Nape awajibu CHADEMA, asema siku saba ni nyingi mno!

KOMRAD NAPE LIVE NA WANAHABARI MUDA HUU CCM LUMUMBA K/KOO. AWAJIBU CHADEMA..

."..siku saba walizonipa nyingi sana,ushahidi upo kwa kila nachosema...waende mahakamani leo wasisubiri siku saba....wakati huo huo wamsaidie mzee Slaa kuja na ushahidi mahakamani wakusema CCM IMEINGIZA SILAHA,TUNATAKA AJE AOMBE RADHI kwa njia ile ile na tutadai fidia bilion 3, na tayari wanasheria wameshaanza hatua"
ASANTENI.

My take.siasa ya tanzania imeharibika,kila mtu ni mbabe,wanaoumia ni wananchi.

Nape is unrepentant! meaning the battle is now joined, CDM your reputation is at stake, do all it takes to shame the devil; you have nothing to loose but integrity! which I deem is everything.
 
Tuache mbwembwe na ushabiki usio na maana tusubiri waende mahakamani tujue moja na muongo kati Nape au slaa full stop...
 
Nape kaka yangu. Angalia sana. Unamaadui wengi sana ndani ya chama chako. Hawa kina dr.slaa ndio wangekuwa waokozi wako kama hujui. Wewe ni mpinga ufisadi na kina dr pia ni wapinga ufisadi. Kwanini usistuke kuwa huna support nyingine zaidi yao kuliko kujivunia chama chako chenye dola wakati wengi wao ndio mafisad? Jaribu kuangalia hapo. Najua una mtazamo mzuri lakini kwa style yako utapotea sababu elewa maadui wako ndani ya chama chako hawatakupa support ng'oo. Jaribu kuwa mjanja kama nyoka na mpole kama kobe kaka.
 
Nilishaapa kutochangia chochote kuhusu Nape. Waungwana tunapoteza muda wetu! Na chama chake kisipoangalia atawagharimu sana.
 
Picha ya kihindi ndio imeanza patamu hapo kila mmoja anajifanya mwamba mtakutana mahakamani.
 
Mnampa kichwa sana kumjadili Nape humu, kichwa chake hakina akili yule dogo, yuko kama baba yake. Amesahau kuwa baba yake Mzee Nnauye alizikwa nyumbani kwa mzee Yusuph Makamba kwa sababu hakuwa hata na Nyumba ya maana ya kuzikwa. Nape Acha kuwa kama babako. Ushauri tu wa bure, ongeza busara kidogo we bw mdogo.

Sasa hapa baba yake kaingiaje? Kwanini tunashindwa kujadili hoja tunajadili mtu?
 
Aliyekuwa mgombea wa ubunge CHADEMA jimbo la Igunga, Joseph Kashindye, anena "Awali nilidhani kuwa mahakama ni mali ya CCM
kumbe si kweli"

Huu ni unafiki wa kisiasa. Ni mara ngapi tumesikia kauli za CHADEMA wakiituhumu mahakama kuwa inailinda CCM? Kumbe walikuwa wanatoa kauli za kupotosha umma kwa maslai ya chama chao. Hii inadhihirisha kwamba kauli nyingi zinazotolewa na CHADEMA ni kauli za kulaghai na kupotosha watanzania. Hali hii haikubaliki.
 
Nape umeshakaa kwenye kona mbaya, nadhani waliokutuma kuusema mchemko ule, bado hawajakutuma uombe radhi! Una kila dalili za kuanza kuweweseka, unajua ulikosea, ila huuoni mlango wa kutokea! Ulikuwa wapi kutoa madai ya kumtaka Slaa kukanusha na kudai fidia?
Watoto wa mjini wanasema 'msala huo mwanangu', na imeshakula kwako!
 
uzuri anaueshitakiwa hapa ni Nnape na siyo CCM. Unajua kitakachotokea hapa? Wadhamini wa wanasheria wa CHADEMA watakiwa ni lile kundi lililoko CCM lilalomwona Nnape kama kibaraka wa lile kundi la pili linaloshindania uraisi wa 2015.
Sitabiri lakini kama kesi hii itapelekwa mahakamani usishangae kwisha baada ya wiki moja na jamaa akaishia kwa babu Seya.
 
Nape Moses Nnauye
August 21.Ni wazi kuwa Dr Slaa ameanza kuzeeka vibaya,na kazi ya siasa imeanza kumshinda,namshauri awaachie vijana.
 
Waliozoea kusema uongo sasa ni mwisho.
Wananchi tutajua nani ni nai katika kusema ukweli.

Its Nape Vs Dr Slaa/Mnyika

Pambano la raundi tisa.

Kulia kwangu GREEN Corner ni CCM,Kushoto kwangu BLUE/RED corner ni CDM

Ticker tape:
CCM uzoefu wa miaka 36
CDM uzoefu wa miaka 15

CCM wameshinda kwa KO miaka yaote
CDM wanaishia raundi ya pili katika uhai wao

Lets get ready to RUMBLEEEEEEEEEEEE!!!!!!!!
Vipi leo umekunywa Glass ngapi za gongo?
 
Nape usichanganya mambo mawili hasa unapogusia masuala ya kisheria. Hoja iliyopo mbele yako kwasasa ni wewe kutoa uthibitisho pasi shaka kuwa CHADEMA wanapata mshiko toka nje.

Suala la nyie kuwa mnaandaa janjaweeds kwenye makambi ya wananchi na mmeagiza silaha ni hoja nyingine na huenda mwendesha mashitaka wa serikali akaona haina tija na kuitupilia mbali kama alivyofanya kipindi mahita ni IGP mlivyomtuma na visu vyenye nembo ya CUF au umeshasahau?
 
Hizi ndio siasa za bongo banaaa! Wanatusumbua tu akili hawa kwenye mitandao na vyombo vya habari wakikutana wanapiga laga kwa kwenda mbele sisi tunatoana macho bureeeeeee.

Tuna mambo mengi sana kwenye nchi hii yanayosumbua akili zetu. Hawa wanabalance siasa zao na wanajua wanachokifanya.

Ukitaka kumshitaki mtu kama kakukosea kuna sababu gani za kutangaza si uende mahakamani tuuu!!!!!!!! Huku ni kutafuta umaarufu tu hakuna lolote.
 
Back
Top Bottom