Nape awalipua Dr. Slaa na Mbowe, amtetea Pinda

Nape kwa maneno yako aya una maana unapeleka muswada bungeni wa kuifuta ccm. Jk,pinda,ra,chenge,lowasa,mwakyembe,malecela,chiligati,na wote ambao sijaweza kuwaorodhesha ni wafanyabiashara. Kwa ufupi ni sawa na kuifuta ccm. Nape u r sowing the seed for your own destruction. Nalazimika kuamini kuwa maneno myasemayo ccm ni kama ya chizi wala hayasikilizwi. Mfano mzuri ni maneno ya bosi wako aliyesema kiwanja cha simba pale jangwani aliyeanza kujenga na kuzungusha mabati kuwa abomoe,mpaka leo anachekwa na pako vile vile. Sasa nape nawe ongeza vijineno vyako ili wafanya vioja wawe wengi.
 
Aliye na kiwango cha kujua Mh.Mbowe anatakiwa kutumia gari la aina gani ni serikali, Nape anatakiwa kujua hilo na iwapo serikali ya CCM waliamua kumpa Kiongozi wa kambi ya upinzani gari la thamani kuzidi la PM huo ni kuiukaji wa taratibu na inaonyesha CCM walitoa gari hilo kutaka kumnyamazisha lakini kinyume chake Mh.Mbowe ameendelea kusimamia kile anachokiamini

Ushauri kwa Nape
Akilpeleke chama chake na serikali mbele ya vyombo vya sheria kama PCCB ili wachunguzwe
 
Huyu Bw. mdogo mbona hazungumzii kabisa kuwaondoa mafisadi kwenye chama chake kama alivyokuwa akitamba miezi michache iliyopita? Ina maana amenywea kwa mafisadi walio ndani ya Chama cha magamba, sasa anaona apambane na "mafisadi' wa cdm?. Nadhani anatakiwa awaeleze wananchi jitihada zake za kuwang'oa mafisadi ndani ya chama chake zimefanikiwa kiasi gani badala ya kuanza porojo za kuunga unga!
 
Alisema, baraka hizo za Mbowe kwa mwaka zinasababisha Taifa kupata hasara ya Sh. milioni 25 na kwa kuwa watendaji wengine wa Chadema pia wanalipwa posho badala ya mishahara, kwa ujumla wanaliingizia Taifa hasara ya Sh. milioni 487.

Alifafanua kuwa, fedha hizo ambazo ni hasara hiyo inayosababishwa na Chadema kugeuza mshahara kuwa posho ili isilipwe kodi wakati wafanyakazi wengine wote wanatozwa kodi, zingeweza kununua vitabu vya Sayansi 48,000 kwa sekondari nchini na madawati mengi.
...

Hivi huyu Nape kaishia vidudu nini? Ni vitabu vipi 48,000 vya sayansi vinavyoweza kununuliwa kwa sh 487,000,000 (kwa wastan wa kila kitabu sh 10,145.83) na hela ikabaki kwa ajili ya madawati? Vitabu tu vya mitaala vya shule ya msing kimoja kinauzwa sh 10,000 mpaka 15,000 (aende bookshop za Mtaa wa Samora aulizie). Vitabu vya sayansi kwa O-Level kama Lambert, Abort, Nelcon, etc vinauzwa zaidi ya sh 50,000.

Au kwa sababu watoto wake wanasoma international schools/au nje ambako kila mtoto anapata vitabu hapohapo shuleni?
Au kwa sababu anapata mishahara mitatu (DC, Katibu Mwenezi, na kutoka kwa Mafisadi) na hivyo ye akinunua kitabu kwa sh 100,000 anaona kama ametoa sh 10,000 tu?
Au kwa sababu anajua anaongea na watu ambao serikali yake imewanyima elimu na hivyo hawaelewi hata akisema vitabu vya sayansi ni nini na viauzwa bei gani (angejaribu kutumia idadi ya madawati akaona jinsi atakavyopingwa kwa sababu hata mwananchi wa kawaida anaijua hesabu yake)?

Mwacheni aendelee kuudanganya uma, anasahau kwamba sasa watu wameelevuka na watatumia hesabu hiyo hiyo kuthaminisha ni vitabu vingapi vya sayansi vingeweza kununuliwa na fedha ya Epa (zaidi ya sh 130,000,000,000), Kagoda (Zaidi ya sh 40,000,000,000), Dowans (Zaidi ya sh 94,000,000,000), Kiwira (sikumbuki ni bil ngapi), Na hizi za kunyanyua makampuni ya pamba yaliyoathirika na mtikisiko wa uchumi duniani (sh 48,000,000,000) na zingine nyingi wanazoiba kwa kushirikiana na Barick na migodi mingine?

Tutaikomboa nchi yetu kutoka mikononi mwa madhalimu, walanguzi, wala rushwa na wanyanyasaji wa haki za kibinadamu (walioko tayari kuona damu ya binadamu wenzao ikimwagika na wao wanaendelea kuinjoi madaraka, wanatufanya sadaka na kafara za utajiri wao).

Na siku tukijikomboa, wachimbe makaburi yao wenyewe wajizike kabla sisi hatujawafikia.
 
Dogo anavuta ile sigara kubwa(Ndumu) ndio maana anaropoka ropoka tu bila hata data. Endelea hivyo hivyo kwani ndani ya thithiemu wenye busara wapo kimya. We dogo huna tofauti na yule mzee mliyemvua gamba a.k.a Mzee Kinundu a.k.a Mgosi.
 
Huyu bwana asijifanye kumwosha sana Pinda,hiyo sifa ana anayo mpa pinda mbona watanzania wengi wanayo wengine hawatumii hata sh 1000 kwa siku,hawana hata baiskeli.Mbona anachokifanya pinda hatukioni zaidi ya kulia lia kila mara mbele ya hadhira na kunyamaza kimya.HATUONI MAAMUZI BINAFSI ANAYOYAFANYA KAMA WAZIRI MKUU ZAIDI YA YEYE KUPELEKWA PELEKWA KAMA UPEPO.Asitugeuze watanzania kuwa bafu la kuogea na kujisafisha kisiasa.ALAAAH!
 
Hivi amepewa kazi ya kuwa Mkuu wa Propaganda?

Mimi nashindwa kuelewa naomba mnisaidie wakuu au ukiwa katibu wa itikadi na uenezi ndo unatakiwa pia ufanye mambo ya propaganda? Hizi ni dalili za kuishiwa, yaani CCM choka mbaya! Hivi kwa anaweza kulinganisha ufisadi wa CDM na wa CCM. Ni mabilioni mangapi ambayo yamepotelea mikononi mwa CCM?

Na hizo hadithi za alinacha azitolee huko huko kwa watu wasioelewa. Hebu aje MZA au aende ARS akatoe huo utumbo kama hawajamkamua!! Tumbafu zake!!
 
Siku za Nape zinahesabika,niliwahi kusema huyu kijana ni mnafiki.Sasa nasubiri kauli ya mwisho itakayotolewa na chama kuwa"Alimshauri Mwenyekiti wa Chama Vibaya"hapo ndio atakua ameangukia pua!
 
Really?

Najilazimisha kuamini kuwa mdogo wangu huyu ana uchungu kweli na upotevu wa fedha za umma na kuwa kipimo hiki anchokitumia ataanza kukitumia kwenye PPF, ATCL, n.k na atatoa pendekezo kuwa posho na mishara ya Wabunge ipunguzwe kwa asilimia angalau 30 halafu tuone ni kiasi gani cha fedha tutaokoa halafu tukiziokoa tutafanya nazo nini.
HALI ILIVYO NDANI YA CCM KIUCHUMI NI KIOO AU TASHWIRA YA YALIOMO SERIKALINI.
"Nape: Nikwambie ukweli, hali ilivyo ndani ya Chama watendaji wanafanya kazi kwa mazoea. Hali ya uchumi katika Chama ni mbaya. Huwezi kuamini kwamba kwamba katika mazingira ambayo tuna mali zenye thamani takriban Sh bilioni 50, kinachoingia kwa maana ya mapato ni takriban Sh. bilioni moja hivi. Ni lazima sasa tujiimarishe katika sehemu zote; sio tu kimaadili na kisiasa lakini pia kiuchumi."
Nape mnauye katika mahojiano yake na Raiamwema toleo la №183 tarehe 20-26 April/
Kwa Mantiki hiyo Mbali na nchi yetu kua na rasilimali na utajiri wa kutosha bado wananchi wako katika umasikini wa kutupa kutokana na ufisadi wa chama tawala
.MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
Sikuzote no avatarnilijua ni mwelewa kumbe zero,pesa za mbowe ni za jasho lake,cdm inapata ruzuku kila mwezi so nipesa za walipa kodi,acha uchama ufisadi upo ndani ya chaema
 
Kuna mtu alipata sema kuwa kuishabikia ccm ni kupungukiwa akili.,
Ile thread ilileta mjadala sana,
Sasa kwa haya ya wakina Nape (ambao watu waliwaamini)
Nadhani picha ipo clear sana kwamba CCM, imeishiwa kabisa!
Hoja ni kwamba kama vijana kama Nape wapo hivi na ndio wanaitazama Nchi katika namna hii, na vijana ndio mustakabali wa taasisi yeyote!
Mtu atuambie kama kuna ukombozi toka kwa vichwa hivyo vyenye mtazamo wa akina Nape (vijana wa ccm)
 
Huyu dogo ana matatizo gani? Ameambiwa akitaka kukoga nyoyo za watanzania aeleze ni jinsi gani serikali ya CCM inatekeleza ilani ya uchaguzi. Hii ya kuiimba Chadema as if CCM ndio chama cha upinzani haina mshiko hata robo na wala haitasaidia kurudisha mapenzi yaliyopotea kwa CCM. Just wasting his time for nothing!!!!

Tiba

Exactly
 
watu wengine wehu kweli, Hivi unaweza ukasimama mbele za watu na ukasema Mbowe kapata utajiri kwa jasho lake. Fanya utafiti utajua kuwa mbowe ni fisadi hajaanza leo kaanza muda mrefu na kuna muda alikuwa nalink na biashara chafu. Ufisadi wake tayari umeshajidhihirisha kwa kujilipa mapesa ya ruzuku baada ya uchaguzi wa 2005 na sasa anataka alipwe pesa nyingi kwa magari chakavu.
 
Nape anafikiri kuwa WaTZ ni karunguyeye kama wale wazee wa ccm ! Eti pinda anaishi maisha rahisi , yapi ? Mshahara zaidi ya 15 m. ! Mjinga huyu kijana.
Mkuu kumuita mjinga pia unampa cheo huyu jamaa ni zaidi ya mjinga!
 
Hivi huyu Nape kaishia vidudu nini? Ni vitabu vipi 48,000 vya sayansi vinavyoweza kununuliwa kwa sh 487,000,000 (kwa wastan wa kila kitabu sh 10,145.83) na hela ikabaki kwa ajili ya madawati? Vitabu tu vya mitaala vya shule ya msing kimoja kinauzwa sh 10,000 mpaka 15,000 (aende bookshop za Mtaa wa Samora aulizie). Vitabu vya sayansi kwa O-Level kama Lambert, Abort, Nelcon, etc vinauzwa zaidi ya sh 50,000.

Au kwa sababu watoto wake wanasoma international schools/au nje ambako kila mtoto anapata vitabu hapohapo shuleni?
Au kwa sababu anapata mishahara mitatu (DC, Katibu Mwenezi, na kutoka kwa Mafisadi) na hivyo ye akinunua kitabu kwa sh 100,000 anaona kama ametoa sh 10,000 tu?
Au kwa sababu anajua anaongea na watu ambao serikali yake imewanyima elimu na hivyo hawaelewi hata akisema vitabu vya sayansi ni nini na viauzwa bei gani (angejaribu kutumia idadi ya madawati akaona jinsi atakavyopingwa kwa sababu hata mwananchi wa kawaida anaijua hesabu yake)?

Mwacheni aendelee kuudanganya uma, anasahau kwamba sasa watu wameelevuka na watatumia hesabu hiyo hiyo kuthaminisha ni vitabu vingapi vya sayansi vingeweza kununuliwa na fedha ya Epa (zaidi ya sh 130,000,000,000), Kagoda (Zaidi ya sh 40,000,000,000), Dowans (Zaidi ya sh 94,000,000,000), Kiwira (sikumbuki ni bil ngapi), Na hizi za kunyanyua makampuni ya pamba yaliyoathirika na mtikisiko wa uchumi duniani (sh 48,000,000,000) na zingine nyingi wanazoiba kwa kushirikiana na Barick na migodi mingine?

Tutaikomboa nchi yetu kutoka mikononi mwa madhalimu, walanguzi, wala rushwa na wanyanyasaji wa haki za kibinadamu (walioko tayari kuona damu ya binadamu wenzao ikimwagika na wao wanaendelea kuinjoi madaraka, wanatufanya sadaka na kafara za utajiri wao).

Na siku tukijikomboa, wachimbe makaburi yao wenyewe wajizike kabla sisi hatujawafikia.
Mkuu umeongea ukweli mtupu, nakugongea thanx kabisa! Hawa watu cku yao inakaribia!
 
Alifafanua kuwa, fedha hizo ambazo ni hasara hiyo inayosababishwa na Chadema kugeuza mshahara kuwa posho ili isilipwe kodi wakati wafanyakazi wengine wote wanatozwa kodi, zingeweza kununua vitabu vya Sayansi 48,000 kwa sekondari nchini na madawati mengi.

Alisema mambo ya CCM ni ya kimungu
, ndiyo maana Watanzania wameendelea kukiamini na kukipa ridhaa ya kuongoza nchi kwa amani na utulivu.
Source: Habari Leo

Kuna mambo 2 nimegundua ktk kichwa cha Nape Nnauye;ama ANA MTINDIO WA UBONGO au huwa anazungumza AKIWA KATOKA KUVUTA BANGE;nasisitiza tena hayo ndiyo niliyoyagundua kwa kijana huyu!
 
Nape ni bogusi sana ingawa nilikuwa na matumaini naye wakati akigombea madaraka ndani ya CCM. Baada ya kupata madaraka hayo ameonyesha rangi zake halisi kuwa hakuna mwana-CCM mwenye akili. Vile vile kila ninapoona picha zake naona kama vile anazeeka kimaumbile kwa kasi ya haraka sana, inawezekana na akili zake pia zinazeeka haraka sana.

Njia anayotumia ya kujenga chama chake ni kuwa (a) anakubali kuwa chama chake hakifai kama ambavyo CDM wanavyosema, (b) anashambulia CDM kuwa nao hawafai zaidi kuliko CCM. Hiyo siyo njia nzuri ya kujenga chama cha kisisasa, kwani kama atafanikiwa basi wananchi wanaweza wakahamia chama kingine zaidi ya CCM na CDM. Ninamtegemea aje na hoja za kuonyesha kwa nini watu waipende CCM siyo atuambie kwa nini watu wasiipende CDM.

Mzee wangu kichuguu,

Ndio mnashituka?Si niliwapa angalizo mapema?Loh! Taifa letu linakabiliwa na janga kubwa sana,Usishangae kabisa hata tubadilishe katiba still mambo yatakuwa vile vile tu.Tatizo letu ni KUBWA kweli kweli.Tuweke mambo sawa ili tuende sambamba na matunda yatakayoletwa na mabadiliko ya katiba.Katibu mwenezi anaeneza matusi dhidi ya watu,hiyo ndiyo dividend ya kujivua gamba at its best.Eish!
 
Nape kazi kujilamba midomo tu,hana lolote anazungumza kama anatoa mahubiri watu waokoke......Yani ndio kiongozi ambaye angeongoza wanawa ubungo huyu Mungu wangu weeee.Bola hakupewa na tunashukuru NEC kumchagua awe katibu mwenezi kwani tumeshaiona tabia na hulka yake.Ubunge kupitia jimbo la Ubungo sahau kilaza kama wewe.........
 
Huyu NAPE ni limbukeni mkubwa kakosa cha kuongea,ANGUKO LA CCM LIMETIMIA
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom