Orodha ya ahadi za Kikwete kwa wananchi 2010-2015[/h] AHADI - ALIITOA AKIWA WAPI...

  1. Kujenga reli mpya kutoka Dar es Salaam mpaka mikoa ya Kanda ya ziwa - Nzega, Tabora
  2. Mkoa wa Tanga kuwa Jiji la Viwanda - Tanga mjini
  3. Tabora kutumia maji ya Ziwa Victoria - Igunga
  4. Kulipa madeni ya chama cha Ushirika mkoa wa Shinyanga (SHIRECU) - Shinyanga
  5. Kumaliza migogoro ya Ardhi nchini - Dodoma
  6. Wakulima kuacha kutumia jembe la mkono - Dodoma mjini
  7. Kuwapatia trekta wakulima - Kata ya Mrijo, Dodoma
  8. Wananchi kutoondolewa kwenye Ranchi ya Misenyi - Kagera
  9. Kujenga Uwanja wa Ndege Misenyi - Kagera
  10. Kupanua Uwanja wa Ndege Bukoba - Bukoba Mjini
  11. Kujenga uwanja wa ndege mkubwa Kigoma - Kigoma Mjini
  12. Mtukula kupatiwa umeme kutoka Uganda - Kagera
  13. Mikoa ya Kagera, Kigoma, Lindi, Rukwa na Ruvuma kuunganishwa katika gridi ya taifa ya umeme - Kagera
  14. Kuimarisha Takukuru kwa miaka mitatu - Kagera
  15. Hukumu kwa waliopatikana na hati ya kuua albino - Mbeya
  16. Kununua meli kubwa kuliko MV Bukoba - Kagera
  17. Kuanzisha benki ndogondogo kwa ajili ya wajasiriamali
  18. Serikali kuvisaidia vyama vya ushirika - Mwanza
  19. Kuimarisha usalama Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika kwa kupeleka kikosi maalum chenye vifaa kupambana na wahalifu - Mwanza
  20. Wilaya ya Geita kuwa hadhi ya mkoa Januari mwakani - Geita
  21. Kulinda muungano kwa nguvu zote - Pemba
  22. Kuwajengea nyumba waathirika wa mafuriko Kilosa - Morogoro
  23. Kununua meli mpya kubwa Ziwa Nyasa - Mbeya mjini
  24. Kujenga bandari Kasanga – Rukwa
  25. Kumaliza tatizo la walimu miaka mitano ijayo - Songea
  26. Kufufua mgodi wa makaa ya mawe Kiwira - Mbeya
  27. Kuzuia hatari ya kisiwa cha Pangani kuzama - Tanga
  28. Kununua bajaji 400 kwa ajili ya kubeba wajawazito hasa vijijini - Iringa
  29. Kujenga barabara yenye kiwango cha lami kutoka Same mpaka Kisiwani – Kihurio na kuiunganisha na barabara kuu ya Moshi - Dar es salaam - Same mkoani Kilimanjaro
  30. Kumaliza tatizo la maji katika wilaya ya Same - Same Mjini
  31. Kuboresha barabara za Igunga - Tabora
  32. Kusambaza walimu 16,000 katika shule za sekondari zenye upungufu makubwa wa walimu - Kisesa Magu
  33. Kununua vyandarua viwili kwa kila kaya - Mbeya Mjini
  34. Kuzipandisha hadhi hospitali maalumu saba nchini kuwa za rufaa ili kuipunguzia mzigo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN) - Hydom Manyara
  35. Kulinda amani nchini kwa kuzuia chokochoko za kidini, kikabila na kisiasa - Musoma
  36. Kulinda haki za walemavu - Makete
  37. Kujenga baabara ya Njombe - Makete kwa kiwango cha lami,urefu wa kilomita 109 - Iringa mjini
  38. Kujenga barabara Musoma – Mto wa Mbu Arusha - Arusha
  39. Kuanzisha jimbo la Ulyankulu- Shinyanga Mjini
  40. Kujenga barabara ya lami Manyoni-Kigoma – Kaliua,Tabora
  41. Kukarabati barabara ya Arusha Moshi - Arusha Mjini
  42. Kuboresha barabara ya Handeni, Kondoa, mpaka Singida - Dodoma
  43. Kuwafidia wanakijiji ng'ombe waliopotea wakati wa ukame mwaka 2009 - Longido
  44. Vijiji vyote vilivyoko kilomita 15 kutoka kwenye bomba kuu la mradi mkuu wa maji wa Ziwa Victoria - Shinyanga-Kahama kuunganishiwa maji - Shinyanga
  45. Tatizo la umeme kufikia kikomo Novemba mwaka huu mkoani Arusha – Arusha mjini
  46. Kukopesha wavuvi zana za kilimo - Busekera, Wilaya ya Musoma
  47. Kuwapatia maji wakazi wa Wilaya ya Longido - Longido
  48. Kujenga barabara ya lami kupitia pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Seregenti – Ngorongoro
  49. Utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya kilimo kuwasaidia wafugaji kuweza kupata na kutunza mifugo yao vizuri - Mbulu mkoani Manyara
  50. Kusambaza maji nchi nzima - Babati vijijini
  51. Kusambaza umeme, utoaji wa huduma za afya, na uboreshaji wa kilimo cha umwagiliaji na utoaji ruzuku kwa wakulima. mwaka 2010-2015 - Babati vijijini
  52. Kuongeza mara tatu idadi ya wananchi wanaonufaika na ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa mfumo wa vocha - Iringa
  53. Kuhakikisha Isimani inapata maji ya uhakika - Iringa
  54. Kuiwekea lami barabara inayokwenda katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, ambayo ndiyo hifadhi kubwa kuliko zote Tanzania - Iringa
  55. Kulinda usalama wa wananchi kwa ujumla ili kudumisha amani na sifa ya nchi -Ifunda
  56. Kutokomeza malaria 2015 - Bunda, mkoa wa Mara
  57. Kuwapa wanawake nafasi zaidi - Kilolo, Iringa
  58. Ahadi kuisadia Zanzibar kuendeleza miradi mbalimbali ya kijamii - Kibandamaiti Mjini Zanzibar
  59. Kuipandisha hadhi hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar kuwa ya rufaa - Kibandamaiti mjini Zanzibar
  60. Kuisaidia Zanzibar kila panapohitajika msaada - Kibandamaiti
  61. Serikali kujenga upya bandari ya Mbambabay - Ruvuma
  62. Ununuzi wa Meli mpya yenye uwezo wa kubeba tani 400 - Mbambabay Ruvuma
  63. kufufua chama kikuu cha ushirika cha wakulima wa Mbinga (MBICU) – Ruvuma
  64. Ahadi Rais wa Marekani Barack Obama kuimwagia misaada Tanzania – Ruvuma
  65. Ahadi hakutakuwa na umwagaji wa damu baada ya uchaguzi-Dar es Salaam
  66. Mtwara kuwa mji wa Viwanda – Mtwara
  67. Ahadi ujenzi wa kwanda cha dawa ya kuua viluilui vya mbu - Kibaha
  68. Hospitali ya Tumbi kuwa ya mkoa - Kibaha
  69. Halmashauri ya manispaa ya Kibaha kutenga eneo maalumu la viwanda - Kibaha
  70. Barabara za angani (flyovers )
  71. Mchinga complex kila wilaya Dar es salaam
 
Ana neutralize sumu mkuu, hata mimi nilitaka kuamini kuwa MS labda amebadilika lakini kitambo tu kijacho atachafua hali ya hewa kama si hapa basi jukwaa la dini.

yaanio ni kama mtoa mashuzi flani hivi, akiona watu wamenyuti kwa hasira anaamua kuupepea ili upotee, jamaa akitaka kuongeza credibility anafanya hivyo. itabidi mod wabuni mbinu za kupunguza hizo thanx na likes.
 
Bwana mdogo Nape kwa hoja hizi umepotoka kiasi kwani inaonekana uliziandaa kabla na hazireflect uchambuzi wa bajeti mbadala mimi nilitegemea ungekuja na data kwamba mfano Cdm wanasema watakusanya kiasi kadhaa kwenye kodi ya misitu lakini haiwezekani kwa sababu a,b,c au CDM wanasema wakifuta posho itasave this much wewe ukaja na figure tofauti uliyoifanyia kazi.

Otherwise hapa umepiga politiki ambayo backfiring yake ni kwa mwenyekiti wako, je ile miahadi aliyokuwa akiahidi mwaka jana kwenye kampeni iko reflected kwenye budget hii? Meli mpya ziwa Victoria, Reli mpaka Ngara, Umeme wa uhakika 24 hrs etc. Just one thing Nape na haihitaji fedha za kigeni wala ubunifu wa hali ya juu simamieni na serikali yako kupiga marufuku watu kusimama kwenye daladala. Ukiweza hili ndiyo muanze kuzungumzia mambo makubwa makubwa.

Mkuu mimi ndio maana nikasema Jamaa yuko Obsessed na Dr. W Slaa kama angejipa Muda wa Kutosha angekuja na Tamko ambalo lina make sense lakini KAKURUPUKA
 
hivi huyu ndo mshauri wa mwenyekiti wa chama hahaaa JK una kazikwa kweli!!!
 
Ndugu wana jf kuna post imetumwa na achebe ikionyesha namna nape anavyoponda bajeti ya upinzani iliyosomwa bungeni leo na zitto kabwe.

Ninachomkumbusha nape ni kuwa ahadi ya july ikifika mafisadi wote watakuwa wameondoka tunasubiri utekelezaji. Usidhani tutasahau kauli yako uliyoitoa kwa mbwmbwe ukizani tutasahau

na zikibaki siku saba nitakukumbusha tena, ndugu yako riz alisema atawachukulia watu hatua za kisheria mpaka leo yapata mwezi mmoja hola.

Kwa mwenedno wenu huu wa kuzania watu watasahau imekula kwenu kwa hiyo ndugu yangu nape nakukumbusha kauli yako inakaribia muda wa kuitekeleza.
 
Nape ujabainisha kwanza ahadi alizozitoa JK wakati wa kampeni zipi zimo ndani ya bajeti,MELI KILA MAZIWA YA TANZANIA,treni mpya mpaka kagera,BAJAJI KWA WAJAWAZITO,madaraja,Barabara za juu mkoa wa DAR,machinga complex mikoa yote,Daraja la kigamboni,maragaras,Chuo kikuu mkoani mwanza,MKUU ZIPO NYINGI KAMA NDO HIVYO nani muongo JK AU CHADEMA
 
72.Kununua bajaj nchi nzima kwa ajili ya kusaidia akina mama waja wazito
73.Kuifanya Kigoma kuwa kama Dubai
74.Kulipa deni la chama cha ushirika Mwanza TZS 3bn
75.Kutopenda kusafirisafiri maana nawaudhi wananchi
 
Jamani wanaJF Nape ametoa hoja haitaji kushambuliwa bila hoja, mwenye majibu sahihi na afanye hivyo kupitia hutuba yake aliyoitoa. Swali la msingi kwa Nape ikiwa CDM ni waongo kwa ahadi chache walizotoa basi aelewe kuwa CCM watakuwa waongo zaidi kupitia AHADI ZA JK na bajeti iliyowakilishwa majuzi juzi.
Huwezi aminini jinsi ambavyo 96tril zitavyopatika kutimiliza uongo wa JK! Hivi hata viwanja vya machinga complex tano vimeshapatikana? hebu cheki hizo ahadi ni ngapi zimekuwa reflected to and to what extend in budget presented by Hon. Mkulo?

Hata kwenye mpango wa maendeleo wa miaka mitano, ahadi hizi hazijafanyiwa kazi ipasavyo kumbuka shughuli za maendeleo kwa mwaka 2011/12 zinahitaji Shs 8trln wakati bajeti in Shs 4trl, hapa vipi ni uongo au ndo ukweli wenyewe wa chama chetu cha CCM mdororo aka Magamba
 
Kama kawaida ikiwekwa post inayomuhusu nape na ccm humu itajaa matusi na kejeli mpaka sasa mnaanza kuingilia maisha na mke wake utafikiri hata unamfahamu. Nilidhani zichambuliwe hoja zake alizotoa kama ni za pumba tumuumbue badala ya kubaki kumtukana na kumkejeli.... Are real discussing kujenga au hapa hakitakiwi chochote kinachoisema chadema?.... Zitto ilimchukua muda gani kutoa crticism zake juu ya bajeti ya mkulo? Mbona hamkusema kawahi sana? Kutoa zito si hoja katoa nape kaharibu hali ya hewa.. Ama kweli panawenyewe hapa....
 
Mbona wachangia wale wale mnajirudia?
Jibuni kwa hoja na si kejeli.
Msiwe na jazba kama kama Mbowe aliyesema heri kufa umesimama alafu kesho yake akajisalimisha polisi mwenyewe.
Kuna wengine mlikejeli hotuba ya Mkulo kuhusu idadi ya pages, Leo vipi ya Zitto ni 53pages hamsemi.
Jengeni hoja acha matusi.
 
Back
Top Bottom