Nape atasafisha chama alichokuwa anakichafua?

Hapa uswe, huyu jamaa ameanza vibaya, anaongea maneno mengi bila kufikiria. Huenda hakutegemea kupata cheo hiki. Najua ana msimamo na anajua kujenga hoja, lakini tatizo la kuwa na gamba la kijani ni unafiki. Ndiyo maana mtu anaweza kusema kile ambacho haamini.
 
jamani naombeni muelewe kitu kufa kwa nyani miti uteleza Mungu kashapanga ccm iporomoke na juu ya hilo Mungu atalitekeleza kila atakaye kuwa anaingia ataonekana mbaya na afai kwa sababu nchi inatakiwa kubadilishiwa mfumo mzima na Mungu
 
Ndio maana wanashikwa mikono na kikwete kwenye CC. Kikwete kawapigania yeye na January kwasababu katika ccm hakuna mwenye akili kama hawa. Wacha wafe na hiyo familia yao.
 
CCM ni nyoka waliojivua gamba kwa kuondoa lie la zamani lililochakaa na kubaki na jipya linalongara kama vile wamezaliwa leo. Lakini ukweli kuwa bado ni nyoka yule yule tu. Kama alikuwa kifutu, swila, chatu au nyoka mwengineyo bado hajabadilika akawa mjusi. Kwa hiyo watanzania tusicheze naye hata kidogo, ataendelea kutumaliza kwa sumu yake itakayokugandisha damu na kufanya mioyo yetu ishindwe kufanya kazi
 
Njia na style wanayotumia kukijenga Chama ni Ya Enzi za Ujima!
Mie Simwamini Januari kwani Kama Babake anaitwa 'gamba' nae anajichomeka humo humo basi hana Heshima!Mzee Makamba alijitahidi kwa Kiasi chake na Si halali kumtoa madarakani kwa kumwita Gamba!Kama Januari hakuona babake kadhalilishwa mie naona kabisaa na Hakutendewa haki kwa namna alivoondolewa!Angeondolewa kISAYANSI Na Si Kiujima!Tuasimwani januari hana machungu ya kweli!kama kashindwa kumwonea huruma babake je atamuonea nani!
Pili,Nape na Wenzake naona kama wanapayuka!Kwani Tatizo la CCM kuchuja siamini kama ni Chenge,Makamba na Rostamu!Bali ni Maisha Bora Kukosekana!Wanachi sikuhizi hawana shida na jina la Mtu Kwani siku hizi hapendwi mtu!Bali wanataka dawa ziwepo hospitali,mahitaji muhimu apate kwa bei nzuri nk nk!Ukianza kutaja Taja sijui chenge,Unabugi stepu,Uonesha njia kukabilina na changamoto za Maisha magumu kila kukicha,na huko tuendapo mtazomewa manake mwakolia mambo ambayo hayawagusi wananchi na hayana Tija Msiwe wavivu wa kufikiri mkaishia kuuza sura ilhali mabadiliko hayaji!Mnakazi ngumu na msipojicheki mtakiua chama badala ya kikijenga hasa pale Mtapoanza Kuzomewa!Walioondoka wameondoka na mliobakia Muoneshe mikakati kupunguza makali na machungu ya Maisha na si kupiga bla bla na zeze!
Mgosi Makamba leo twamuona Gamba!Narudia huyu mzee si gamba ni Mstaafu na Tukiendelea kuwashambulia CCM wenzetu ndio tunazalisha makundi mapya!Haki ni laziama Itendeke na Ionekane Kutendeka
 
Kujivua gamba maana yake ni nini kwa watanzania? Let them face justice system for crimes they have committed. We want all cc members to be charged for what they did to Tanzanians haya sio maombi magumu kutekeleza.
 
Mheshimiwa Nape nakuandikia ujumbe huu kwa niaba ya secreatriet nzima mpya ya chama chetu kipya kimechojivua magamba juzi, Mimi ni mwanachama hai mwenye mapenzi dhati ya Chama changu cha mapinduzi lakini yasiokuwa na matumaini tena ni miongoni mwa maelfu ya wana ccm tuliokata tamaa.

Ndugu Nape nilikuwepo dodoma wakati zoezi la kujivua gamba na niliondoka siku 4 baadae nikifuatilia matukio mbalimbali yaliotokana na ujivuaji wa Gamba kwa chama chetu, Ukweli ni kwamba hakuna mabadiliko kwa wakata tamaa wote wa ccm walioyaona na hakuna ameoweza rudisha roho yake au mapenzi yake kwa chama kwa tukio la secreatariet ya makamba kujiuzulu kwa kifupi haina Imapct yeyote hadi leo.

Mh. Nnauye madhara ya au matatizo ya chama chetu hayako ndani ya Magamba yapo ndani ya Damu Mwananchi aliopo Kibondo Tandahimba kaisho hateswi na ROSTAM AZIZI, CHENGE AU MAKAMBA sio Kweli anateswa na mfumo wa chama ambao ni DAMU NA SIO MAGAMBA kama chama hakitaki kujua hilo ni kwamba tusishangae 2015 tukapata 40% ya kura zote kutoka hizi 61%
Usichokijua huko vijijini viongozi wote wa vijiji wa chama chetu walishinda kwa kuiba kura sio kwa kuchaguliwa na wananchi hii ni kuanzia serikali za vijiji madiwani hadi wabunge jambo hili limefanyika kwa kulindwa na dola wananchi huko vijijini wanateswa na hawa madiwani na viongozi wa chama chetu wa serikali za vijiji hawa nao ni Magamba kwani wananchi wameapa hawatafanyiwa ushenzi huu tena .

Mheshimiwa Nnauye kujivua gamba na huku mnalindwa na dola tunaongeza wigo mkubwa wa uadui kwa wananchi hata wale wanachama wetu wanajiuliza kwanini tunalindwa kama kweli tupo sahihi na tunapendwa.

Wakati nipo Dodoma ulitangazwa mkutano wa kutambulisha secretariet ya Chama chetu cha Taifa ilikuwa ni wazo zuri lakini kilichonishangaza azimio hilo lilipitishwa jumatano saa tisa mchana kama kutakuwa na mkutano wa kutambulisha secretariet ya taifa siku ya Alhamis saa saba mchana Nyerere square katika mkoa wa Dodoma na jukumu walipewa CCM mkoa dodoma ilikuwa ni kazi ngumu kwani mkutano ulikuwa unafanyika ndani ya masaa machache na kibali cha mkutano kilikuwa hakijaombwa kwani sheria inataka ndani ya massa 24 sina uhakika kama Kibali kiliombwa na kama kiliombwa hakikukidhi Haja kwani kiliombwa chini ya muda kwa sisi wananchi wanachama wapenzi wa kweli tunasema huu ni uhuni huwezi kujivua gamba ukaendeleza uhuni uleule hii inaleta shaka kwani CCM hivi kwani vitu vya kisanii kila mahali na kila wakati huwezi kusimama kwenye jukwaa unasema umejivua gamba waakti hata vibali vya mkutano umefoji au havipo huu ni uhuni jee tutendeleee kuongozwa na uhuni uhuni tuu wasa CCM wa sasa wana watoto wamesoma shule wanachambua wanaelelewa wanawafumbua macho hata wazee wao mbumbu yaani wanachama mazoea kwa hiyo nyinyi mtakipeleka chama pabaya kuliko hata mzee makamba.

Ni aibu wewe na secreatariet yako yote kusimama na kuwadanganya watanzania eti watu watatu ndiyo wameleta matatizo ya kukiua chama huu ni utoto bwana Nnauye Rostam hawezi kubuni biashara atangaze tender yeye na ajipe tender yeye hao alioshirikiana nao wapo wapi mbona bado wanahodhi madaraka makubwa tu ndani ya chama na serikali hayo ndiyo magamba kuna watu waliopitisha document hizi wakasaini wakakaa vikao wakabariki vikao mbalimbali vya matukio ya ufisadi mbona huwataji hao wapewe siku 90 hao waondoke ndani ya serikali ndiyo kujivua magamba huko chama hakitajengwa kwa nyimbo za komba tulifikiri nyimbo za komba na makundi ya bongo fleva yangetuletea ushindi lakini wananchi wamebadilika ulishuhudia kipigo kitakatifu uchaguzi uliopita hawa ndio watanzania wa sasa Bwana NNAUYE nguvu yenu ni ndogo sana tukiwapima na vijana pinzani wetu toka chadema kama kina Zito kabwe, John Mnyika, Mbowe ,Dr slaa kama wanavyomwita mashabiki wake kama ni Dr Wa Ukweli ( mnyonge mnyongeni acha aitwe hivyo anauwezo wa kujieleza kwa hisia za maslahi ya nchi kuliko ma madr na maprofessor wetu waliojaa bungeni kazi kupiga makofi hata katika mambo yasiyofaa.

Nikirejea safari yangu ya Dodoma nilishuhudia kiongozi mmoja akitoa Oda watafutwe vijana 800 jioni hiyo kwa ajili ya kuhudhulia mkutano huo wakutambulisha secreatatiet pamoja na watoto wa halaiki wa shule lakini ilionekana mda saa ya wa shule ni umeisha kwenda na uwezekano wa watoto wa shule ni mgumu kupatikana lakini watajitahidi ila walipatikana madalali wa 5 kwa ajili ya kumobilize watu hao 800 Nilishtushwa sana na jambo hilo kesho yake nilisikia watu mia 650 wamepewa kadi mpya, mheshimiwa NNAUYE mliopwapatia kadi hawawezi na hawatakuwa wanachama wetu abadan hao ni mamluki wakuletwa kwa ajili ya posho huu ni uhuni chama kinaendeshwa kihuni mnamdanganya mwenyekiti kama mmeingiza wanachama 650 lakini uongo hao wanachama hawapo hatutajenga chama kihuni namna wewe na sekreatarieti yako mnafanya mambo ya kihuni mzee mkama anamdanganya Nani Gamba ni kuwa wa kweli kama misingi ya chama navyotaka propoganda na hadaa itatusaidia tena .

Mzee mkama wananchi wataipa CCM heshima iwapo utawaambia wazi mbunge wetu wa shinyanga mjini hafai anakichafua chama kwa sababu ameiba kura za wananchi Hili ni gamba kwa wananchi wa shinyanga tumepoteza chama shinyanga wana CCM wenyewe tunataka kuona tunashinda kwa haki na mwizi wa kura fisadi hatukai naye , NNAUYE mwambie makongoro Mahanga umeiba kura ukonga step down uchaguzi mpya uitwe CCM tushinde kwa uhalali tuweke watu safi huko ndiko kujivua magamba bila ya hivyo mtapokelewa nchi nzima na wanachama waletwao na magari kutoka sehemu mbalimbali na posho juu lakini mashabiki wetu watakuwa ni walewale mashabiki maslahi kwa sababu hata katika mikutano ya chama ya kata wanachama inabidi wapewe posho ya pesa au chakula au usafiri ndiyo wahudhurie mikutano yetu hili ni tatizo kwa hiyo gamba limevuka lakini saratani yetu bado ipo ndani ya damu.Ni upumbavu kujisifiaeti tumemchukua shitambala wa Chadema toka mbeya impact yake nini kwetu mtu ambae alikiuza chama chama chake kwetu an haaminiki tena kwenye chama chake huyu katika medani za kisiasa hafai hata kualikwa kwenye mkutano wa kijiji wa chama chochote

Mheshimiwa Mkama na secretarieti yeko sisi ndio wanachama wenu ni rahisi sisi kuwa assess kuliko nyie kujipima tunasema UVCCM Inauwa chama inatakiwa kuvunjwa iundwe upya vijana hao kwa maadili ya kitanzania hawafai na wanapoendelea kusimama kwenye majukwaa mnazidi kuwakera watu wamepoteza mvuto kupita kiasi ni watoto wakosa adabu hawawezi kuwatukana mawaziri wakuu wastaafu wa nchii halafu bado wakaendelea kupewa majukwaa hilo ni kosa la kiufundi mnafanya kabisa umma wa wana ccm na hata watanzania wenye itikadi mbalimbali walifadhaishwa na vijana hao kuendelea kwao kuonekana kwenye majukwaa ni kukiua chama mzee mkama unaonekana umezungukwa na vijana wahuni wanapoteza mvuto wa chama badilisha UVCCM hARAKA kuwin vijana damu mpya.

Mheshimiwa Nnauye nimefadhaishwa na hotuba yako ya kutambulisha secretariet yako darajani manzese umenikatisha tamaa kabisa na wewe kuongea propoganda sisi tu wasomi wenzako hatutaki propoganda za kama kuna watu wametumwa Tabora ukiwa na maana ya chama cha upinzani kumchafua Rais wetu na viongozi wa dini watatumika huu ni ujinga upumbavu katika karne hii tunataka kuona tunazungumzia secretariet mpya itafanyaje kazi kuibana serikali iwajibike kwa wananchi sbb nyinyi ndio chama tawala mzee makamba tuliweza kumsamehe kwa umri wake na elimu yake lakini hata wewe msomi unaongea pumba watu wanataka issues na upangue issues na challenge zinazosukumwa na opposition kwa mtaji huu 2015 chama kitakuwa kinatembelea mkongojo na kitakuwa hakijiwezi imekuwa kama tumelogwa kila anayepewa nafasi anakuwa bogus.

Mh.January makamba nimesikitika sana kusema watu wana wadanganya wanavyuo kwenda kuzomea umekosea wanavyuo ni wanataluma kama wewe ingawa wewe umewahi kufika kabla yao na si kwa nguvu yako acha dhihaki ya kipumbavu tunajua ulivyoingia kwa kubebwa hadi kufika hapo tangu kikwete akigombea uraisi na wewe kuingizwa kifix hadi kufikia hapo sio kusema wewe ni intelligent kiasi cha kuwadhihaki watoto wa wakulima kuwa wanatolewa vyuoni kuja kuzomea unatakiwa kuomba radhi jumuiya ya wanafunzi vijana wanauwezo wa utambuzi mkubwa sana sio wana ccm wa zamani hawawezi tena kuunga mkono upumbavu tunatakiwa kuwa smart na chama kuweka thinkers kwa ajili ya strategic watu wapo kwa maslahi ya nchi siyo kwa ajili ya chama kama akili zako zinavyokutuma walichozomea wanachuo ni makosa ya wazi katika mswada wa sheria kwa ajili ya faida yao na vizazi vyao ni tofauti wazomeaji WA CCM tuliowaleta ccm kule karimjee tukidhani wanachuo wanazomea kwa kuwa mswada ni wa ccm mnatupeleka wapi kujivua gamba ni kubadilika kabisa kimaadili hata kimaisha tusijivue gamba kwa kufukuza wanachama 10 hiyo haisaidii wewe ni mbunge lakini umeona upupu unaofanywa na wabunge wa ccm hata kama kitu hakina tija wanapitisha na kuunga mkono kwa kuwa ni cha CCM huko ndiko kuua chama chama hakiuwawi na rostam pekee kwa makosa yake ya kijinai chama kinauawa na makosa ya kimfumo ndiyo maana bunge liliopita liliongozwa na chadema wakati nyie mkiendelea kupinga hoja za maana eti kwa kukua tu ni za opposition na kuunga mkono ujinga wananchi wakatuhukumu Gamba livuliwe bungeni wabunge wafanye kazi ya umma na sio ya ccm .lakini kumbuka kuwaomba msamaha wanavyuo uliosema wanaletwa kuzomea kumbuka watoto hao wengine wamefanya kazi ya kupigania uhuru wa nchi hii kwa uadilifu mkubwa na wamekufa maskini na heshima bila skendo viongozi wa sasa.

Mheshimiwa mkama huwezi jivua Gamba kama Arusha watu wanasema meya hakupatikana kihalali na watu wameuawa kujivua gamba kama mtendaji mkuu wa chama mshauri mwenyekiti wetu na Rais wa JMT Mh. Kikwete uchaguzi urudiwe arusha nina imani CCM itashinda na hata kama ikishindwa itakuwa na heshima zaidi kuliko tulionayo kama tupo pale kwa wizi wakura au kwa mabavu na hujuma na kulindwa na dola huku ndiyo kujivua magamba lakini nimeshangaa mwendawazimu mmoja huyo kaimu wa vijana bwana Shigela anasema uchaguzi ni halali hata wakitoa saa moja uchaguzi haurudiwi huu ni uhuni ccm inakuwa chama cha kihuni nani anampa ruhusa ya kutoa kauli zenye kuhatarisha amani kiasi hiki na viongozi wa chama mnakaa kimya Mkama unakaa kimya, Nnauye january mwenyekti wa chama unakaa kimya kwa kauri ya uhuni namna hii wakati sisi CCM tu watuhumiwa kama tumeiba kura mimi ninakaa Arusha kwa sasa wana ccm leo hii hatuifiki hata 30% ya wananchi wa arusha wenye hasira ya upatikanaji wa meya kinyemela wakiamua wanaenda kumtoa Meya kwa Nguvu CCM hatutaweza kuwazuia hata polisi hawataweza kuwazuia nguvu ya umma kwa hiyo mtutolee hao wahuni haraka kabla hawajakimaliza chama chetu tunahitaji watu kwa ajili ya kufikiri na wananchi wa sasa wanataka watu wanaofikiri kwa ajili yao sio kwa ajili ya ccm kwa sbb nusu ya watanzania hawana vyama na ni wapiga kura.Huyu Shigela hajui tunisia iliondoka madarakani kwa ajii ya kijana mmoja tu wa kimachinga alienyanyaswa na mgambo wa city ,tunataka watu wenye kufikri Meya wa arusha anaweza akasababisha chama tawala kikaanguka na kutolewa madarakani kwa nguvu ya umma kama chama kitaendelea kukumbatia wahuni wa aina hii.
Naomba tujivue gamba la ukweli na sio hadaa hii ya siku 90 za rostam, chenge, na lowasa hii haina impact hata ya 5% kwa mwanacnhi aliyoko kijijini huko songea anaenunua sukari kilo Tsh 2000 na petrol Tsh2300.
NAWAKILISHA



hili lote linasababishwa na katiba ya CCM ambayo inamfanya mwenyekiti kuwa DIKTETA , HUOGOPWA NA AKISHA MTEUA MTU BASI HATA KAMA MTU ALIKUWA NA BUSARA AWE NA DEGREE, AWE PROFESSOR, AWE MA MASTERS, AWE, PHd , UJASIRI WOTE UNAISHA ANABAKI KUCHEZA MZKI WA KUMDURAHISHA MWENYEKITI.


ILI CHAMA KIWEZE KUSILILIZA KILIO CHA WATU NI VIZURI HIZO NAFASI ZA RAIS NA MWENYEKITI IKATENGANISHWA, VINGINEVYO TUENDELEA KUSHUHUDIA UDAHALLILISHAJI WA WASOMI HADI CHAMA KINAFUKA HAKIKA NAUYE BADILI SITAILI AU UNATAKA TUSEME KELELE ZOTE ULIKUWA UNATAKA ULAJI?



MATATIZO YA WATANZANIA KWA SASA NI HAYA
(1) serikali ya ccm imekaa mbali na matatizo ya wananchi, k.m ajira, afya, maji elimu BORA SIYO BORA ELIMU.
(2) WATU WACHACHE NDANI YA SERILAKI YA CCM WANATUMIA SERIKALI KUWAIMBIA WANANCHI WAKE NA HILO WATZ WAMELIJUA KWA HIYO DAWA NI SERIKALI KUACHA WIZI, nec NI THINK TANKERS MNA JUKUMU LA KUIBANA SERIKALI IACHE WIZI AU MUWAFUKUZE WEZI.
(3) uTAWALA WA SHERIA HAUFUATWI KWA USAWA, KUNA WATU WANAOGOPWA!
(4) HAKUNA MAJAJTI AMBAO NI INDEPENDENT, HATUNA WAANDISHI WA HABARI WENGI AMBAO NI INDEPENDET BALI WANAGANGA NJAA KWA KUNULIWA KUPENDEZESHA SERIKALI.
(4) HATUNA BUNGE IMARA, SIITA ALIJITAHIDI LAKINI CCM NEC IKATAKA KUMFUKA, SERILAKI YEYOTE ISIYO KUWA NA BUNGE IMARA INAJMALIZA KABISA, HIVYO NEC MPYA NI JUKUMU LENU SIY LA JK, KUWAAMBIA WABUNGE WENU WA CCM WATETEE HOJA ZA WANANCHI HILO LIKO KWENYE UWEZO WENU, WANACHOKIFANYA WABUNGE WA CCM HAKIKA KITAWAHUKUMU MUDA SI MREFU ,YAANA INAUDHI MPAKA NINATAMANI BOMU LIANGUKE HAPO DODOMA WAISHE WOTE HAWAFAI! Wanatia kinyaa, Nape muwashauri wabunge kuwa wanakiuua chama wabadilke waache mipasho na zomea zomea.

(5)ninakushauri nape chukua hotuba ya obama aliyohutubia ghana isome kwa makini hasa usiku ukiwa mwenyewe hotelini au nyumbani irudie rudie then ndio uanze kazi uliyopewa acha kubwabwaja, SIE NI NA WATU HUMU JAMII HAKIKA WANAIPENDA CCM NDIYO MAANA TUNAWAPENI USHAURI MURUA, LAKINI MKIENDELEA KUKATAAA HAKIKA 2015 WOTE TUTAUNGANA KUIMALIZA CCM NA HAKIKA HISTORIA ITAJIANDIKA KWA SERIKALI YA KULINDA WACHACHE ITAVYOENGULIWA MADARAKANI KWA KURA NYINGI MNO!! TENA TUTAMOBOLOZE VIJANA WOTE NA HAKIKA HAMTABAKI!!
 
:angry:SIKU moja baada ya Chadema kutangaza orodha mpya ya watu, kinachodai kuwa ni mafisadi ndani ya CCM, Katibu wa Uenezi na Itikadi wa chama hicho tawala, Nape Nnauye amesema orodha hiyo ni sawa na mchezo wa kuigiza.:brick:













:angry: NEVER CUT YOURE NOISE TO SPITE YOUR FACE:brick:
 
Nape ndo unataka kutuambia nini?mbona mi sikuelewi....kwani mafisadi mliowapa siku 90 ni wepi?Kwa nini mnacheza na akili zetu kiasi hiki?Ama kweli nyoka ni nyoka hata akivua gamba...!
 
:angry:SIKU moja baada ya Chadema kutangaza orodha mpya ya watu, kinachodai kuwa ni mafisadi ndani ya CCM, Katibu wa Uenezi na Itikadi wa chama hicho tawala, Nape Nnauye amesema orodha hiyo ni sawa na mchezo wa kuigiza.:brick:












:angry: NEVER CUT YOURE NOISE TO SPITE YOUR FACE:brick:
Na hawa ndio wana nia ya kujivua magamba kweli? Au wao ndio wanafanya mchezo wa kuigiza? Ninachoona mambo ni yaleyale ya kuteteana. Ingefaa Nape aulize ushahidi wa ufisadi huo upo wapi, ikijulikana kama hakuna ushahidi wowote, ndio aseme kuwa utangazaji wa mafisadi ni mchezo wa kuigiza.
 
"Hata yaliyosemwa Tabora na Dk. Slaa, ni hila za hao hao wenye shutuma za ufisadi lakini sisi tumejipanga vizuri wasijidanganye kuwa tutarudi nyuma, tutahakikisha chama kinakuwa safi na wenye shutuma wakafanye shughuli nyingine,” alisema Nape.

Ni hatari kwa kiongozi asiyejua kupambanua mambo. Badala ya kumshukuru Dr na CDM kwa kuwataja mafisadi ambao wao wameshindwa kuwataja, ameanza kumlamu......

Hii ina maana waliotajwa na Dr. Slaa tangu miaka ya nyuma na hawa waliotajwa juzi hawako kwenye list ya Nape ya mafisadi?
Atutajie basi list yake tuione! Au kwa vile mkuu wa nchi naye yumo kwenye hiyo list?

Source: Nape: Mafisadi wanamwinda Kikwete, ippmedia
 
Makosa ya ufisadi kwa kiasi ambacho yametajwa na CDM na kuthibitishwa kihalisi, na watuhumiwa kushindwa kujibu ni dhahiri kwamba ni makosa ya jinai ya kiwango cha UHUJUMU UCHUMI kwa sheria za sasa!!!!!!! Sasa akina Nape wanapojaribu kuyageuza kuwa tuhuma za kisiasa sijui watanzania tuwaeleweje?????? Ukweli wa wazi ni kwamba CCM imenasa na hakuna dawa kinyume na madai ya Nape na wenzake!!!!!!!! Wao wenyewe na Mukama wake wameshuhudia jinsi watanzania wanavyochukia CCM!!!!!!!!!! Sijui haya anayoeleza ataanzia wapi kuyatekeleza!!! The fact is "CCM is finished-it is just a matter of time". Ile 61% wanayodai katika uchaguzi watanzania hata mtoto mdogo anajua ni takwimu za UWT na siyo kura za watanzania!!!!!! Aidha wabunge 19 batili ni sehemu ya kazi hiyo ya UWT!!!! Pale Dodoma waliweza kuwaondoa mafisadi papa watatu na kwa kufanya hivyo wakathibitishia watanzania uhalisi wa ufisadi ndani ya CCM; sasa bado 14 ambao wanajulikana kwa majina!!!!!!!!!! Wakumbuke maneno ya hekima ya Mwl Nyerere kwamba dhambi ya ukabila/udini haina tofauti na dhambi ya ufisadi!!!!!!!!!! CCM yote ni UFISADI MTUPU!!!! IN BRIEF: CCM NA SERIKALI YAKE ARE ALREADY DEAD ONLY WAITING FOR MAZISHI-NO WAY FOR REVERSING ANYTHING NOW!!!!!!!!!!!!!!!!! PEOPLES POWER IS GOING TO ASSUME POWER NOT LONG FROM NOW!!!!!!!!!! Gbagbo alijaribu yuko wapi!!!!!!!!!!!! Sasa ni zamu ya CCM na serikali yake!!!!!!!!!!
 
Hofu yangu ni kuwa, nyoka akivua magamba anakuwa kama kijana.
Dawa ya kumuua nyoka si kumkwangua magamba, bali kukiponda kichwa. Mafisadi ambao CDM inawataja ni magamba tu. CCM itakufa kama kichwa chake kitapondwa. Sio kwa kuikwangua magamba
 
D Slaa amekwisha taja wewe hujataja sasa hapo nani anaigiza,Nape ngoma huiwezi wewe
 
Makosa ya ufisadi kwa kiasi ambacho yametajwa na CDM na kuthibitishwa kihalisi, na watuhumiwa kushindwa kujibu ni dhahiri kwamba ni makosa ya jinai ya kiwango cha UHUJUMU UCHUMI kwa sheria za sasa!!!!!!! Sasa akina Nape wanapojaribu kuyageuza kuwa tuhuma za kisiasa sijui watanzania tuwaeleweje?????? Ukweli wa wazi ni kwamba CCM imenasa na hakuna dawa kinyume na madai ya Nape na wenzake!!!!!!!! Wao wenyewe na Mukama wake wameshuhudia jinsi watanzania wanavyochukia CCM!!!!!!!!!! Sijui haya anayoeleza ataanzia wapi kuyatekeleza!!! The fact is "CCM is finished-it is just a matter of time". Ile 61% wanayodai katika uchaguzi watanzania hata mtoto mdogo anajua ni takwimu za UWT na siyo kura za watanzania!!!!!! Aidha wabunge 19 batili ni sehemu ya kazi hiyo ya UWT!!!! Pale Dodoma waliweza kuwaondoa mafisadi papa watatu na kwa kufanya hivyo wakathibitishia watanzania uhalisi wa ufisadi ndani ya CCM; sasa bado 14 ambao wanajulikana kwa majina!!!!!!!!!! Wakumbuke maneno ya hekima ya Mwl Nyerere kwamba dhambi ya ukabila/udini haina tofauti na dhambi ya ufisadi!!!!!!!!!! CCM yote ni UFISADI MTUPU!!!! IN BRIEF: CCM NA SERIKALI YAKE ARE ALREADY DEAD ONLY WAITING FOR MAZISHI-NO WAY FOR REVERSING ANYTHING NOW!!!!!!!!!!!!!!!!! PEOPLES POWER IS GOING TO ASSUME POWER NOT LONG FROM NOW!!!!!!!!!! Gbagbo alijaribu yuko wapi!!!!!!!!!!!! Sasa ni zamu ya CCM na serikali yake!!!!!!!!!!
Nani kakuambia Dodoma alitposwa mtu au watu pale? Ingia Tovuti ya CCM upate ukwei utazame orodha ya wajumbe waoya wa Kamati Kuu mpya ya CCM.

http://www.cms.ccmtz.org/index.php?page=535

WAJUMBE WA KAMATI KUU MPYA YA CCM KWA MUJIBU WA TOVUTI YA CCM.


1. Ndugu Kakaya Mrisho Kikwete - Mwenyekiti
2. Ndugu Pius Msekwa - Makamu Mwenyekiti (Bara)

3. Ndugu Amani Abeid Amani Karume - Makamu Mwenyekiti(Zanzibar)

4. Ndugu Wilson Mukama - Katibu Mkuu
5. Capt. (mst) John Zefania Chiligati - Naibu Katibu Mkuu (Bara)
6. Ndugu Vuai Ali Vuai - Naibu Katibu Mkuu (Zanzibar)
7. Dr. Ali Mohamed Shein - Mjumbe
8. Ndugu Edward Ngoyai Lowassa - Mjumbe
9. Ndugu Shamsi Vuai Nahodha - Mjumbe
10. Alhaj Ali Hassan Mwinyi - Mjumbe
11. Ndugu Benjamin William Mkapa - Mjumbe
12. Dr. Salmin Amour - Mjumbe
13. Ndugu John Samwel Malecela - Mjumbe
14. Ndugu Nape Nnauye - Mjumbe
15. Ndugu Mwigulu Mchemba - Mjumbe
16. Ndugu January Makamba - Mjumbe
17. Ndugu Asha Abdallah Juma - Mjumbe
18. Ndugu Abdulrahman Kinana - Mjumbe
19. Ndugu Anna Makinda - Mjumbe
20. Ndugu Pandu Ameir Kificho - Mjumbe
21. Ndugu Anna Abdallah - Mjumbe
22. Ndugu Rostum Aziz - Mjumbe
23.Dr. Mohamed Gharib Bilal - Mjumbe
24. Ndugu Pindi Hazara Chana - Mjumbe
25. Ndugu Andrew Chenge - Mjumbe
26. Dr. Maua Abeid Daftari - Mjumbe
27. Ndugu Samia Suluhu Hassan - Mjumbe
28. Ndugu Mohamed Seif Khatib - Mjumbe
29. Ndugu Haji Omar Kheri - Mjumbe
30 . Dr. Abdallah Omari Kigoda - Mjumbe
31 . Ndugu Abdurahman Kinana - Mjumbe
32 . Ndugu Anne Semamba Makinda - Mjumbe
33. Ndugu Fatuma Said Ali Mchumo - Mjumbe
34 . Ndugu Zakia Hamdan Meghji - Mjumbe
35. Ndugu Omar Yussuf Mzee - Mjumbe
36. Ndugu Emmanuel John Nchimbi - Mjumbe
37 . Ndugu Ali Ameir Mohamed - Mjumbe
38. Ndugu Yussuf Moh'd Yussuf - Mjumbe
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom