Nape ana wadhifa gani SERIKALINI?

Malova

JF-Expert Member
Apr 21, 2011
784
228
Taarifa kwa umma juu ya uamuzi wa Raisi kutengua baraza lake la mawaziri ilitolewa na Nape Nnauye. Binafsi sielewi, yeye ana wadhifa gani serikalini? Viongozi wengine au idara ya mawasiliano ya Ikulu ilikuwa wapi mpaka yeye atoe taarifa ya Serikali kwa umma kupitia vyombo vya Habari? Lakini pia uamuzi wa kutengua baraza unafanywa kupitia kamati kuu ya CCM, yenyewe kama nani Serikalini? Mwenye kujua anieleweshe.
 
ni kutengeneza vitisho ili watakao teuliwa waendelee kukichangia chama kwa rasilimali za umma,,,kuonyesha jeuri ya chama kwa viongozi,,wengi walishaanza kuwapuuza,kutowapa mafuta ,kuwakirimu,kuwachangia,,,,huon,hapo kuna wengine watamuomba awapigie debe,,,,ccm bwana,,,,,:rockon:
 
Kimsingi taarifa za kulisuka balaza la mawaziri hazikupaswa kutolewa na nape kupitia waandishi wa habari kwa umma. Nape kama kiongozi ndani ya chamachake walipaswa kuchagua watu wanaowataka na kupeleka taarifa hiyo kwa kurugenzi ya ikulu ili kutoa taarifa kwa umma. Tunatambua kuwa mawaziri na manaibu wanatoka ndani ya CCM. Kurugenzi ya ikulu haiwezi kutoa taarifa ya mabadiliko toka baraka ndani ya chama. Ninachokiona ni Nape kukurupuka kwa kutaka kujipa na kukipa umaarufu ccm kuwa ndio wamefanya maamuzi hayo. Nape alipaswa kupeleka taarifa kurugenzi ya ikulu na hao ndio wangetoa taarifa kwa umma.
 
Ni mkuu wa wilaya ya Masasi

Labda useme ni mkuu wa wilaya mstaafu! na pia ni msemaji wa chama tawala. Lakini bado hastaili kutoa taarifa za serikali. Ule umbea wa mabadiliko ya mawaziri aliotupa, ilikuwa ni taarifa ya Kamati kuu ya CCM - CC. Tusubiri ofisi ya rais nayo inaweza ikawa na chochote.
 
hawaelewi mipaka ya chama au ya serikali . na hii inatokana na kutokuwa na maadili ya uongoz na pia mgawanyo wa madaraka
 
Nahisi ni MC wa CC ya CCM si unakumbuka kile kikao kingine cha CC kilichoweka mikakati ya kuvua magamba huyu huyu Nape akataja majina matatu lakini akaja akakana na kusema ' waandishi wa habari walimnukuu vibaya' akasahau kuwa tuliidaka hiyo na kuiongeza kwenye CV yake kwamba inawezekana sana ni Incompetent au hasimamii anayo yaamini. Hvyo tusimruhusu atake mind zetu kwa hili la mawziri, hakawii kujeuka kuwa hajasema...

Never allow a person to tell you "no" who doesn't have the power to say "yes."
 
Taarifa kwa umma juu ya uamuzi wa Raisi kutengua baraza lake la mawaziri ilitolewa na Nape Nnauye. Binafsi sielewi, yeye ana wadhifa gani serikalini? Viongozi wengine au idara ya mawasiliano ya Ikulu ilikuwa wapi mpaka yeye atoe taarifa ya Serikali kwa umma kupitia vyombo vya Habari? Lakini pia uamuzi wa kutengua baraza unafanywa kupitia kamati kuu ya CCM, yenyewe kama nani Serikalini? Mwenye kujua anieleweshe.

mmh hii nchi inaongozwa na matakwa ya mtu nawala si kwa taratibu na kanuni za utawala
 
hii ni dalili ya ukosefu wa uongozi bora na imara ndani ya serikali.
Kwa maana hiyo basi inabidi tu chama ndicho kishike atamu za uongozi.
 
sasa kama chama kinafanya vikao vyake state house ndo watashindwa kiongozi wa chama kutoa habari ya serikali?,na ninavyohisi ni nape huyuhuyu atakayetutangazia baraza jipya la mawaziri
 
Back
Top Bottom