Nape azungumzia Harambee ya CHADEMA, wamjibu na kusema kakurupuka!

Baada ya kauli ya Nape ya kua CHADEMA wamekua wakipokea fedha chafu na kuzisafisha kwa kupita michango ya wananchi ya kua pesa hizo zitaiweka CHADEMA madarakani na watowaji wa pesa hizo wanawinda rasilimali zetu ,gesi na mafuta ambayo kuna dalili ya kugunduliwa.Kitu amabacho kimeonekana kwa kauli yake,mbali ya kutokua na mantiki ni kichekesho.Kwa sababu ni CCM ambayo iko madarakani imekua ikitumia pesa chafu katika kampeni zake,kuwalazimisha wafanyabiashara na walalahoi kuichangia bila ridhaa yao,kuuza rasilimali zetu dhahabu,almasi na ufisadi mwingine mwingi.
Kwa kauli ya Nape inaonyesha ya kua CCM imeisha kata tamaa ya kurudi madarakani kwa hiyo kwa mawazo yake nikwamba CHADEMA ikichukua madaraka itaendeleza mfumu uliokua ukitumiwa na CCM,kuuza rasilimali zetu ili kupata pesa chafu kiiendesha.Hivyo sivyo,wakati CHADEMA kinakusanya pesa na michango toka kwa wananchi pamoja na ruzuku wanayoipata ,wanaitumia kuwaelimisha walalahoi kuhusu haki zao na uozo wa CCM na utawala kwa ujumla.Wakati CCM ruzuku,pesa chafu,michango ya kuwalazimisha wafanyabiashara na pesa inayoptikana kiufisadi,kwanza wanajinufaisha wao watawala na kiasi kidogo kinachobaki wanakitumia kuwarubuni kwa kuwanunua fulana na,khanga,kofia pilau n.k.
kwa hali ilivyo hivi sasa pesa hazitoshi na wanaionea Wivu CHADEMA kwa walivyojipanga na kuanzisha uzushi usio na kichwa wala miguu.MUNGU IBARIKI TANZANIA.

naam, inauma sana uhai unapoitoka ccm. Afu wale wanaoitwa machizi na waropokaji wanaposhika hatamu! Haleluyah!!
 
hivi ccm walivyochangisha fedha kupitia simu za mkononi kipindi kile ilikuwa inaficha fedha haramu?kama huu ndio mchezo wenu msidhani kila chama ni hivyo.
 
................
Hivi vyote ni vitu visivyo na mashiko kwa sasa. Chamuhimu kwa sasa ni kuongelea mambo ya maendeleo na namna ya kujikomboa kifkra na kiuchumi.[/QUOTE]

ukombozi upi wa KIFIKRA unaozungumzia Rejao? Hivi na wewe unauhitaji ukombozi wa kifikra? mbona juzi tu ulisherehekea MwanzaHALISI kupigwa life ban? wacha kujikorogao kuwa na msimamo wewe.

Haya kujikomboa kiuchumi kutawezekana vipi wakati CCM wameiba na kuweka shekeli za kutosha uswiswi? Si walipuliwe na kama serikali ina utashi iwapeleke mahakaman kitu ambacho si rahisi, kwani naamini na wewe kwa unavyowatetea wezi, lazima una commision yako.
 
Babuuuuu....kumbe bado upo kwenye ulingo wa siasa? Naona story zako ni zile zile za Tangold, Kagoda na Meremeta! Don't you have something new? Badilika bana, tumeshaichoka hiyo mistari yako. Jitahidi uje na swaga nyingine.
Sema umeichoka ww kama ww na mafisadi wenzio mkimsikia dr kaongea kijasho kinawatoka lakini kwa walio wengi bado tunamuhitaji sana.
 
Bw. Nape, kama mzungumzaji mkuu wa chama chetu, umekuwa ukipigia kelele harambee za chadema ukiziusisha na hela haramu. Kama mwana CCM anayeitakia chama chetu mema, tatizo siyo hela za chadema, tatizo ni mafisadi ndani ya ccm na serikali yake. Kuna taarifa za uhakika kwamba viongozi wengi sana ndani ya chama chetu wanaiba sana hela za walipa kodi na kuzipeleka uswisi. tafadhali sana utupatie majina ya hawa vigogo ndani ya ccm....vinginevyo utakuwa unaendeleza ujuha. Zizi lako limejaa na Ng'ombe wa wizi huku unamfukuza mwizi wa kuku na panga

Tafadhali wapigie chadema kelele ukishataoa ufafanuzu kuhusu hela za uswisi
 
Mkuu wewe mbona unaonekana ni mbunge mzuri wa ccm kuliko wenzako woote!
HONGERA SANA TUNATAKA WATU KAMA NINYI NDANI YA CCM ACHANA NA MAVUVUZELA! KAMA NAPE!
 
Bw. Nape, kama mzungumzaji mkuu wa chama chetu, umekuwa ukipigia kelele harambee za chadema ukiziusisha na hela haramu. Kama mwana CCM anayeitakia chama chetu mema, tatizo siyo hela za chadema, tatizo ni mafisadi ndani ya ccm na serikali yake. Kuna taarifa za uhakika kwamba viongozi wengi sana ndani ya chama chetu wanaiba sana hela za walipa kodi na kuzipeleka uswisi. tafadhali sana utupatie majina ya hawa vigogo ndani ya ccm....vinginevyo utakuwa unaendeleza ujuha. Zizi lako limejaa na Ng'ombe wa wizi huku unamfukuza mwizi wa kuku na panga

Tafadhali wapigie chadema kelele ukishataoa ufafanuzu kuhusu hela za uswisi

Ni mtazamo wa kimageuzi ndani ya CCM! One needs to amplify this!
 
Hizo za uswisi tunazitaka bwana nape na zile chenchi zetu za nguzo za umeme feki toka south kumbe ni za mufindi hii sio uzushi ni waziri wako npe alisema bungeni ....cha ajabu kabisa hakna hata mmoja alie chukuliwa hatua madhubuti ktk hili la wai kabisaaaaaa ccm hakuna msafi hata kama ni shehe au askofu ni balaa tpu mmesikia zile shule wanao iba umeme
 
Bw. Nape, kama mzungumzaji mkuu wa chama chetu, umekuwa ukipigia kelele harambee za chadema ukiziusisha na hela haramu. Kama mwana CCM anayeitakia chama chetu mema, tatizo siyo hela za chadema, tatizo ni mafisadi ndani ya ccm na serikali yake. Kuna taarifa za uhakika kwamba viongozi wengi sana ndani ya chama chetu wanaiba sana hela za walipa kodi na kuzipeleka uswisi. tafadhali sana utupatie majina ya hawa vigogo ndani ya ccm....vinginevyo utakuwa unaendeleza ujuha. Zizi lako limejaa na Ng'ombe wa wizi huku unamfukuza mwizi wa kuku na panga

Tafadhali wapigie chadema kelele ukishataoa ufafanuzu kuhusu hela za uswisi

tatizo si nape , tatizo ni chama kwa ujumla.chama ni pamoja na uongozi, wanachama, rasilimali, na mifumo ya kuendesha chama.Mfano chama hichi hicho bado kinadagnya kuwa itikadi yake ni kuwajali wakulima na wafanyakazi, lakini ni kweli ccm bado inamjali mkulima na mfanyakazi?leo kuna tatizo la bei ya pamba kwa kanda ya ziwa.wakulima hawa wameingia gharama nyingi kwa kutegemea bei ingekuwa kama msimu wa mwaka jana.lakini bila kutegemea msimu unaanza mwenyekiti wa bodi ya pamba dr.festus limbu mbunge wa magu(ccm); akatangaza bei ya T.shs 600/= kwa kilo, je ccm kama inawajali na kuwatetea wanyonge imefanya nini kuwasaidia wauze kwa bei waliokuwa wanaitegemea na shs 1000/=?nakumbuka kwenye mdororo wa uchumi duniani serikali iliingiza triaoni 1.7 kusisimua uchumi, japo mpaka leo hatujui pesa hizo zilienda wapi, kwanini isichukue jukumu la kuwasaidia kama enzi hizo z mdororo wa uchumi?pia kama nape hawezi kusema lolote hili la kuteremka bei ni sidicate wa wenye viwanda vya kuchambua pamba na wanunuzi wa pamba, je nape kasema nini badala ya kuwatetea.je kwa hili kweli tunawajali wakulima?nape yupo kama kichwa box wenye chama wametuli wanamuendesha kwa remote , na kumwacha anapayuka
 
KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi Nape Nauye amemshukia Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbrod Slaa, kufuatia kauli aliyoitoa mkoani Morogoro kwamba Chama Cha Mapinduzi kimekuwa kikiingiza silaha nchini.
"Kauli hii inaonyesha ni vipi Dk. Slaa ameanza kuzeeka vibaya, na sasa kazi ya siasa inamshinda hivyo awaachie vijana" alisema Nape na kuongeza kwamba anatambua kuwa uzee siyo laana kama unamwingia mtu vizuri.

Akizungumza na waandishi wa habari, kwenye Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, mtaa wa Lumumba, Dar es Salaam, Nape amesema, mbali na kuzeeka vibaya, hatua ya Dk. Slaa kuizushia CCM kwamba imekuwa ikiingiza siala kinyemela ni dalili kwamba ameona kuwa sasa operesheni ya mikutano ya Chadema hasa ya Morogoro zinazorota.

Kwa mujibu wa Nape, Dk. Slaa amesikika akitangaza mjini Morogoro kwamba, CCM imekuwa ikiingiza siala nchini na kuwapa vijana wazitumie wawapo kwenye makambi ya Umoja wa Vijana wa CCM.

"Kwanza huyu Mzee inaonyesha ni jinsi gani ufuatiliaji wake wa mambo ni vinyu, kutoa madai kwamba tumeagiza siala kinyemela kwa ajili ya makambi ya vijana wetu, wakati inafahamika kwamba wakati huu CCM imo katika uchaguzi mkuu hatuwezi kabisa kuandaa wala kufanya makambi ya vijana", alisema Nape.

"Kutokana na kauli hizi za uzushi, tunazitaka mamlaka zinazosimamia ulinzi na usalama kumtaka Dk. Slaa awapatie ushahidi wa kina kuhusu mtu au tasisi yoyote ambayo inaingiza silaha nchini kinyemela, na kama ushahidi wake utawezesha kupatikana yeyote basi ashughulikiwe kwa mujibu wa sheria", alisema.

"Huyu Mzee imekuwa kawaida yake kuandaa uongo kila anapoona kwamba anakabia kushindwa katika operesheni au mipango yake au ya Chama chake kisiasa. Wakati ule wa Uchaguzi mkuu, alipoona kwamba atashindwa, alizusha kwamba CCM imeingiza kura nchini kutoka nje ya Nchi, lakini ikabainika kuwa ni uzushi", alisema.

Alisema, hatua ya Dk. Slaa kuzusha uongo ni njama ya kuandaa fujo zitakazofanywa watu walioandaliwa na Chadema, kufanya fujo mitaani wakati wa mikutano wa chama hicho mkoani Morogoro. " sasa anatoa uongo huu, ili watu wao waliokusanya watakapofanya fujo azushe kwamba ni vijana waliotumwa na CCM".

nape yule mpuuzi au????kawaida yake kubisha,na mie naamini atakuwa ndiye muhusika mkuu wa mpango mzima,
ndiyo maana mkama anataka kuachia ngazi.
 
Mchezo mchafu wa CCM tumeuzoea. Bora CDM kuliko CCM walioiba na kukwapua fedha za watazania kupitia Kodi na Bili kubwa za Umeme ili kuendesha chama Tunaomba azungumzie suala la kupandisha Malipo ya Unit za Luku na ukusanyaji wa fedha hizo kuendesha CCM. Watanzania sio wajinga ila hawapendi makuu. Tunayaelewa hayo.
 
Back
Top Bottom