NAONA MSO YAONA

Dotto C. Rangimoto

JF-Expert Member
Nov 22, 2012
1,985
1,282
yenyewee.png



.........NAONA MSO YAONA...........

Mmenitia upofu, ambao wanishangaza,
Sizioni tena hofu, ambazo zilitatiza,
Sioni pia machafu, moyo yalouchukiza.
Penye kiza kuna kitu, nakiona kina ishi.

Ingawa nina upofu, nuru sijaipoteza,
Ninachoona turufu, zitele katika meza,
Mwepesi kuona rafu, kama mpira twacheza,
Penye kiza kuna kitu, hiki kitu cha aushi.

Mlonitia upofu, sikiza nawaeleza,
Naona watu kwa safu, nadhifu wamependeza,
Wameshika misahafu, inayo toa mwangaza,
Penye kiza kuna kitu, kinanifanya niishi.

Tangu niwe na upofu, naona mso yaona,
Simba aketi na pofu, salamu wakipeana,
Tembo mbele ya siafu, akimbia hila hana,
Penye kiza kuna kitu, chanifanya nende joshi.

Radhi nife na upofu, nimuone ibilisi,
Nionao upotofu, mfichao kwenye rasi,
Pamba zinakuwa sufu, hariri naona lasi,
Penye kiza kuna kitu, msikatae bilashi.

Dotto Rangimoto Chamchua(Njano5)
Call/whatspp 0622845394 Morogoro.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom