Nape atoa msimamo wa CCM dhidi ya posho za wabunge

Chadema nao watoe tamko la chama sio kila kiongozi wa chadema anaongea msimamo wake. Mara Mnyika mara Zitto mara shibuda tumwamini yupi
 
Nape nakupongeza sana na viongozi wengine mliofikia uamuzi wa kutoa msimamo wa chama CCM unaolenga kukidhi maslahi ya taifa
 
Chadema nao watoe tamko la chama sio kila kiongozi wa chadema anaongea msimamo wake. Mara Mnyika mara Zitto mara shibuda tumwamini yupi
Hapa umeongea cha maana mkuu. CDM kama chama hawana msimamo wa pamoja. Kila mtu ana mtizamo wake. Hongera sana Nape na CCM kwa kulifanyia kazi suala la posho mapema.
 
Tamko hili sio la Nape ni la chama kwa nini tunamshambulia Nape binafsi. Kwenye agenda ya posho tunapaswa kuunga mkono tamko hili kwani tumekuwa sehemu ya watanzania waliopinga ongezeko la posho
 
Chadema nao watoe tamko la chama sio kila kiongozi wa chadema anaongea msimamo wake. Mara Mnyika mara Zitto mara shibuda tumwamini yupi
Hawa ndio watu wanaoongea kama Bata, hujui kama Mnyika ni katibu wa wabunge wa CHADEMA? hakuna sababu hata ya CHADEMA kuliongelea hili wakati wao wenyewe wabunge ambao wako Bungeni tayari katibu ameshatoa tamko rasmi.
Hii ndio shida yenu watu wenye akili za shake well before use, weka mbali na watoto half empty glass brain.
 
Hivi mtu unajisikiaje unapopinga kila kitu hata kizuri kinachofanywa na ccm kwa maslahi ya taifa
 
Na wewe nashindwa kukuelewa, kwani aliyepinga posho ni Nape au CCM? kumbukeni Nape ni ofisa habari wa CHAMA kwahiyo anatoa taarifa kwa umma kwa niaba ya chama na hivi ndivyo ninavyofahamu mimi.
Siamini kwamba kila atakaloongea Dr Slaa basi ni kauli yake au msimamo wake, bali huwa anaongea kauli ya chama ambayo inatokana na vikao au maagizo maalum. Hapa mimi bado hamjaniingiza kwenye mkenge huu.
Huu ni msimamo wa Chama. Nape amekiwakilisha tu chama. But kwa CDM ni tofauti...kila kiongozi wa CDM ana msimamo wake tofauti linapokuja suala la posho.
 
Hapa umeongea cha maana mkuu. CDM kama chama hawana msimamo wa pamoja. Kila mtu ana mtizamo wake. Hongera sana Nape na CCM kwa kulifanyia kazi suala la posho mapema.
[h=6]Maadhimisho ya miaka hamsini ya Uhuru yamegharimu shilingi bilioni 64 hivi. Hii ni jumla ya malipo yote ya posho, mishahara, vitendea kazi n.k. Inajumuisha yale maonesho ya "wizara na idara" mbalimbali pamoja na gharama za tukio lenyewe la Disemba 9. Wapo wanaosema kutokana na ukuu wa tukio lenyewe ni gharama za lazima tena ni ndogo; ilitakiwa iwe si chini ya "bilioni 100". Lakini wengine wanasema kwa kutumia visifa mbalimbali "ni wizi, wehu, uporoaji" n.k.. wewe unaonaje?[/h]
 
Maadhimisho ya miaka hamsini ya Uhuru yamegharimu shilingi bilioni 64 hivi. Hii ni jumla ya malipo yote ya posho, mishahara, vitendea kazi n.k. Inajumuisha yale maonesho ya "wizara na idara" mbalimbali pamoja na gharama za tukio lenyewe la Disemba 9. Wapo wanaosema kutokana na ukuu wa tukio lenyewe ni gharama za lazima tena ni ndogo; ilitakiwa iwe si chini ya "bilioni 100". Lakini wengine wanasema kwa kutumia visifa mbalimbali "ni wizi, wehu, uporoaji" n.k.. wewe unaonaje?
Hapa tunaongelea kuongezeka kwa posho za wabunge. Habari za maadhimisho ya Uhuru zinatoka wapi? think BIG mkuu
 
Hawa ndio watu wanaoongea kama Bata, hujui kama Mnyika ni katibu wa wabunge wa CHADEMA? hakuna sababu hata ya CHADEMA kuliongelea hili wakati wao wenyewe wabunge ambao wako Bungeni tayari katibu ameshatoa tamko rasmi.
Hii ndio shida yenu watu wenye akili za shake well before use, weka mbali na watoto half empty glass brain.

masaburi yako inakuwasha. ni makosa kudhani kila anachoongea Nape au Mnyika ni tamko la chama mengine ni misimamo yako binafsi. Tamko la chama mara nyingi linatoka kama andishi kama alivyofanya Nape sio kama Mnyika kakutana na waandishi wa habari barabarani wanamuuliza msimamo wake kuhusu posho kisha unasema ni tamko la chadema
 
hata kama makinda ni wa ccm hakuna geni Nape au CCM kutofautiana na Spika. Shibuda na Selasini na baadhi ya wabunge wa chadema na wao wametofautiana na Mbowe kwenye suala la posho. hakuna ajabu
 
Ni uzumbukuku kuchanganya kumchukia Nape na uzito wa hoja aliyotoa kuhusu posho za wabunge.
 
Tamko hili sio la Nape ni la chama kwa nini tunamshambulia Nape binafsi. Kwenye agenda ya posho tunapaswa kuunga mkono tamko hili kwani tumekuwa sehemu ya watanzania waliopinga ongezeko la posho

Kimsingi simpingi NAPE na chama chake kwa hili la maneno, ila nampinga NAPE na chama kwa vitendo, ni mambo mengi sana tumeambiwa na ccm lakini imekuwa tofauti, tuko pamoja na ccm kama wakiamua kulisimamia hili la poshio kwa vitendo ili lifanyike ,

Hapa sisemi posho ziondolewe au zisiondolewe, kuna mabo mawili ya kufanya
1. Hizi posho waendelee kupewa hawa jamaa wa posho il akwakuwa wameziongeza kwa 185% basi wafanyakazi nao waongezewe 185% kwani maisha si magumu kwa wabunge tu.

2. Au basi hizi posho ziondolewe ili haya matabaka wanayoyaunda yasiwepo lasivyo kiama kinakuja muda si mfupi.
 
Hapa tunaongelea kuongezeka kwa posho za wabunge. Habari za maadhimisho ya Uhuru zinatoka wapi? think BIG mkuu
Si niliwahi kusikia kamati kuu ya CCM IMEITAKA SERIKALI KUSHUSHA BEI YA SUKARI! JE SERIKALI ILITII MAAGIZO YA KAMATI KUU YA ccm?
Sijawahi kuona serikali hii ikitii maagizo ya CCM.
 
Hivi kwenye hiyo statement kuna MAHALI NIMESEMA NATAKA KUHAMA CHAMA KWASABABU WAMEPANDISHA POSHO???????!!!!! KESHO NA KESHOKUTWA MTASEMA NAPE BINGWA WA KUKANA!!!!!!!!!!!!!!!!
Mjomba, kwa kumbukumbu zangu ulishawahi kudai kwamba wewe si mwanachama wa JF. Leo imekuwaje tena! Kigeugeu! Naona gamba limeng'ang'ania kiunioni. Mzee EL bado anadunda tu. Kelele zooote ulizokuwa unatupigia hapa kumbe ulikuwa unatuchosha masikio yetu tu. Kama umeshindwa la gamba una uhakika gani kwamba JK atakusikiliza kwa hili linalowahusu Wabunge ambao wa CCM ambao wakisema shiiiii, nyie wote lazima muufyate? Kwa busara ni heri unyamaze tu uache mambo yajiendeshe yenyewe kama anavyofanya Mwenyekiti wako.
 
Hizo kauli ni kama zinatolewa na chama cha upinzani. Chama tawala chenye wingi wa wabunge hakitakiwi kutoa kauli za kulalamika kama vile hakina la kufanya. Nape CCM ni chama tawala na ndicho kilichoidhinisha ufujaji wa hela za umma kupitia hizo posho (kumbuka vyama vya upinzani vilipinga na kupendekeza kufutwa hata kwa hiyo 70,000)!

Kipindi hicho mlikuwa kimya na sasa mnataka tuamini mlikuwa hamjui kinachoendelea? Au chama kunasubiri kusikia wananchi wanapokea vipi ufujaji ndipo kinatoa tamko na tamko lenyewe legelege. Wawajibishe wale waliotaka kulibebesha taifa mzigo huu hapo tutaelewa!
 
Ni uzumbukuku kuchanganya kumchukia Nape na uzito wa hoja aliyotoa kuhusu posho za wabunge.

Kacheck malaria, inaweza kuwa imepanda sana, kwa sababu unaweweseka sana! we mwenyewe hushituki?
 
Hivi kwenye hiyo statement kuna MAHALI NIMESEMA NATAKA KUHAMA CHAMA KWASABABU WAMEPANDISHA POSHO???????!!!!! KESHO NA KESHOKUTWA MTASEMA NAPE BINGWA WA KUKANA!!!!!!!!!!!!!!!!

Tatizo si kukana mkuu ila mnachokingea na utendaji wenu ni tofauti kabisa,hapo mmeonesha msimamo lakini mtaweza kweli kuyasimamaia hayo mnayoyasema?
 
Ilianza hivi,

Katibu Wa Bunge (Hakuna Posho),
Spika Wa Bunge (Posho Ipo Maisha Yamepanda)
Tukasikia Mkuu Wa Kaya Kagoma Kusaini Waraka Wa Posho,
Na Sasa Chama Chao Kinalaani Posho.

Yupi wa kumuamini? Kitakachofuata ni nini?
"CCM VIGEUGEU"

Taratibu mpango wa kuwahamisha kwenye mjadala wa katiba unaanza kufanikiwa.Magamba bwana!
 
CCM imeona si vema kukaa kulikalia kimya na hivyo imetoa msimamo wake kama ifuatavyo:
CCM imeona isikae kimya au Nape ameona asikae kimya? CCM imefanya kikao gani kuamua hayo?
 
Back
Top Bottom