Nape awa swahiba wa 'Lo-Che Unit'...

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Katibu Mwenezi wa CCM, Nape Mnauye ameonekana kuwa na urafiki wa karibu na kundi la Lowassa na Chenge ambalo wanachama wa CCM wamelibatiza jina la 'LO-CHE UNITY' hapa Dodoma.

Nape amekaririwa akisema kuwa hakuna ajenda ya kuwafukuza wanachama wowote wale wa CCM kwani ajenda hiyo haipo mbele ya Mwenyekiti wa Chama Taifa, Rais Jakaya Mrisho Halfan Kikwete.

Nape alikanusha vikali habari zilizoanzishwa jana humu kwenye JamiiForums baada ya mimi kumtupia swali juu ya ukweli wa habari hizo. Katika kuonyesha uswahiba wake na LO-CHE UNIT, Nape amekuwa akiambatana na wafuasi wakubwa wa kundi la Lowassa ambao ni Hussein Bashe na Ole Millya.

Wachambuzi wa mambo wanadai kuwa Nape amelazimishwa kusalimu amri na Wakubwa zake ndani ya Chama. Nape amenywea na kuamua kulinda kitumbua chake.

Nikiripoti kutoka Vikao vya CC na NEC ya CCM Dodoma,mimi ni Vuta-Nkuvute wa JamiiForums.
 
Nape a.k.a kifisadi kidogodogo kinachochipukia. Nilisema mimi kuwa kuna siku nape nae atageuka. Wanachofanya hawa jamaa ni kuwa wakikuona unachonga sana wanakupa good time uzoee then mwenyewe unabadilika. Now you see!!!???
 
Katika mazingira haya ndipo huwa namkumbuka Waitara wakati anajitoa CCM wakati huo akiwa UVCCM mkoani Tanga alivyosema hawezi kurudi Dar kumuandilia chai E mannuel Chimbi (Wakati huo akiwa M.kiti UVCCM). Katika hali ya kawaida sijui Nape anaweza akamwambia nini hata mke wake kwamba mwanaume unaweza kujibaraguza ndani ya maneno yako kirahisirahisi kama shoga/CD anayejiuza, kweli siasa ngumu
 
na wewe huna maana, unataka kutwambia kuwa nape amenunuliwa....???

hayo ni maneno ya wakosaji wa cdm.
 
Nilishawahi kuwaambia Lowassa ni mashine kubwa kuliko inasaga na kukoboa kwa wakati mmoja.
 
Uongo siku zote hushindwa. Nape na CDM yake hiyo waendelee tu na usanii. Siku ikifika hawataona pakukimbilia. Hivi huyu si alikuwa ni kigogo kwenye CCJ. Kulibadilika nini kwenye CDMi hadi akaamua kurudi na kuwa kiongozi huko. Ama kweli wamepata uwanja mpana wa kutuchezea.
 
Lowassa ni msanii wa kusomea.Alimaliza hapa UD Fine and Perfoming Arts.Hawamuwezi hata kidogo.........
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom