Nape asema Edward Siyo msafi

Akiongea na MakutanoShow sasa hivi ameongelea kuhusu mgombea urais kupitia CCM baada ya kuulizwa kuhusu tuhuma za rushwa zinazohusishwa na mbio za urais.

Amesema hata kama mtu akijaza wapambe wake CC na NEC siyo kigezo cha kuteuliwa kuwa mgombea urais kwa urahisi.

Alitoa mfano mara tatu kuhusu Lowassa kwamba siyo msafi na hata Nyerere alisema hivyo. Alisema kwamba siyo lazima kuwepo ushahidi bali kama watu wanaongea tu na kukuhisi inatosha kuthibitisha kwamba wewe siyo msafi.

what a load of bull s****, mbona nape akiulizwa kuhusu swala la abeid kumteka ulimboka anasema hayo ni maneno tu hakuna ushahidi...ccm bana mnapotaka nyie ndo mnaulizia ushahidi ikija lowasa mnamshambulila tu bila ushahidi...
 
Nape huyo huyo alishakaririwa akiwaita watu wanaohama CCM kuwa ni sawa na 'oil chafu'. Akesema kwani unapoendesha taasisi kubwa kama CCM ni sawa na gari ambapo hufika mahali huitaji kusafishwa kwa kumwaga oil chafu na kuweka nyingine mpya.

Kama Lowassa siyo msafi aka ni "oil chafu" si wasafishe hili gari la CCM kwa kuimwaga hii "oil chafu" na kuweka oil mpya? Kubadilisha oil mara kwa mara ni muhimu sana to keep your car running well. Over time your oil breaks down and your filter becomes clogged with contaminants.

Mfano wa oil chafu hapo chini baada ya gari kutembea miles 10,000. Ukiiangalia kwa macho tuu oil siyo safi kabisa. Kwa nini sasa iendelee kuachwa kwenye gari wakati hata aliyeunda hilo gari alishasema hiyo oil ni chafu? Wenye hii gari walituambia juzi juzi kuwa wataimwaga ndani ya siku 90 lakini wapi. Caution: take great care when working with a hot engine.


180px-This-is-oil%2C-10%2C000-miles-without-an-oil-change-on-a-10-year-old-car-6557.jpg
 
Nape amepena! Atakuwa alichelewa vitumbua nzega huyo hana lolote.
 
nape c uliswma unatoa cku 90,ss ikawaje? Leo tena unaendelea kuongea tumechoka bana!....hebu tuone km El atajibu
 
kwa pointi ya nape kuwa siyo lazima kuwe na ushahidi badi watu wakihisi na kuongea inadhihirisha uchafu wake bac anakiri chama chao kimejaa mafisadi wengi wakiwemo kina chenge,lowasa et al bt hawachukuliwi hatua.wao kama chama wanafahamu hivyo lakini hakuna uchukuaji wa maamuz magumu kwan ni kanuni zao kulea mafisadi na wezi.watasema yote mpaka tufike 2015.

kwa kuongea za mdomoni wanaweza sana. Hao watu ni wanafiki sana. Ona wale waliosaini kumuondoa pinda kilichowapata kwenye chaguzi zao.
 
Akiwa kama "mmoja wa watendaji wa chama" hana haki ya kuongelea hadharani maovu ya baadhi ya viongoz wa chama kama vile yeye ni chama kingine. Anatakiwa achukue hatua kuhakikisha hao wasio wasafi wanaondolewa chaman kama hawawez basi yeye atoke kwe nafas za utendaji kwa kushindwa kwake kuwashugulikia.
Mwanao ana tabia mbaya baba unaenda kulalama kwa jiran?huez kua mzika upstairs.

ahaa haa mkuu CCM ni chama cha kidemokrasia; kila mtu atapewa nafasi ya kujitetea; hatufukuzani kwa nguvu za baba mkwe au ukanda; Nape ameongea kwa nafasi yake na wanachama wote wanaokitakia mema chama chetu tupo nyumba yake tunamuunga mkono kwa nguvu zote; CC sio mwisho wa hatima ya wagombea wanaopachikwa kwa misingi ya rushwa na ufisadi; CCM inaelewa fika makosa yaliyofanyika ya kutosikiliza maoni ya wanachama ambao ndio wapiga kura; tumepoteza majimbo si kwasababu ya Chadema inakubalika; bali wanaccm tulitumia nguvu yetu ya kura; hivyo basi hata mimi wakiweka mtandao nipo tayari kukipigia kura upinzani hiyo ndiyo demokrasia; hakuna mwenye uwezo wa kununua kura yangu.

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Nape mzee wa kukurupuka.
Poleni sana Magamba. Waziri mkuu wenu Bwana Pinda aliwaambia eti mkiwagusa Kina Lowasa na Chenge na Rostam na wengine wanaotuhmiwa kwa rushwa kubwa kubwa taifa litayumba. Kwa maana nyingine PM Pinda na CCM a.k.a Magamba wanataka kutuambia wao hawana uwezo wa kuwapiga stop mafisadi. Hii inamaana nzuri sana kuwa kinatakiwa chama m-badala kuweza kushughulika na mafisadi Edward Lowasa na huyo pumbafu anayekwenda kuhongwa hela kwaarabu(Libya, Oman na kwingineko). Nichama gani hicho zaidi ya vuguvugu la mabadiliko? Huko hawacheki na kima. Hawaogopi mafisadi wala mama yake Fisadi.:mad:
 
Akiongea na MakutanoShow sasa hivi ameongelea kuhusu mgombea urais kupitia CCM baada ya kuulizwa kuhusu tuhuma za rushwa zinazohusishwa na mbio za urais.

Amesema hata kama mtu akijaza wapambe wake CC na NEC siyo kigezo cha kuteuliwa kuwa mgombea urais kwa urahisi.

Alitoa mfano mara tatu kuhusu Lowassa kwamba siyo msafi na hata Nyerere alisema hivyo. Alisema kwamba siyo lazima kuwepo ushahidi bali kama watu wanaongea tu na kukuhisi inatosha kuthibitisha kwamba wewe siyo msafi.

Nape pamoja na uvuvuzela wake, bado anaonekana kuwa na ujasiri mkubwa ambao wanaCCM wengi wanakosa. Hakuna anayeweza kumnyooshea kidole wazi wazi Lowasa. lakini Nape anaonekana kuthubutu. Mukama, Samweli Sitta, na wengineo wamenywea. Amekosa tu kuunda timu ya kumsaidia maana wengi waliokuwa upande wake kama akina Samwel Sitta ni ndumila kuwili na wanafiki maana juzi juzi tu Samweli Sitta ameongea huko Moshi kwamba CCM baada ya kikao cha sasa imeimarika zaidi tofauti na matarajio yangu kwamba yuko kundi la Nape.
 
kwa hili nakuunga mkono nape,amwe watanzania tusikubali lowasa aweke bei yetu, yaani kwa sasa ameshamaliza kununua uongozi wa ccm, sasa naelekea kwangu mimi na wewe, je wewe una bei? mimi sina bei, pia nape hana bei na amejidhihirisha ivo. au unampenda membe, au unampenda slaa, haijalishi, kwa kuwa wote tunaipenda tanzania. lowasa hata kama angekuwa na uwezo wa kuhutubia masaa 12 bila wasikilizaji wake kumchoka amekosa sifa kwa kuwa

1. hata baada ya kutabiriwa na wachungaji matapeli kama TB joshua, bado hajauamini utabiri huo kwa kuwa ameendelea kununua kura ili aendeleaa kusogea ikulu, hana imani hata chembe zaidi ya ulafi wa madaraka

2. jk nyerere alishatuonya mapema kuhusu mtu huyu

3 kuna watanzania tena ma=profesa wanashabikia eti tujaribu dikteta, ni sawa , lakini dikteta mwizi ni hatari zaidi wote manjua loiwasa ni mwizia anayesubiri kufikishwa kisutu kuhusu ricmond et la
 
Watz ni wavivu wa kufanya hata utafiti mdogo tu kama hii habari ya EL. Sikilizeni enyi msioona mbali:-

1. Kwamba EL si msafi halipingiki. Nape yuko sahihi kusema hivyo lakini pia ni kichekesho kuwa yeye na Katibu Mkuu walipiga 'U turn' ya ajabu kukana ultimatum ya zile siku 90 ambazo EL na wenzake walipaswa kujiengua wenyewe kusafisha chama. Nape na wenzake wamezidiwa kete na kuonekana chochote wanachokiongea sasa kuwa hakina ukweli kwa sababu it is ironically useme mtu si msafi na kweye CC mumpitishe hadi kugombea uNEC na hakuna mahala mmemjadili na kumchukulia hatua kichama. Hayo yataonekana kuwa majungu.

2. Utafiti wangu unanionyesha kuwa EL kamwe hataweza kupitishwa jina lake kuwa mgombea maana CCM si wajinga mnavyodhani. Kwa sasa, jina lake linatumika ili msiwafikirie wenzake ambao hamuwasemi na katika hao atatajwa mmoja na ndipo mtashangilia (mazingaombwe ya Mwanakijiji) kuwa EL amekomolewa kumbe ndivyo ilivyopangwa. Ni hivi EL hana ugomvi na Rais Kikwete wala Membe wala Migiro. Na hata siku moja hutamsikia Rais wetu wala Membe akisema hayo wazi wazi. Hawa wako pamoja sana na ndio maana ya kuwa na mikakati ya muda mrefu na ambayo huwezi kuipredict kiurahisi kama wenzetu wa CHADEMA wanavyotake political risks bila kuzichambua.

3. EL yeye hana shida ataendelea kula pension kama EX-Premier na atakuwa ndani ya NEC, ndani ya CC na Mbuge wa huko kwake kwa hivyo yuko safe & liquid kona zote. Na atakuwa Mweyekiti Kamati ya Bunge na Bodi zenye mashiko ya posho, haitaji Urais. Sana sana wakiona hata mmepumbazika kwa kumhurumia eti jina lake kutopitishwa kwenye Urais basi Rais ajaye kwa kuwa ni mtu wake anampa uWaziri wa nguvu basi mnabaki kung'ang'aa macho kuwa kaonewa kumbe ndivyo ilipangwa!

4. Kosa kubwa linalofanywa na upizani ni hili.
Kwanza hamko wamoja kwa hiyo hata kwenye fair ground ikipigwa kura leo wale wasioipenda CCM wanagawanyika kati ya CHADEMA, CUF, NCCR n.k wakati wapenzi wa CCM wao watafia hapo hapo hasa WATAKAPOONA KUWA JINA LA ANAYEPEPERUSHA BENDERA YAO SI EL ALIYEWAUMIZA WENGI KWENYE CHAGUZI ZA NDANI BALI NI MWINGINE MSAFI ( MIGIRO, MAGUFURI, MEMBE etc) jambo ambalo si kwa sababu za mnyukano bali mpango wa muda mrefu.

Pili uchaguzi wa kumpata rais ni wa nchi yote kila kitongoji na si maeneo machache tu ya nchi. Uchaguzi Mkuu ni zaidi ya political rally za M4C mkoa fulani au kanda fulani. Unahitajika kuwa na watu wengi kila kitongoji nchi nzima ambao wanaushawishi kwa wengine na pia kuwasimamisha wagombea Ubunge kote nchini kila kitongoji kama wafanyavyo CCM. Sasa angalia CCM imepanua wigo wa ujumbe wa NEC toka mkoa hadi kila wilaya TZ nzima na hao wanaochaguliwa wanaushawishi fulani wa ama kiuwezo au hata kifedha na pia wana marafiki wao na ndugu zao ambao ndio watawapigia debe CCM (Kimya kimya au kwa uwazi). Chaguzi za CCM Mikoani na za Jumuiya zake UVCCM, Wazazi na UWT ni mtandao tosha ambao unafanya hata CHADEMA na CUF humu wanajadili habari za mama Simba vs mama Malecela bila kujijua mpaka wanasahahu kuwa kuwa BAWACHA au Baraza la Wanawake wa CUF n.k.

Swali ni kuwa mbona hatuoni maandalizi ya namna hii ya mfumo wa kutafuta wawakilishi wa jumuiya za vyama vingine vya upinzani katika mtandao mpana kama huu wa CCM Tanzania nzima (haijalishi kuwa hata kama wa CCM pia una mapungufu lakini unaibua ushindani mkubwa sana).

5. Sikiliza CHADEMA, hakuna ubishi Dr. Slaa ni jembe na anapendwa lakini uchaguzi ni maandalizi ya kuwa na mtandao wa kupata watu wengi (Bara na Visiwani) wawakilishi watakaomsaidia nchi yote kuwashawishi watu wengine waone kuwa kweli huyu akipewa chi kama Rais basi si kwamba itakuwa yake na kakundi kake kadogo kwa Mbowe, Lissu, Mnyika, Mdee bali kwamba kuna watu wengi nchi nzima (bara na visiwani) wenye uwezo kuendesha Wizara zote na Mikoa yote bila kutikisika.

6. Mwisho, ni bayana pia kuwa hata thread za Zitto na mikwara mbuzi yake ya kuutaka Urais ni kanya boya akitegemea kuzua tafrani CHADEMA maana anatumika. Tunashukuru kuwa hilo limejulika kwa wengi sasa maana amepwaya na ataishia kuwa looser tu kwa kuwatumikia mabwana wawili na kamwe hatasimamishwa na CCM (hata akihama leo CHADEMA) kuwa mgombea na wala hakuna mgombea binafsi anayeweza kupita kuwa rais leo Tanzania ; demokrasia yetu haijafikia hatua hiyo hata Marekani bado!

EL si mgombea urais, anawaandalia watu wake makao ili naye aendelee kufurahia utukufu wa mtandao wake. WaTz hatupendi kujishughulisha na kuchambua kwa undani mambo ya juzi na kesho bali ya leo tu!!!
Mfano, leo Mh. ShyR Banji ametaka kutwangana na Mh. mama Simba kwenye uchaguzi wa UWT. Hivyo atakuwa na hasira naye na pia pia EL kwamba ndiye alikuwa sponsor wa mama Simba lakini kesho atasimamishwa mama Rose Migiro, msomi na hana tuhuma, Banji atakuwa wa kwanza kumpigia hata kampeni Tz yote kwa jina la kumkomoa EL hahahahahahahahahah!!!

Sitaki kusikia mtu akilialia baada ya uchaguzi mkuu (2015) kuwa tumeibiwa kura!!!! Mtu anajiibia kura yeye mwenyewe kuanzia sasa kutegemeana na mfumo wa maandalizi yake.

Ombudsman, niko huru na niko tayari kutoa msaada wa kweli kwa ajili ya maendeleo ya nchi yangu Tanzania.
 
TUTAPIGA KELE SANA NA KUTOA MAPOVU TUKIWA NYUMA YA PC,IPAD na PHONE ZETU LAKINI KIUHAKIKA NAONA HUYU BWANA EL ANAKUA RAISI WA NCHI HII, SITAKI KUAMINI HILI LAKINI TAYARI UKIWA MTU MAKINI UNAONA KABISA HUYU BWANA ANACHUKUA NCHI HII, WENGI MTAPINGA NA KUSEMA IN A NEGATIVE WAY LAKINI UKIWA MAKINI UTALIONA HILO, SI DHANI KAMA WATU HAWA MNAO SEMA NI VIBARAKA WAKE WANAOPITA KWA KUSHINDA KWA VISHINDO VIKUBWA KAMA BOM LA B52 NI WAJINGA KUMCHAGULIA MTU WAKE.

NI UKWELI CHADEMA WATALETA UPINZANI MKUBWA, LAKINI KWA HULKA YA WATANZANIA WA LEO WANO ONA KILA MTU ANAKULA KWA UREFU WA KAMBA YAKE WATAKUBALI KUFUATA USEMI WA KUWA MKONO MTUPU PIA ULAMBWA, HILI BADO NI TATIZO KUBWA SANA. NA NJIA HII ITATUMIKA KUWAANGUSHA WAPIGANIA UKOMBOZI, AMA KWA HAKIKA NIVIGUMU KWA MTANZANIA WA LEO ALIOPO NYARUGUSU,NAMTUMBO NA KUNGINEKO UKAMUAMBIA AMCHAGUE MTU ATAKE MLETEA MAENDELEO YA UKWELI BILA KUMPA CHOCHOTE....COZ WAO WAMEZOEA HIVYO NA HII IMEDHIHIRISHWA NA HUYU BWANA NA WATU WAKE. PIA WABUNGE WENGI WAMEDHIHIRISHA KUA WAKICHAGULIWA WANAJINUFAISHA WAO KWA KUOMBA UJIRA MKUBWA, WANANCHI NAO WANAONA NJIA PEKEE YA KUPATA UJIRA TOKA KWA MBUNGE NI RUSHWA NA SIO POROJO NA AHADI UCHWARA ZA KUA MABOMBA YATA TOA MAZIWA NA KILA MMOJA ATAPEWA CARD AWE ANAKULA BURE KFC.

KWA KIFUPI.....
MPANGAJI ALIOKO IKULU HATAMBUI KUA MWENZAKE KAISHA LIPIA KODI NA ANAMSUBIRI AFUNGE VIRAGO NAE AINGIE, NA MPANGAJI HUYO ALIOKO IKULU ANAHISI BADO BABA MWENYE BYUMBA HAJA PATA MPANGAJI MPYA

MUNGU TUNUSURU NA UTUPE HEKIMA KATIKA KUIKOMBOA NCHI YETU,....
 
Hata hivyo msafi ni nani CCM? tusiumize vichwa sana tuendelee kusubiri siku ifike... zaidi tumuombe Mungu asaidie maana sisi wenyewe hatuwezi sasa.
 
Nape huyo huyo alishakaririwa akiwaita watu wanaohama CCM kuwa ni sawa na 'oil chafu'. Akesema kwani unapoendesha taasisi kubwa kama CCM ni sawa na gari ambapo hufika mahali huitaji kusafishwa kwa kumwaga oil chafu na kuweka nyingine mpya.

Kama Lowassa siyo msafi aka ni “oil chafu” si wasafishe hili gari la CCM kwa kuimwaga hii “oil chafu” na kuweka oil mpya? Kubadilisha oil mara kwa mara ni muhimu sana to keep your car running well. Over time your oil breaks down and your filter becomes clogged with contaminants.

Mfano wa oil chafu hapo chini baada ya gari kutembea miles 10,000. Ukiiangalia kwa macho tuu oil siyo safi kabisa. Kwa nini sasa iendelee kuachwa kwenye gari wakati hata aliyeunda hilo gari alishasema hiyo oil ni chafu? Wenye hii gari walituambia juzi juzi kuwa wataimwaga ndani ya siku 90 lakini wapi. Caution: take great care when working with a hot engine.


180px-This-is-oil%2C-10%2C000-miles-without-an-oil-change-on-a-10-year-old-car-6557.jpg

Nape nae ni oil chafu imeshindwa kuendesha gari la ccm kwa kushindwa kuwawajibisha mafisadi amwagwe iwekwe nyingine.
 
akiongea na makutanoshow sasa hivi ameongelea kuhusu mgombea urais kupitia ccm baada ya kuulizwa kuhusu tuhuma za rushwa zinazohusishwa na mbio za urais.

Amesema hata kama mtu akijaza wapambe wake cc na nec siyo kigezo cha kuteuliwa kuwa mgombea urais kwa urahisi.

Alitoa mfano mara tatu kuhusu lowassa kwamba siyo msafi na hata nyerere alisema hivyo. Alisema kwamba siyo lazima kuwepo ushahidi bali kama watu wanaongea tu na kukuhisi inatosha kuthibitisha kwamba wewe siyo msafi.

i hate those who hate el!!
 
Watu koungea tu bila ushahidi inatosha kumtia mtu hatani? Nape acha utani, kama hivyo ndivyo unavyoamini basi hujui utawala wa sheria
 
Akiongea na MakutanoShow sasa hivi ameongelea kuhusu mgombea urais kupitia CCM baada ya kuulizwa kuhusu tuhuma za rushwa zinazohusishwa na mbio za urais. Amesema hata kama mtu akijaza wapambe wake CC na NEC siyo kigezo cha kuteuliwa kuwa mgombea urais kwa urahisi. Alitoa mfano mara tatu kuhusu Lowassa kwamba siyo msafi na hata Nyerere alisema hivyo. Alisema kwamba siyo lazima kuwepo ushahidi bali kama watu wanaongea tu na kukuhisi inatosha kuthibitisha kwamba wewe siyo msafi.
Nafikiria jinsi Nape atakavyoonekana akitiwa POLONIUM maana mwenyewe alivyo kama ametiwa mkorogo. Natamani kufa nisiione tanzania ajayo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom