Nape amfananisha na punda mbunge wa Iringa mjini (Peter Msigwa)

Syo hawajajitambua we unakosea kichaa hajitambui, ila htambuliwa na watu baada ya kuchafuka, sasaa hawa ni vichaa wapya bado hawajafuka subiri kidogo tu wachafuke then dunia nzima itawatambua kuwa ni vichaa bila hata kuambiwa, na wenzao tume ya katiba ritz rejao ,zomba au zombo na wengine wengi....
Kichaa sio lazima aokote makopo,wewe na nape wote vichaa ambao amja jitambua,nyambafu.
 
Hawa magamba kweli hawana ishu maana kwa jinsi ninavyolijua soko kuu la Iringa sijaona sehemu ya kufanyia mkutano wa hadhara, au ilikuwa na wa ccm tu! Kweli mfa maji hakosi kutapatapa. Cdm for life
 
Katibu wa itikadi na uenezi Nape Nnauye amesema mchungaji Peter Msigwa ni sawa na punda kwenye kundi la ng'ombe na kwamba anawabebea mizigo CCM lakini 2015 watamuondoa asije akawaambukiza magonjwa ng'ombe wao.Amesema hayo leo katika mkutano wa hadhara uliofanyika sokokuu la manispaa ya Iringa

nape anatia huruma kwani analamba matapishi ya cdm kila wanakotia maguu wakiondoka nae anaenda kwa style ya kuwabeba watu kwa malori na bado hawapati kaishiwa sera na hoja sasa anaishia kufananisha watu na vitu ambavyo havipo wala kufikirika, oh mara oil chafu mara kinyago na sasa punda. Kama siasa imemshinda akafanye kilimo kwanza nacho kitamtoa kwani siasa ndo basi tena kwake
 
hivi nape ana IQ ya ngapi?hivi hakuna kijana mwingine ambaye anaweza kuchukua mikoba ya huyu mtu?....

Kwa bahati mbaya ccm hawana kijana mwingine zaidi yake maana kijana anaemfuta ndo makamba
 
Muda si mrefu tutamkuta nape kwenye mipasho badala ya siasa!
 
japo ni siasa bt kwa nafasi ya nape na ili kuhakikisha wanarudi magogoni 2015 hazitasaidia ameacha kuwaeleza wananchi utekelezaji wa ilani ya ssm lakini sio biashara za ngombe na pundamilia
 
Katibu wa itikadi na uenezi Nape Nnauye amesema mchungaji Peter Msigwa ni sawa na punda kwenye kundi la ng'ombe na kwamba anawabebea mizigo CCM lakini 2015 watamuondoa asije akawaambukiza magonjwa ng'ombe wao.Amesema hayo leo katika mkutano wa hadhara uliofanyika sokokuu la manispaa ya Iringa

katibu wa itikadi na uenezi wa Chama cha mapinduzi ( CCM) Taifa Bw. Nape Nauye amekiri kuwa CCM ilipoteza jimbo la Iringa mjini kwa makosa yake na kuwa kosa hilo kamwe halitarudiwa tena na kumfananisha mbunge wa jimbo hilo Mchungaji Peter Msigwa kuwa ni msindikizaji wa CCM katika jimbo hilo.


Kwani alisema kuwa kosa lililofanyika katika uchaguzi mkuu mwaka 2010 kwa kushindwa kuongoza kura za ubunge ni kutokana na makosa yaliyojitokeza hivyo kupelekea madiwani kushinda na Rais Jakaya Kikwete kupata ushindi mkubwa ila ubunge baada ya yule waliomchagua wana CCM Frederick Mwakalebela jimbo hilo lilichukuliwa na upinzani kosa ambalo kamwe halitarudiwa tena.


Asema vyama vya upinzani ni vyama vya wanaharakati kwa ajili ya kuikumbusha serikali ya CCM kwa pale inapokosea na sio kuja kuongoza nchi.


Pia Nauye aliuagiza uongozi wa serikali ya mkoa wa Iringa kuhakikisha unafungua mara moja barabara ya Magereza inayoelekea Hospitali ya mkoa ambayo imekuwa ikichangia usumbufu wa wagonjwa Kwenda kutibiwa.


Akiwahutubia wakazi wa jimbo la Iringa mjini katika viwanja vya Soko kuu Leo ,Nauye alisema kuwa moja Kati ya kilio kikubwa kwa wakazi wa mji wa Iringa ni hatua ya uongozi wa Magereza Iringa kuifunga barabara hiyo kwa ajili ya matumizi ya Magereza mkoa wa Iringa jambo ambalo linasababisha usumbufu kwa wananchi wanaofika Hospitali hiyo ya mkoa.


Hivyo alisema tayari amemwagiza mkuu wa mkoa wa Iringa DKT Christina Ishengoma kuhakikisha anasimamia zoezi hilo ili barabara hiyo ifunguliwe na kupunguza kero za wananchi na wagonjwa wanaofika kutibiwa katika Hospitali hiyo ya mkoa.


Aidha Nauye amewacharukia madaktari wa Hospitali za umma ambao wameendelea kuichafua serikali iliyopo madarakani kwa kushindwa kutoa dawa kwa wagonjwa na kuwaelekeza maduka yao kwa ajili ya kununua dawa hizo.


Alisema kuwa kumekuwepo na utaratibu mbaya kutoka kwa baadhi ya madaktari na wauguzi kushindwa kuwapa dawa wagonjwa wanaofika kutibiwa na badala yake kuwaandikia dawa hizo na kuwaelekeza maduka ya Kwenda kununua dawa hizo maduka ambayo yanamilikiwa na madaktari hao.


Hivyo alitaka madaktari wanaofanya hivyo kuacha Mara moja Kwani kuendelea kufanya hivyo ni kuwanyanyasa wananchi hao ambao wanafika kutibiwa.


Akielezea kuhusu bajeti ya mwaka 2012/ 2013 Nauye alisema kuwa bajeti ya serikali ya sasa imepunguza utegemezi kutoka asilimia 42 hadi asilimia 26 pekee hivyo aliwataka wapinzani kuacha kufuru kwa kuponda bajeti hiyo.


Alisema kuwa katika bejeti ya miaka ya nyuma ilikuwa haiweke bajeti ya ndani ila kwa sasa serikali imetenga bajeti ya maendeleo zaidi ya trioni 2 ambayo pia wapinzani walipaswa kuizungumza badala ya kuendelea kukosoa hata pale serikali inavyofanya vema.


Pia alisema kuwa vyama vya upinzani vinapaswa kuendelea kusema unwell zaidi badala ya kuendelea kufanya siasa ya kudanganya umma wa watanzania kwa mambo ambayo yanaukweli .


Katika hatua nyingine Nauye alivitaka vyama vya upinzani kuendelea kuifanya kazi ya katakana CCM huku CCM ikiendelea kuchapa kazi na kudai kuwa vyama vya Upinzani ni sawa na kuku wako kumshikia manati na kudai kuwa wapinzani wote walitoka CCM hivyo iwapo CCM wachafu hata wao wamegoma huku.

Kwa upande wake mstahiki meta wa Manispaa ya Iringa Amani Mwamwindi alisema kuwa uongozi wa Manispaa ya Iringa umeendelea kujenga barabara za mji huo katika kata zote 14 ikiwa ni pamoja na kuendelea na kuboresha huduma za afya.

Alisema kuwa kutokana na msongamano wa wagonjwa katika Hospitali ya mkoa wa Iringa uongozi wa Manispaa ya Iringa ulimwomba Rais Jakaya Kikwete kusaidia kiasi cha shilingi milioni 600 ambazo zimefanikisha ujenzi wa Hospitali ya Manispaa ya Iringa eneo la Frelimo ,Hospitali ambayo imeanza kazi.
 
Matusi, Uzushi, Ubinafsi, Rushwa, Ufisadi, Umbea, Makundi, Wizi, Matumizi mabaya ya Madaraka, uongo imekuwa ni sera KUU ya kudumu ccm.
 
Miaka 50 ya sera za Matusi za serikali ya ccm zina karibia ukingoni sasa
 
ao.jpg

Nape anasemaje na hii ni oil chafu?
 
Miaka ya nyuma tulizoea kusikia vyama vya upinzani vikitumia maneno makali (matusi) kufikisha ujumbe, na tuliamini kabisa kuwa vyama hivyo havijakomaa na vinahitaji muda vitakua na kuacha maneno hayo.

Sasa hivi ni ssm ndo wameamua kurudi ktk utoto na kuanza kutukana majukwaani huku vyama vya upinzani vikijieleza na kunadi sera zake kwa ufasaha kabisa.

vimekuwa vikiwafungua waTZ macho na kuwapa uelewa wa mambo yote yanavyokwenda ktk nchi hii.

Sasa nadhani ssm imekosa mwelekeo na inajiandaa kurudi kule wenzake walipotoka.

Huu ndo mwisho wa chama tawala? cjajua mbado!
 
Katibu wa itikadi na uenezi Nape Nnauye amesema mchungaji Peter Msigwa ni sawa na punda kwenye kundi la ng'ombe na kwamba anawabebea mizigo CCM lakini 2015 watamuondoa asije akawaambukiza magonjwa ng'ombe wao.Amesema hayo leo katika mkutano wa hadhara uliofanyika sokokuu la manispaa ya Iringa

Hii nayo ni sera.....huyu kijana ni mjinga sana wananchi wanataka kusikia habari za maendeleo si porojo na mipasho.....aache kuzungumzia watu na personalities zao huyu Kijana wa CCJ ana kazi ya kumoboa Magamba
 
Msigwa Usilipize ubaya wowote.Mungu aliyetengeneza njia ataendelea kutengeneza hata 2015.CCM hawajasikia kilio cha Watz
 
Mimi ninachokiona hapa kuhusu Nape ni ile hali ya ilimradi liende, huyu jamaa anajua fika kuwa chama kina kuwa imara pale kinapokuwa na mass popularity, na ili aweze kudhoofisha psychologia za wachache lazima aongee maneno kama hayo. Ushauri wangu kwa Nape ni Huu. Kama anafikiri vyama hivi vya upinzani ni wanaharakati wa kukumbusha CCM kuwajibika kwa wananchi, hana sababu ya kutoa mapaovu majukwaani kwani wanaharakati hawana nguvu yoyote ya kimageuzi. Lakini kama anaona huu moto wa M4C ni wa kudumu na wamabadiliko ya kweli, basi atulie afanye shunghuli zake, kwani hata kama anasema eti '' hata kama watahama wanachama wote wa ccm na kuhamia upinzani, yeye peke yake tabaki kukikomboa chama'' Haya ni maneno ya mtu ambae hajui anachokisema( Samahani) Lakini pia ni hali ya kijikosha ili uonewe huruma. Kumwita mwenzako ni ' Kama Punda wa mizigo au Oil chafu, yote ni maneno tu yakutamkwa ambayo hadhuru wala hayamuondolei mtu UTU, lakini kumbuka wote tuna karibia mto na unaanza kutukana mamba kabla haujauvuka.... Cha msingi ungetulia tu kaka yangu, wasijekukutumia kama vuvuzela ukajakosa matamu mbele ya safari..... Nawasilisha.
 
Katibu wa itikadi na uenezi Nape Nnauye amesema mchungaji Peter Msigwa ni sawa na punda kwenye kundi la ng'ombe na kwamba anawabebea mizigo CCM lakini 2015 watamuondoa asije akawaambukiza magonjwa ng'ombe wao.Amesema hayo leo katika mkutano wa hadhara uliofanyika sokokuu la manispaa ya Iringa

siasa si mchezo wa kuigiza.

chama ukipendacho ni lazima ukipiganie
 
Ukimwona baba anang'ang'ania kujitambulisha mbele ya watoto (eti mimi ndo baba yenu) au mkewe (mimi ndo mume wako) ujue kuna shida kubwa inamsibu baba huyo; nape kulikoni kujitambulisha eti unamliki punda anayekubebea mzigo???
 
Back
Top Bottom