Nape atasafisha chama alichokuwa anakichafua?

.........Nadhani hawa jamaa ni waropokaji kuliko Makamba...naomba waendelee hivyo hivyo ili sisi tuimarike...........
 
Hongera Mkuu Kama kweli watasoma na kuelewa mtakiponya chama lakini hivi hata wajivue Mara Mia ni kazi bure, kwa sisi wa Arusha sijui watajivuaje hasa hii ya umeya kamwe CCM Arusha imekufa hata wafanyeje hadi watakapo rekebisha swala la umeya, Yule kada wa vijana angejua asiongea maana anawazidishia wana Arusha uchungu, wasipoangalia kunaweza kutokea maafa mengine tena.
 
teh teh mmeshakibatiza upya chama cha magamba (ccm), kwa kweli msiwalaumu hao walioteuliwa kukiongoza kwani hata ww ukipewa fursa unakuwa na wakati mgumu kuongea na wananchi unawaambia nini wakuamini 50 haujadeliver chochote leo utawaeleza nini zaidi ya sound
. Viongozi hawapendi kuelezwa kweli wanataka kusikia wananchi wamefurahi wanakupenda wale wanaozomea walevi au wamenunuliwa mabadiliko kwa ccm bado sana
 
Mimi nashangazwa na tuhuma za 'kuzomea' alizotoa January Makamba. Tuchukulie mahala serious kama vile Bungeni -- hivi mabingwa wa kuzomea mle ndani ni akina nani? Tuseme kile cha ukweli.
 
Halafu wanazungumzia eti mafisadi watoke chamani!! hao ni akina nani? Kama january Marope na mwenzake Nape (ambaye kweli nilikuwa nina mategemeo makubwa kutoka kwake) ni majasiri - basi na wawataje hao wanaotakiwa kutoka -- siyo lelemama tu!

Kweli mnaimba na kucheza ngoma ile ile -- pamoja na ujana wenu -- hamna loloote!!!
 
Halafu wanazungumzia eti mafisadi watoke chamani!! hao ni akina nani? Kama january Marope na mwenzake Nape (ambaye kweli nilikuwa nina mategemeo makubwa kutoka kwake) ni majasiri - basi na wawataje hao wanaotakiwa kutoka -- siyo lelemama tu!

Kweli mnaimba na kucheza ngoma ile ile -- pamoja na ujana wenu -- hamna loloote!!!

Umesema yote, kama wahenga walivyosema sikio la kufa halisikii dawa"

"CCM NI SIKIO LA KUFA SIDHANI KAMA WANAWEZA KUSIKIA YOTE HAYA"
 
Halafu Makamba Jr anapaswa kujua kuwa zomeazomea sio ya wa2 flani tu. Kuzomea ni kuonyesha kutoridhika. Sio tatizo msomi kumzomea mpumbavu. Ili mradi asimzomee mjinga
 
Well said mkuu, mwanakijiji wa Tandahimba na Kibondo hateswi na Ra, El wala Ym bali anateswa na "kibali cha kufoji" kufanya mkutano Dodoma. Yeees!!
Kidumu chama cha mapinduzi...
 
mbona Jk hajajivua gamba wakati yeye ndio dereva wa hilo basi la mafisadi hiyo janja ya nyani tumewashtukia nape naye atafute kukundi cha taarabu hizo taarabu zake hatuzitaki.kama kweli unauchungu na mafisadi mwambie boss wako Jk naye avue gamba tujue kwel4 umeamua kupambana na ufisadi
 
mheshimiwa nape nakuandikia ujumbe huu kwa niaba ya secreatriet nzima mpya ya chama chetu kipya kimechojivua magamba juzi, mimi ni mwanachama hai mwenye mapenzi dhati ya chama changu cha mapinduzi lakini yasiokuwa na matumaini tena ni miongoni mwa maelfu ya wana ccm tuliokata tamaa.

Ndugu nape nilikuwepo dodoma wakati zoezi la kujivua gamba na niliondoka siku 4 baadae nikifuatilia matukio mbalimbali yaliotokana na ujivuaji wa gamba kwa chama chetu, ukweli ni kwamba hakuna mabadiliko kwa wakata tamaa wote wa ccm walioyaona na hakuna ameoweza rudisha roho yake au mapenzi yake kwa chama kwa tukio la secreatariet ya makamba kujiuzulu kwa kifupi haina imapct yeyote hadi leo.

Mh. Nnauye madhara ya au matatizo ya chama chetu hayako ndani ya magamba yapo ndani ya damu mwananchi aliopo kibondo tandahimba kaisho hateswi na rostam azizi, chenge au makamba sio kweli anateswa na mfumo wa chama ambao ni damu na sio magamba kama chama hakitaki kujua hilo ni kwamba tusishangae 2015 tukapata 40% ya kura zote kutoka hizi 61%
usichokijua huko vijijini viongozi wote wa vijiji wa chama chetu walishinda kwa kuiba kura sio kwa kuchaguliwa na wananchi hii ni kuanzia serikali za vijiji madiwani hadi wabunge jambo hili limefanyika kwa kulindwa na dola wananchi huko vijijini wanateswa na hawa madiwani na viongozi wa chama chetu wa serikali za vijiji hawa nao ni magamba kwani wananchi wameapa hawatafanyiwa ushenzi huu tena .

Mheshimiwa nnauye kujivua gamba na huku mnalindwa na dola tunaongeza wigo mkubwa wa uadui kwa wananchi hata wale wanachama wetu wanajiuliza kwanini tunalindwa kama kweli tupo sahihi na tunapendwa.

Wakati nipo dodoma ulitangazwa mkutano wa kutambulisha secretariet ya chama chetu cha taifa ilikuwa ni wazo zuri lakini kilichonishangaza azimio hilo lilipitishwa jumatano saa tisa mchana kama kutakuwa na mkutano wa kutambulisha secretariet ya taifa siku ya alhamis saa saba mchana nyerere square katika mkoa wa dodoma na jukumu walipewa ccm mkoa dodoma ilikuwa ni kazi ngumu kwani mkutano ulikuwa unafanyika ndani ya masaa machache na kibali cha mkutano kilikuwa hakijaombwa kwani sheria inataka ndani ya massa 24 sina uhakika kama kibali kiliombwa na kama kiliombwa hakikukidhi haja kwani kiliombwa chini ya muda kwa sisi wananchi wanachama wapenzi wa kweli tunasema huu ni uhuni huwezi kujivua gamba ukaendeleza uhuni uleule hii inaleta shaka kwani ccm hivi kwani vitu vya kisanii kila mahali na kila wakati huwezi kusimama kwenye jukwaa unasema umejivua gamba waakti hata vibali vya mkutano umefoji au havipo huu ni uhuni jee tutendeleee kuongozwa na uhuni uhuni tuu wasa ccm wa sasa wana watoto wamesoma shule wanachambua wanaelelewa wanawafumbua macho hata wazee wao mbumbu yaani wanachama mazoea kwa hiyo nyinyi mtakipeleka chama pabaya kuliko hata mzee makamba.

Ni aibu wewe na secreatariet yako yote kusimama na kuwadanganya watanzania eti watu watatu ndiyo wameleta matatizo ya kukiua chama huu ni utoto bwana nnauye rostam hawezi kubuni biashara atangaze tender yeye na ajipe tender yeye hao alioshirikiana nao wapo wapi mbona bado wanahodhi madaraka makubwa tu ndani ya chama na serikali hayo ndiyo magamba kuna watu waliopitisha document hizi wakasaini wakakaa vikao wakabariki vikao mbalimbali vya matukio ya ufisadi mbona huwataji hao wapewe siku 90 hao waondoke ndani ya serikali ndiyo kujivua magamba huko chama hakitajengwa kwa nyimbo za komba tulifikiri nyimbo za komba na makundi ya bongo fleva yangetuletea ushindi lakini wananchi wamebadilika ulishuhudia kipigo kitakatifu uchaguzi uliopita hawa ndio watanzania wa sasa bwana nnauye nguvu yenu ni ndogo sana tukiwapima na vijana pinzani wetu toka chadema kama kina zito kabwe, john mnyika, mbowe ,dr slaa kama wanavyomwita mashabiki wake kama ni dr wa ukweli ( mnyonge mnyongeni acha aitwe hivyo anauwezo wa kujieleza kwa hisia za maslahi ya nchi kuliko ma madr na maprofessor wetu waliojaa bungeni kazi kupiga makofi hata katika mambo yasiyofaa.

Nikirejea safari yangu ya dodoma nilishuhudia kiongozi mmoja akitoa oda watafutwe vijana 800 jioni hiyo kwa ajili ya kuhudhulia mkutano huo wakutambulisha secreatatiet pamoja na watoto wa halaiki wa shule lakini ilionekana mda saa ya wa shule ni umeisha kwenda na uwezekano wa watoto wa shule ni mgumu kupatikana lakini watajitahidi ila walipatikana madalali wa 5 kwa ajili ya kumobilize watu hao 800 nilishtushwa sana na jambo hilo kesho yake nilisikia watu mia 650 wamepewa kadi mpya, mheshimiwa nnauye mliopwapatia kadi hawawezi na hawatakuwa wanachama wetu abadan hao ni mamluki wakuletwa kwa ajili ya posho huu ni uhuni chama kinaendeshwa kihuni mnamdanganya mwenyekiti kama mmeingiza wanachama 650 lakini uongo hao wanachama hawapo hatutajenga chama kihuni namna wewe na sekreatarieti yako mnafanya mambo ya kihuni mzee mkama anamdanganya nani gamba ni kuwa wa kweli kama misingi ya chama navyotaka propoganda na hadaa itatusaidia tena .

Mzee mkama wananchi wataipa ccm heshima iwapo utawaambia wazi mbunge wetu wa shinyanga mjini hafai anakichafua chama kwa sababu ameiba kura za wananchi hili ni gamba kwa wananchi wa shinyanga tumepoteza chama shinyanga wana ccm wenyewe tunataka kuona tunashinda kwa haki na mwizi wa kura fisadi hatukai naye , nnauye mwambie makongoro mahanga umeiba kura ukonga step down uchaguzi mpya uitwe ccm tushinde kwa uhalali tuweke watu safi huko ndiko kujivua magamba bila ya hivyo mtapokelewa nchi nzima na wanachama waletwao na magari kutoka sehemu mbalimbali na posho juu lakini mashabiki wetu watakuwa ni walewale mashabiki maslahi kwa sababu hata katika mikutano ya chama ya kata wanachama inabidi wapewe posho ya pesa au chakula au usafiri ndiyo wahudhurie mikutano yetu hili ni tatizo kwa hiyo gamba limevuka lakini saratani yetu bado ipo ndani ya damu.ni upumbavu kujisifiaeti tumemchukua shitambala wa chadema toka mbeya impact yake nini kwetu mtu ambae alikiuza chama chama chake kwetu an haaminiki tena kwenye chama chake huyu katika medani za kisiasa hafai hata kualikwa kwenye mkutano wa kijiji wa chama chochote

mheshimiwa mkama na secretarieti yeko sisi ndio wanachama wenu ni rahisi sisi kuwa assess kuliko nyie kujipima tunasema uvccm inauwa chama inatakiwa kuvunjwa iundwe upya vijana hao kwa maadili ya kitanzania hawafai na wanapoendelea kusimama kwenye majukwaa mnazidi kuwakera watu wamepoteza mvuto kupita kiasi ni watoto wakosa adabu hawawezi kuwatukana mawaziri wakuu wastaafu wa nchii halafu bado wakaendelea kupewa majukwaa hilo ni kosa la kiufundi mnafanya kabisa umma wa wana ccm na hata watanzania wenye itikadi mbalimbali walifadhaishwa na vijana hao kuendelea kwao kuonekana kwenye majukwaa ni kukiua chama mzee mkama unaonekana umezungukwa na vijana wahuni wanapoteza mvuto wa chama badilisha uvccm haraka kuwin vijana damu mpya.

Mheshimiwa nnauye nimefadhaishwa na hotuba yako ya kutambulisha secretariet yako darajani manzese umenikatisha tamaa kabisa na wewe kuongea propoganda sisi tu wasomi wenzako hatutaki propoganda za kama kuna watu wametumwa tabora ukiwa na maana ya chama cha upinzani kumchafua rais wetu na viongozi wa dini watatumika huu ni ujinga upumbavu katika karne hii tunataka kuona tunazungumzia secretariet mpya itafanyaje kazi kuibana serikali iwajibike kwa wananchi sbb nyinyi ndio chama tawala mzee makamba tuliweza kumsamehe kwa umri wake na elimu yake lakini hata wewe msomi unaongea pumba watu wanataka issues na upangue issues na challenge zinazosukumwa na opposition kwa mtaji huu 2015 chama kitakuwa kinatembelea mkongojo na kitakuwa hakijiwezi imekuwa kama tumelogwa kila anayepewa nafasi anakuwa bogus.

Mh.january makamba nimesikitika sana kusema watu wana wadanganya wanavyuo kwenda kuzomea umekosea wanavyuo ni wanataluma kama wewe ingawa wewe umewahi kufika kabla yao na si kwa nguvu yako acha dhihaki ya kipumbavu tunajua ulivyoingia kwa kubebwa hadi kufika hapo tangu kikwete akigombea uraisi na wewe kuingizwa kifix hadi kufikia hapo sio kusema wewe ni intelligent kiasi cha kuwadhihaki watoto wa wakulima kuwa wanatolewa vyuoni kuja kuzomea unatakiwa kuomba radhi jumuiya ya wanafunzi vijana wanauwezo wa utambuzi mkubwa sana sio wana ccm wa zamani hawawezi tena kuunga mkono upumbavu tunatakiwa kuwa smart na chama kuweka thinkers kwa ajili ya strategic watu wapo kwa maslahi ya nchi siyo kwa ajili ya chama kama akili zako zinavyokutuma walichozomea wanachuo ni makosa ya wazi katika mswada wa sheria kwa ajili ya faida yao na vizazi vyao ni tofauti wazomeaji wa ccm tuliowaleta ccm kule karimjee tukidhani wanachuo wanazomea kwa kuwa mswada ni wa ccm mnatupeleka wapi kujivua gamba ni kubadilika kabisa kimaadili hata kimaisha tusijivue gamba kwa kufukuza wanachama 10 hiyo haisaidii wewe ni mbunge lakini umeona upupu unaofanywa na wabunge wa ccm hata kama kitu hakina tija wanapitisha na kuunga mkono kwa kuwa ni cha ccm huko ndiko kuua chama chama hakiuwawi na rostam pekee kwa makosa yake ya kijinai chama kinauawa na makosa ya kimfumo ndiyo maana bunge liliopita liliongozwa na chadema wakati nyie mkiendelea kupinga hoja za maana eti kwa kukua tu ni za opposition na kuunga mkono ujinga wananchi wakatuhukumu gamba livuliwe bungeni wabunge wafanye kazi ya umma na sio ya ccm .lakini kumbuka kuwaomba msamaha wanavyuo uliosema wanaletwa kuzomea kumbuka watoto hao wengine wamefanya kazi ya kupigania uhuru wa nchi hii kwa uadilifu mkubwa na wamekufa maskini na heshima bila skendo viongozi wa sasa.

Mheshimiwa mkama huwezi jivua gamba kama arusha watu wanasema meya hakupatikana kihalali na watu wameuawa kujivua gamba kama mtendaji mkuu wa chama mshauri mwenyekiti wetu na rais wa jmt mh. Kikwete uchaguzi urudiwe arusha nina imani ccm itashinda na hata kama ikishindwa itakuwa na heshima zaidi kuliko tulionayo kama tupo pale kwa wizi wakura au kwa mabavu na hujuma na kulindwa na dola huku ndiyo kujivua magamba lakini nimeshangaa mwendawazimu mmoja huyo kaimu wa vijana bwana shigela anasema uchaguzi ni halali hata wakitoa saa moja uchaguzi haurudiwi huu ni uhuni ccm inakuwa chama cha kihuni nani anampa ruhusa ya kutoa kauli zenye kuhatarisha amani kiasi hiki na viongozi wa chama mnakaa kimya mkama unakaa kimya, nnauye january mwenyekti wa chama unakaa kimya kwa kauri ya uhuni namna hii wakati sisi ccm tu watuhumiwa kama tumeiba kura mimi ninakaa arusha kwa sasa wana ccm leo hii hatuifiki hata 30% ya wananchi wa arusha wenye hasira ya upatikanaji wa meya kinyemela wakiamua wanaenda kumtoa meya kwa nguvu ccm hatutaweza kuwazuia hata polisi hawataweza kuwazuia nguvu ya umma kwa hiyo mtutolee hao wahuni haraka kabla hawajakimaliza chama chetu tunahitaji watu kwa ajili ya kufikiri na wananchi wa sasa wanataka watu wanaofikiri kwa ajili yao sio kwa ajili ya ccm kwa sbb nusu ya watanzania hawana vyama na ni wapiga kura.huyu shigela hajui tunisia iliondoka madarakani kwa ajii ya kijana mmoja tu wa kimachinga alienyanyaswa na mgambo wa city ,tunataka watu wenye kufikri meya wa arusha anaweza akasababisha chama tawala kikaanguka na kutolewa madarakani kwa nguvu ya umma kama chama kitaendelea kukumbatia wahuni wa aina hii.
Naomba tujivue gamba la ukweli na sio hadaa hii ya siku 90 za rostam, chenge, na lowasa hii haina impact hata ya 5% kwa mwanacnhi aliyoko kijijini huko songea anaenunua sukari kilo tsh 2000 na petrol tsh2300.
Nawakilisha

burigi, watakusikia?
 
Well said kaka Burigi,umenena vyema,mwenye masikio na asikie,mwenye macho haambiwi tazama, tumechoshwa jamani!
 
Burigi kwa kweli umeeleza vizuri sana lakini siamini kama chama kinaweza kukusikiliza kwani bado wanaamini kwamba wananchi ni mbumbumbu. Na nafikiri Chama bado hakijamini kwamba nguvu ya umma inaweza kukitoa siku moja. Wafikirie Afrika ya Kusini, kaburu aliachia madaraka pamoja na nguvu zake zile sebuse CCM. CCM lazima iwe wazi. Kuhusu kufukuza wanachama, sioni kama ni wazo zuri kwani CCM kupitia serikali ilitakiwa kuwashughulikia hawa mafisadi kwa taratibu na sheria za nchi kisha wananchi wataona kwamba CCM imejivua gamba. Siyo kuwaomba eti ndani ya siku 90. Huo ni uzaifu mwingine wa kuchukua hatua mara moja kosa linapoonekana. Ukiwafukuza uachama watakwenda chama gani? Jibu ni kuwafilisi tu hawa watu kwani hiyo njia ilitumiwa na Mwl. Nyerere. Zaidi ya hapo ni changa la macho tuu.
 

Uteuzi wa Nauye nilimwandikia NIKIULIZA NAUYE ATAUWEZA MZIKI WA CHADEMA ni muda mfupi kama siku mbili ama tatu zilizopita nimepata yaleyale niliyosisitiza kuwa yamepitwa na wakati.Nauye kaludia yaleyale ya zama zilizopita za kukusanya watu kwa kuwshulutisha kuhudhuria mikutano na kutoa kadi za kujionyesha [Show-off].

Hakuna Kipindi cha CCM kuwa wawazi na kufanya vitu vya ukweli na sio [fake] kama kipindi hiki, si kipindi cha kushindana na CHADEMA ni kipindi cha kujishusha na kuwaludia wananchi na si kipindi cha kujikosha kwa kuonyesha hakuna athari za kichama na yaliyotekea.

Nauye anatakiwa kuendesha Propaganda za kukiludisha chama kwa mikakati mahususi ya muda mrefu na sio ya nguvu za soda alizoanza nazo tena akiwachokoza wasomi wa chuo kikuu.Si muda mwafaka kujibu tuuma zozote bali ni muda wa kujipanga ni jinsi gani HESHIMA YA CCM ITALUDI.

Cha kwanza Nauye yapaswa kitengo chako cha uenezi na Itikadi kukubali CCM imepolomoka, na kuwa kwa kukubli hilo tayari ni mwanzo wa tiba.Na imani unaweza ila watakao kuzunguka wantatakiwa wasiwe hao UVCCM waliokuvua uwanachama wa UVCCM.Unapaswa kuwa na timu nje ya waliokua kwenye mfumo huo, wapo vijana wazuri ndani ya CCM wasio na kashifa ambao wanaweza kupanga mikakati ya kisasa na kuludisha hadhi ya CCM kwenye macho ya watanzania.

Kukubali UKWELI ni mwanzo mpya Nauye si wakati wa kujibu mapigo ya Chadema ni mwanzo wa operation mpya ya kuibua ni jinsi gani wananchi wataipokea CCM bila kulazimishwa bali kwa hiari yao watahudhuria.

Yakupasa wewe na timu yako kuumiza kichwa [Kusoma Sana alama za nyakati kila siku na kujadiliana kwa umakini watanzania wasikie nini kutoka CCM.].Na pia kuwe na wasemaje ambao kwanza wanamvuto na scandalless kwenye macho ya UMMA.

Nilishauri ni wakati mwafaka kwa CCM kuwa na KITENGO CHA MASOKO NA MAHUSIANO. [Marketing and Public Relation], kitengo hiki kitawajenga nini wananchi wanataka kusikia wakati gani na nani azungumze, kwa niaba ya chama na si kila mtu.Hata kwenye mikutano kulumbana ili kujibu hoja za Chadema ni CCM kutafuta kifo chake kwa sasa, kijitume kukwepa majibu yoyote yenye nia yakuingiza CCM kwenye mtego.Ni vyema pia kukubali CHADEMA imekumbatia vijana ambao kwa sasa ni changamoto kubwa kwenye maswala ya uelewa na hivyo kuwa waibuaji wazuri wa hoja zenye kubeba maana halisi ya wantanzani hasa vijana.

Ni vyema na wakati mwafaka kuanzisha kitengo cha vijana wasomi wenye kuipenda CCM, vijana wapya wenye ufahamu ambao wao wako tayari kutetea ITIKADI ya chama cha Mapinduzi kwa HOJA kwa uelewa wa ufasaha wa kiwango cha kumueleimisha mtanzania wa kawaida wa kiwango cha dalasa la saba, na wakti huo anauwezo wa kuwakilisha mada kwa wasomi wa chuo kikuu kwa HOJA , sio kujivuna kwa kua unatoka katika chama kilichoshika dola.Vijana hawa watumike kuwepo kwenye mijadala ya kichama na jamii kuelimisha umma na wanachama kuwa sasa CCM inatoka kwenye mfumo wa CCM maslahi na kuelimisha yale yote chama kinakusudia jamii iyapate.

Zama za kada wa CCM ni vyema zikabuniwa na kupewa aina mpya ya muonekano,Kada wa CCM sio yule anayeweza kuwa mtukanaji wa mzuri wa vyama vya upinzani, kada wa CCM awe ni yule anyeweza kujitolea kwenda akufundishe Shule ya Kata kwa muda wa wake wa ziada [Party Time].

Kada wa CCm awe na kieherehere kwenye maswala ya jamii, kama ni mtaani awe ni wa kwanza kumuona mkuu wa wilaya na kuomba ufumbuzi wa tatizo la mtaa ama kata yake kabla ya jamii aijachukua hatua yenyewe, Makada wawe ni jibu sio chanzo cha matatizo.


Ni kipindi cha Nauye wewe na timu yako kujituma usiku na mchana kutembelea na kukaribisha kupokea ushauri toka kwa wanachama,Kufanya maamuzi mazito ya kuwaondoa madarakani viongozi waliotemwa na wananchi, bila kusita.

Uwazi [Transparency] ni ugonjwa kwa CCM,ni wakati pia wa kuluhusu wanachama wake kujieleza, ila wawaelekeze kama ni kiongozi au mwanachama akitoa maoni yake mwishoni mwa maojiano yake aseme NI MAONI YAKE BINAFSI NA SI MSIMAMO WA CHAMA.
 
Wabunge 19 wa CCM ni batili kwa mujibu wa Katiba ya sasa ya Tanzania; Je hilo nalo mmeliona ninyi sekretariat mpya????? Ninyi ndiyo mtaimaliza CCM na kuizika kabisa!!!!!!!!!!!!!!!!!CCM imezeeka, inanuka!!!!!!! Usanii utaiua CCM! Eleweni matatizo ya msingi na kuyatafutia ufumbuzi!!!!!!!!!!!!!! Mwalimu alitumia kweli kujenga CCM; msidhani waTz ni mazuzu tena!!!!!!!!!!!!!!!!

Sasa unamkandia huyu aliyeandika hii article au Secretariat ya CCM?Mimi nadhani hii post imeandikwa kiumakini na inasema ukweli.Ingawa nina mtizamo tofauti kuwa hao mafisadi waliotajwa wameshiriki na bado wanashiriki kuiua nchi yetu.Hao ni nguzo ya kila deal za kimagumashi.
 
Nimeupenda waraka wako mkuu, sijaona kitufe the THANKS ningekugongea. Wasiwasi wangu ni uwezo wa hao viongozi wenu wa CCM kwani hata ukiwatafunia vipi lakini huwa hawawezi kumeza. Namaanisha kuwa viongozi mliobadili hawana tofauti na mliowatoa. Angalia hoja wanazokazania majukwaani, hakuna tofauti na usanii wa Makamba na nionavyo mimi inawezekana mmewapumzisha polisi na kuweka mgambo ili walinde amali za chama chenu. kazi mnayo, yetu macho yanayosubiri kushuhudia anguko la CCM ifikapo au hata kabla ya 2015. Chama chenu kinachujuka kila kukicha na viongozi wenu wamelala usingizi wakifikiri kuwa watanzania hawaoni madudu wanayoyafanya. Kifo chema sana mnajiandalia. Hongereni
 
Kwa wale waliofuatilia Mkutano wa CCM Manzese kuna Kauli aliyoitoa January Makamba dhidi ya Wasomi wasiokuinga Mkono Chama Cha Magamba ( CCM). Makamba aliwaita wasomi Watanzania ni watu WANAOBURUZWA, YAANI WASIO JUA KUCHAGUA NI Chama kipi wakiunge Mkono na ni Chama kipi wakitose.

Yaani Implication ya January ni Kwamba Wanavyuo wote wa Vyuo Vikuu vya Tanzania ni Mazumbukuku Ulimwengu Uko Huku, ni Mazuzu wasio na Akili ya Kujiamulia.

Mpaka sasa sijasikia kauli yeyote kutoka kwa Wasomi na Wanataaluma ya Kukemea kauli hii ya Dharau kutoka Kwa Kiongozi wa CCM aitwaye Makamba. Ukimywa huu wa Wanazuoni haunifanyi niamini kwamba Makamba yuko sasa ila tu naamini kwamba wazuoni wanajipanga kulitolea Ufafanu.

Wakati nasubiri Tamko Wanazuoni Napenda kuchukua Nafasi kumtaka Ndugu January Makamba Aombe Radhi wanazuoni wote Aliowatukana Jana

Nawakilisha
 
Kwa mtaji huo kijana January anaweza kabisa kumalizia kazi aliyonza baba yake - flush ccm down the drain!
 
Back
Top Bottom