Nape athibitisha yeye ni chaguo la vijana

the horse

JF-Expert Member
Sep 27, 2011
652
441
Habari za kuaminika kutoka ukumbi wa mikutano wa mwalimu Nyerere,uliopo chuo cha Mipango, Dodoma. Ndugu Nape Nnauye alipoingia ukumbini vijana wote walilipuka kwa vifijo na shamra shamra za kumpokea kiongozi wao huyo makini.
Lakini nae Nape kwa uhodari mkubwa akaendelea kukonga mioyo a vijana hao kwa kuwaburudisha kwa kupiga gitaa kwa umahiri mkubwa.

Hakika ni Kijana anayeonyesha njia kwa vijana wengine...!
 
Attachments

  • DSC_9872.JPG
    DSC_9872.JPG
    390.9 KB · Views: 410
  • DSC_9873.JPG
    DSC_9873.JPG
    409.6 KB · Views: 371
  • DSC_9913.JPG
    DSC_9913.JPG
    328.7 KB · Views: 261
  • DSC_9924.JPG
    DSC_9924.JPG
    493 KB · Views: 223
kati ya viongozi wa ccm wenye unafuu nape ni mmoja wao. Tatizo wanatamtumia bila yeye kujijua na chama alichopo kimeshachina hivyo na yeye anaweza kuchina muda wowote
 
huo mkutano ulikuwa wa vijana au vijana wa ccm, maana wanaojiita vijana wa ccm wakati mwingine wana miaka hata 40.
 
nape yeye ni katibu wa itikadi na uenezi wa chama...sasa mbona wanampokea kama vile ni mwenyekiti wa uvccm? anaanza kujiona yeye ni kiongozi wa vijana asijisahau yeye ni katibu mwenezi tu cheo kidogo sana kwenye chama lakini kaamua kukikuza na kujiongezea madaraka mwenyewe
 
Angekuwa chagua lao wangemletea zengwe la umri kwenye uchaguzi wa mwenyekiti? UVCCM ya sasa ni ya nani ? Maana kama ni EL Nape hana lake hapo? Labda kwa Bwana SIX! Maana Bwana Ritz1 hakaai meza moja na huyu ndugu pia? Hivi Riz1 bado ndiyo mtunza mali za UVCCM? Kiukweli NAPE alikuwa ni jaribio la kuunganisha makundi ndani ya CCM, lakini yeye akajisahau akadhani wajibu wake mkubwa ni kuliiangamiza kundi la EL ambalo limeibuka na ushindi katika chaguzi za Jumuiya za CCM?
 
kuna habari zinachekesha sana,
Sasa walimshangilia kwa sababu ya burudani ya gitaa aliyotoa ama kwa kufanikisha lile zoezi la kuvua magamba kwa siku 90 aliloahidi?

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
acha ku generalise we Farasi, sema ni chagua la vijana wa ccm tu
vijana wengi walioko mtaani hata hawamfeel huyu mshkaji
 
aiseee babaangu mbona kwenye picha naona wazeeee alafu anapiga gita wakati watanzania wanakufaa na njaaa
 
Mkuu, yaani ameonyesha yeye ni chaguo la vijana kwa kupiga guitar na kushangiliwa?...Mbona kuna vijana wengi wa BSS wanaoweza kufanya hivyo?

Na nadhani "ameonyesha kuwa ni chaguo la vijana" wa CCM.
 
Habari za kuaminika kutoka ukumbi wa mikutano wa mwalimu Nyerere,uliopo chuo cha Mipango, Dodoma. Ndugu Nape Nnauye alipoingia ukumbini vijana wote walilipuka kwa vifijo na shamra shamra za kumpokea kiongozi wao huyo makini......

Chuo kimefunga au bado kinaendelea huo ukumbi upo umbali gani kutoka chuoni hasa kumbi za mihadhara,wanawaghasi tu wanafunzi chuoni au ndo mwendelezo wa siasa vyuoni.
 
Habari za kuaminika kutoka ukumbi wa mikutano wa mwalimu Nyerere,uliopo chuo cha Mipango, Dodoma. Ndugu Nape Nnauye alipoingia ukumbini vijana wote walilipuka kwa vifijo na shamra shamra za kumpokea kiongozi wao huyo makini.
Lakini nae Nape kwa uhodari mkubwa akaendelea kukonga mioyo a vijana hao kwa kuwaburudisha kwa kupiga gitaa kwa umahiri mkubwa.

Hakika ni Kijana anayeonyesha njia kwa vijana wengine...!

====================================================================

So what? Vijana wa CCM wanajidanganya sana. Ishu siyo Nape wala nani, ishu nzito ni CCM. Mapepo mitaani wiki hii yamekuwa hayasumbui, kumbe yapo hukko Dodoma. RIP - CCM
 
Habari za kuaminika kutoka ukumbi wa mikutano wa mwalimu Nyerere,uliopo chuo cha Mipango, Dodoma. Ndugu Nape Nnauye alipoingia ukumbini vijana wote walilipuka kwa vifijo na shamra shamra za kumpokea kiongozi wao huyo makini.
Lakini nae Nape kwa uhodari mkubwa akaendelea kukonga mioyo a vijana hao kwa kuwaburudisha kwa kupiga gitaa kwa umahiri mkubwa.

Hakika ni Kijana anayeonyesha njia kwa vijana wengine...!

nape una ID ngapi umu mdogo wangu??
 
wewe ulitaka apokelewe vip? ndani kwenyewe ni ccm kichwa cha habari kingetakiwa kiwe hivi nape ashangiliwa kwa ndelemo na wa ccm wenzake ndani ya ukumbi wa ccm
 
Back
Top Bottom