Nape alipotembelea Tanzania Daima

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797


Katibu wa Nec, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye akizungumza na viongozi wa magazeti ya kampuni ya Free Media Ltd, wachapishaji wa magazeti ya Tanzania Daima na Sayari, alipotembelea ofisi za magazeti hiyo mjini Dar es Salaam. 4/7/2007. Kulia ni Mhaririri Mtendaji wa Kampuni hiyo, Absalom Kibanda.


Tuesday, July 05, 2011




Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye akizungumza na Mhariri Mtendaji wa magazeti ya Kampuni ya Free Media Ltd, wachapishaji wa magazeti ya Tanzania Daima na Sayari, Absalom Kibanda alipotembelea ofisi za magazeti hiyo mjini Dar es Salaam. 4/7/2007. Kushoto ni Naibu Mhariri Mtendaji wa kampuni hiyo, Asbert Ngurumo
Nape akiwa katika chumba cha habari cha gazeti la Tanzania Daima, alipotembelea ofisi za gazeti hilo 4/7/2011. Wapili kilia ni Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Free Media Ltd, Abnsalom Kibanda.

Nape akimsalimia mpigapicha mwandamizi wa kampuni ya Free Media. Francis Dande wakati wa ziara hiyo. Wapili kulia ni Mhariri Mtendaji wa kampuni hiyo Absalom Kibanda


Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye akiagana na Mhariri Mtendaji wa Free Media Ltd, Absalom Kibanda baada ya ziara katika ofisi za kampuni hiyo 4/7/2011. Katikati ni Naibu Mhariri Mtendaji wa kampuni hiyo Asbert Ngurumo.

Mwandishi wa Tanzania Daima Irene Mark akiwa kazini wakati wa ziara hiyo ya Nape
 
In a Free Media Nations Hajawahi kutokea Mpiga Debe wa Chama Tawala anatembelea Magazeti yote yanatoa habari Nchini

Kwa CCM huu ni Mpango wa kuyafanyia nini hayo Magezeti?
 
Ungetumege basi yaliyojiri katika hayo mazungumzo yao mkuu tukawa na uwanja mpana wa kuchangia.
 
Ungetumege basi yaliyojiri katika hayo mazungumzo yao mkuu tukawa na uwanja mpana wa kuchangia.
Tanzania Daima hana cha kusema, alipokwenda Mwananchi ndio alisema Mengi kuhusu Gamba, Mwezi Ujao Mkutano wa NEC n.k

Tanzania Daima hakwenda na Utitiri wa Wapambe kama Magazeti Mengine...
 
- Saafi sana Nape anaonyesha kuheshimu upande wa pili pia, ndio modern politics hizo, so yupo 100% right on the track!

Willie @ NYC, USA.
 
NNAPE hata ukitembelea magazeti yote TZ hautaweza kuwazuia kuanika uozo wa CCM, kikubwa gamba hili.
 
Mbona huyo Irene Mark kajikwatua sana? Anataka kumtega au... lol
 
Anajitahidi sana kufanya mambo KISOMI,lakini tatizo ni kwa hao watendaji na mambo yanayoendelea,leo hii ujinga unaoendelea hapa nchini NAPE ataongea hadi povu limtoke,maana watz nao wanaonaaaaa........unadhan media zitaandika mazuri ya chama........
- Saafi sana Nape anaonyesha kuheshimu upande wa pili pia, ndio modern politics hizo, so yupo 100% right on the track!Willie @ NYC, USA.
 
- Saafi sana Nape anaonyesha kuheshimu upande wa pili pia, ndio modern politics hizo, so yupo 100% right on the track!

Willie @ NYC, USA.

Ulisema Nape ni mtu makini na unamwamini, ulikubaliana naye kwenye sarakasi za siku tisini za kuvuliwa mapacha magamba. Kiko wapi sasa???? Siasa za chumbani zimetoka nje hapatoshi.
 
Nionavyo mimi Nape hana tatizo, tatizo ni chama alichoingia huyu bwana ndo maana mpaka leo hii nae aonekane FISADI. Halafu naona jamaa kama shavu limemtoka....
 
Pale anaomba nini toka freemedia??au anaomba fair game kwenye uchaguzi wa igunga??anasawazisha uwanja wa mipra kwa uchaguzi ujao??sidhani kama itasaidia labda kama anataka kuwanunua kwa mlango wa nyuma!!anyway ziara njema ila usipotoke na kupagawa wakiandika ukweli kuhusu magamba...akadhani wamemgeuka
 
Back
Top Bottom