Napata tabu mwenzenu jaman anaeyejua suluhu ya tatizo hili anisaidie wana JF

1. Andaa maji ya kuoga safi na yawe vuguvugu, kamulia limao mbili usisahau kuondoa vimbegu vya limao katika maji. Tumia mchamnganyiko huo kuoshea sehemu zako za siri kila baada ya kujisaidia.
2. Katika vyoo vya public epuka sana kutumia maji yale unayokuta kule chooni sababu wengine sio wasafi kabisa hurudishia uchafu wao mlemle kwenye ndoo.
3. Epuka kushare makopo ya chooni.
4. Hakikisha choo unachotumia ni kisafi muda wote, muda mwingine infection huwa tunapata sababu yya uchafu wetu wenyewe.
5. Nenda hospitalini huo ugonjwa unatibika.
 
Ngoja nikaperuzi nitakupa jibu la uhakika kesho na utapona.
 
...i wish ningekuwa dr!jaribu kubadili pedi,chemsha sana maji unayooshea huko chini labda itasaidia,kama dawa na patner pia atumia ila mwende kwa wataalam wa akinamama!pole sana,mungu atakujalia
 
Elli unajua nnajitahidi sana kuzingatia kanuni za usafi muda wote gemmy wangu hana msitu na natumia tissue nikiwa nyumbani ni kujisafisha na maji na kuputa na taulo safi nguo zangu za ndani ni kila baada ya miezi 4 na badilisha mambo tu yameniangukia ila ntazingatia ushauri wenu thanx for your concern
Usingojee miezi minne nguo za ndani zote ulizotumia kabla ya matumizi ya dawa zitupe na uanze na mpya(pamba halisi),na hata hizo mpya usivae kabla ya kuziosha.
 
dr alikuambia sababu ya hayo majimaji ya ukeni kupungua? maybe unahitaji kumuona tena,ungerudi kwake.
kunaweza kuwepo sababu kadhaa za hali hii
1 aina ya chupi unazovaa. zinapaswa kuwa za cotton ili upate hewa ya kutosha.ni ngumu kiasi kupata pure cotton ila huna jinsi
2 hakikisha unaanika chupi zako kwenye jua. mambo ya kuanika chini ya godoro ama bafuni,kunakua na unyevu unaosababisha kuzaliana kwa bacteria. walau mara moja kwa wiki unaweza kuloweka chupi zako kwenye maji ya uvuguvugu yenye jik (1:20 v/v)
3 hygiene issues: nawa mikono kabla na baada ya kujisaidia (kuna hand sanitizer siku hizi,zinauzwa kwenye kichupa kidogo kwenye phamacy). baada ya haja kubwa tumia toilet paper kabla ya maji. jifute kuanzia mbele kuelekea nyuma. kila wakati unapotumia choo jifute ukeni kuanzia mbele kuelekea nyuma, then jifute nyuma kwa style hiyo hiyo ya kuanzia mbele kuelekea nyuma. sikushauri sana kutumia maji unless unakua na kitambaa cha kujifuta kila mara unapomaliza haja (usirudie kitambaa!!!). oriflame wana wet tissue zinaitwa femme,unaweza kuzitumia baada ya kutumia toilet papes.
4 epuka kutumia antibiotic ama madawa makali,huchangia kuua wadudu rafiki wa ukeni. usitumie pia sabuni zenye harufu kali. kuna sabuni maalum ambayo ni soap free ya kunawia ukeni, mary rose wanayo kama upo dsm.
5 usifanye douching (kujiswafi uke kwa kuingiza kidole). google uone jinsi ambavyo unajihatarisha kwa kuingiza uchafu na kusababisha vidonda. uke una mechanism yake ya kujiswafi wenyewe. na kama una hiyo obssession kuna kifaa maalum cha kufanyia douching
wakati unajaribu kuzingatia haya kwa ajili ya kubadili life style, inabidi uende hospitali,onana na daktari wa wanawake ikibidi.utapata ushauri wa kutibu na kuepuka maambukizi mapya.
 
Ninakama miezi miwili nnatatizo la kuwashwa mbele na nyuma nawashwa sana nikajua ni fungus nimetibu sana lakin sikupona nikafanya vipimo vya cultural sensitivity dokta akanambia maji maji ambayo yanakua uken yamepungua hivyo wale bacteria rafik wameanza kunishambulia nimetumia dawa zimeisha nimekaa kama wik moja tatizo limeanza tena plz nisaidieni wana jf

Pole sana Gemmy kwa ugonjwa, samahani sana kwa kuchelewa kujibu kwani sikuwa nimeingia jamvini kwa siku kadhaa...kwa dalili unazosema (kuwashwa na kutoka majimaji), na pia culture & sensitivity imetoa majibu yanayosupport bacterial infection, na pia kwa sababu daktari amekuexamine akaona kuna uwezekano balance ya vaginal pH imevurugika...kuna uwezekano mkubwa umepata maambukizi ya both bacteria na fungus. Hii inawezekana kwani hawa wote ni wakazi wasio na madhara ukeni (normal flora), ila wanakuwa na madhara pale tu vaginal pH inapobadilika nawao kuzaliana kwa wingi, na pia vaginal pH inapobadilika bacteria wengine wanaweza vamia ukeni na kusababisha matatizo.

Tricky part kutibu tatizo lako kwanza ni kurestore hiyo vagina pH, na pili kuclear hiyo infection. Natumai daktari wako alikupa antibacterial na antifungal drugs (kwa miezi miwili ni lazima atakuwa ameshakupa) ziwe za vidonge au za kuweka ukeni locally (pessaries/cream). Lakini cha muhimu zaidi hygiene ya huko ukeni bila kuharibu further vaginal pH. King'asti naona amekushauri kwa kirefu sana kuanzia usafi wa underpants mpaka usafi wa uke na kuavoid douching. Sina cha kuongezea.
 
Back
Top Bottom