Nape ajibu makombora ya Marando

Gosbertgoodluck

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
2,855
401
Jamani,

Huyu bwana mdogo naona amekuja na staili inayoweza kumwingiza kwenye kundi moja la wazee wa taarabu tuliowazoea la mzee Yusufu Makamba na Tambwe Hiza.

Katika siku za hivi karibuni nimeona kasi ya Nnape ya kuropoka na kubwabwaja kama kasuku imeongezeka kiasi cha kutilia shaka uwezo wake katika kukiletea mabadiliko chama chake kilichompatia dhamana ya uongozi.

Sasa ameibuka na kauli yake kwamba Dr. Slaa ni fisadi! Yeye anadhani watanzania ni watoto wanaoweza kudanganywa na kauli nyepesi nyepesi hivyo!!!

Sasa nimeanza kuamini maneno ya watu waliobeza slogan ya kujivua gamba kwamba nyoka akijivua gamba anabaki kuwa nyoka. Na ndivyo ilivyo kwa CCM.

Mwanzoni, nilidhani sasa tutaanza kusikia kauli zenye mashiko kutoka kwa huo uongozi mpya wa ccm ulioingia baada ya kile kilichoitwa kujivua gamba. Nilijua nyimbo za taarabu zitakuwa zimeisha.

Kumbe wapi, kilichobadilika ni wanamuziki tu, hivi ni kweli ccm imeishiwa watu wa maana wanaoweza kuongoza chama professionally?
 
CCM ,hawana hao watu wa kuongoza chama, professionally , hapo kuchagua NAPE, wamefikiria kweli, ndo wakamuona anafaa kuwa kiongozi wao.
 
Wadau katika gazeti la mtanzania Nape Nauye (aka..Tambwe Hizza) amejibu makombora ya chadema na amesema kwamba Chadema wanatapatapa kwa sababu sasa amepatikana mtu makini wa kujibu hoja zao.

Pia amedai kwamba Chadema walizoea kuionea CCM kwa sababu hakukuwa na mtu makini anayejua kujibu hoja.Ameapa ataendelea kuianika Chadema mpaka pale watanzania watakapotambua ni nani fisadi kati ya CCM na Chadema.

Pia amedai kwamba mshahara wa katibu mkuu wa CCM Wilson Mukama hauzidi milioni 3 kwa sababu CCM haina mafisadi kama chadema.Amesema pia kwamba hakuwahi kuomba kujiunga chadema eti kwa sababu yeye si mchaga.

Kuna vyombo vingine vya habari Nape amedai leo atazidi kuilipua na kuimaliza kabisa Chadema.
 
Msameheni bure huyo hiyo NAPE yote ni njaa najaribu kutetea ugali wake ili JK asimtimue amuone kuwa anafaa ingawa moyoni kwake Nape anajua fika kuwa CHADEMA ndio msema kweli na kiboko ya CCM.

Hilo halina ubishi kwa watanzania wote walio na uchungu na nchi yao ila kwa wale wachahe wasio na machungu kwa nchi yao wataona kama Nape anaongea kitu cha maana sana na walio mafisadi ni CDM badala ya CCM.
 
Mbona ameshindwa kuwavua magamba mafisadi, magamba yamekuwa magumu nini, au ile ilikuwa ni nguvu ya soda!
 
Nape ataivuraga CCM yenyewe pamoja na vyama vyote vya upinzania Tanzania. Ingawaje ana mdomo lakini kichwa na nidhamu hana. Nape ni hatari kwa usalama wa Taifa na Amani ya Taifa.

Inawezekana hajaelimika vya kutosha, kwanza mara nyingi sana maneno, msimamo, na taarifa zake zinatofautina na Katibu Mkuu wake, bwana Mukama. Huu Kijana hana uzoefu wa kazi za siasa. ataendelea kuiua CCM. Nape ni Gamba juu ya Gamba
 
Wadau katika gazeti la mtanzania Nape Nauye (aka..Tambwe Hizza) amejibu makombora ya chadema na amesema kwamba Chadema wanatapatapa kwa sababu sasa amepatikana mtu makini wa kujibu hoja zao.Pia amedai kwamba Chadema walizoea kuionea CCM kwa sababu hakukuwa na mtu makini anayejua kujibu hoja.Ameapa ataendelea kuianika Chadema mpaka pale watanzania watakapotambua ni nani fisadi kati ya CCM na Chadema.
Pia amedai kwamba mshahara wa katibu mkuu wa CCM Wilson Mukama hauzidi milioni 3 kwa sababu CCM haina mafisadi kama chadema.Amesema pia kwamba hakuwahi kuomba kujiunga chadema eti kwa sababu yeye si mchaga.
Kuna vyombo vingine vya habari Nape amedai leo atazidi kuilipua na kuimaliza kabisa Chadema.............
dogo credibilit y yake inashuka kwa speed ya ajabu, point na hoja zimemuishia anaanza kubwabwaja
 
Nape, ondoa kwanza Boriti kwenye jicho lako, baada ya hapo geukia jicho la mwenzako.
 
Nape ondoa mafisadi CCM siyo uje na hoja za kijinga hapa mwananchi gani anayekubaliana na CCM kwa sasa mbona mambo yako wazi na hilo unaliona ndugu yangu mmetupiga changa la macho hapa kuwa mnasafisha chama, matokeo yake mmeishia njiani na kwanza ndo mmewarudisha kwenye nyadhifa zao.

Dogo nenda pole pole utashindwa na mengi sana
 
Maneno kama "Chadema walizoea kuionea CCM kwa sababu hakukuwa na mtu makini anayejua kujibu hoja" sizani kama yamelenga kubomoa CHADEMA bali kuzidisha uhasama ndani ya CCM.
Nape anataka tujue kwamba kabla yake wengine wote hawakuwa makini akiwemo MWENYEKITI.
 
Nape ni mpambanaji haswa, CDM mlizoea kumnyanyasa wagosi wa kaya "Makamba na Tambwe hiza" hizi ni zama za kujibu mapigo.

Mapigo ya Nape ni makali kiasi ambacho CDM wameona majibu kutoa Slaa na Mbowe hayatoshi.

Hivyo Komu, Marandu na safari nao wakaingia uwanjani kumjibu Nape. CCM tupo mkao wa kula, upele umepata mkunaji, dawa ya makombora ya CDM imepatikana!!
 
Jamani naomba mwenye kujua kiwango cha elimu ya nape atuwekee humu jamvini maana sidhani kama mtu mwenye at least form four pass anaweza akaongea ujinga kama huo professor safari muongeze kwenye orodha ya mafisadi wa elimu tanzania
 
Tatizo Nape anadhani propaganda ni lazima uongee hata kama ni pumba. Afu anaposema kabla yeye hajawa tambwe hiza wa ccm amna mtu ambaye alikuwa anajua kukitetea na kukisemea chama ana maana gani kwa watangulizi wake. Acha tusubiri siku 90 tuone kama wataoga kichwani.
 
Back
Top Bottom