KATIBU wa Idara ya Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye anadaiwa kuwatisha wanachama wa chama hicho wanaomuunga mkono Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa.
Chanzo chetu kilicho ndani ya chama hicho, kimesema chini ya mkakati huo, Nape amekuwa akiwatisha wana CCM hao wakiwamo wanaotarajia kuwania nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya chama hicho.
"Kuna mkakati mbaya unasukwa na Nape na amekuwa akitumia nguvu zote kuhakikisha wana CCM wanaomuunga mkono Lowassa hawapiti katika uchaguzi wa ndani wa chama chetu.
"Katika kutekeleza hili, Nape anawatisha watu hao moja kwa moja kwa kukutana nao ama kwa kuwapigia simu na kuwaeleza madhara ya kuendelea kumuunga mkono Lowassa.
"Katika hili, amekuwa akiwaambia kuwa, hawatakiwi kuwa upande wa Lowassa na kibaya zaidi anawaambia kuwa, kama wataendelea kuwa upande wa Lowassa, hawatashinda katika nafasi zozote watakazogombea au atakata majina yao pindi watakapogombea," kilisema chanzo hicho.
Kwa mujibu wa chanzo hicho, Nape anatekeleza mpango huo katika ziara zake anazozifanya katika mikoa mbalimbali nchini, kwa kisingizio cha kukijenga Chama cha Mapinduzi.
Chanzo hicho kimeendelea kusema kuwa, hadi sasa Nape ameshawatisha baadhi ya wana CCM walioko katika Mikoa ya Iringa, Mbeya na Ruvuma.
Chanzo hicho, kimeendelea kusema katika utekelezaji wa mkakati huo, Katibu huyo wa Itikadi na Uenezi, amekuwa akimtumia mmoja wa vijana walioko katika Idara ya Mambo ya Nje, aliyetajwa kwa jina moja la Nyakia. Kijana huyo yuko Ofisi Ndogo ya CCM, Lumumba Dar es Salaam.
"Nape anamtumia Nyakia katika mkakati huu kwa sababu kila anapokwenda, anakuwa naye na huyu kazi yake ni kufuatilia kila mkoa ni nani yuko upande wa Lowassa, kisha anampa taarifa Nape ambaye huwaita na kuwatisha au huzungumza nao kwa njia ya simu, akiwataka wasiwe upande wa Lowassa," kilisema chanzo hicho.
Nyakia alipozungumza na MTANZANIA kwa simu juzi, alihamaki na kutaka aelezwe ni nani aliyetoa taarifa hizo katika vyombo vya habari.
Hata hivyo, mwandishi wetu aliposema hawezi kumtajia aliyetoa taarifa hizo, alisema hana taarifa nazo na kutaka aulizwe Nape kwa kuwa ndiye anayejua jukumu lake ndani ya chama.
Nape alipozungumza na MTANZANIA jana kwa simu alisema jambo hilo halipo kwa sababu katika dunia ya sasa, huwezi kumtisha mtu kwa kuwa hakuna sababu ya kufanya hivyo.
"Kwanza kabisa jana ulizungumza na Nyakia, kisha ukazungumza na Chongolo, sasa nasema hivi, jambo hilo halipo kwa sababu mimi siwezi kuwatisha watu katika dunia ya sasa.
"Nakwambia huo ni upumbavu, najua wanaoandaa mambo haya ni Lowassa na wenzake, tafadhali msijiingize katika mambo haya, kama mtaandika andikeni, lakini mwishowe tutaanza kuwapiga wao kisha tutawapiga nyinyi ambao ni rafiki zetu.
"Mimi kazi yangu mikoani ni kuimarisha chama, yaani tukikaa ndani bila kutoka nje yanakuwa matatizo, tukitoka nje yanakuwa matatizo, nasema hayo mambo hayapo, waambieni welete hata mtu mmoja aliyetishwa na mimi au hata aliyetishwa na ofisa wangu.
"Hili siyo jambo jema mnataka kutugombanisha, sasa kama mtaitumia tumieni lakini ipo siku tutaanza kuwapiga na nyingi," alisema Nape kwa hasira.
CHANZO: Gazeti la Mtanzania