Naona aibu jamani, nisaidieni

nyengo
ni kitu cha kawaida wala usiogope
mi mwanangu ni wa kike na ana umri kama wa mwanao nae huwa akifanya hivyo mara chache
ila yeye anashinda na chupi no nepi no pampers mpaka usiku
nilijaribu kuuliza wataalamu wakanambia si jambo baya ni kawaida kwa watoto wa umri huo
pia development stages za watoto hutofautiana,sio lazima wote wapitie stage moja.
hata mama mkwe nae huenda alipitia kwa wanae, so hakuna haja ya kuona haya.
 
Boys will always be boys...I don't see any problem in his behaviour.
 
nyengo usione aibu! hiyo ni kawaida sana Mwanasaikolojia SIGMUND FREUD kaeleza mengi sana ebu ingia mtandaoni ( sigmund Freud psychosexual stages) utacheki ni hatua mojawapo tu ktk ukuaji, ya kwanza inaitwa ORAL stage yaani wewe mpatie mtoto chini ya mwaka 1 utakuta kila kitu akikishika anaweka MDOMONI ..........na kuna stage akifika kama wa kiume anamtamani mama yake mzazi na wa kike anamtamani babayake kimapenzi!
Du kama ni hivyo mtoto anaweza kuwatamani hata wazazi wake mimi nashauri ahamishwe kitandani mara moja kanaweza vunja ndoa hako katoto, au kafungie kwenye kitanda chake pekee cha grill hata za mbao. Mimi na wife huwa tunalala watupu kabisa
du tatizo
 
nivizuri mtoto anaonyesha njia nzuri , kwani huyo mkwe aelewi hiyo kitu inakuaje? ok ila usimuache na nepi mda mrefu
 
yaaani we unakaonea aibu katoto ka mwaka mmoja tena mbele ya mamamkwe je ingekua mbele ya babamkwe fataki...ukimcheki kwa jicho la aibu unamkuta naye anatingisha miguu huku anatabasam...
 
Duh! Muwe mnamkataza kwa kutishia kumchapa.
Au anaonaga wewe unashka shka zako.
Mkataze kabla hajazoea hako katabia.
 
Ni mtoto tu
hajui lolote bado..
Mwache afurahie maisha ya utoto
isimkatishe..
mama mk we anaelewa hilo kama alibaatika
kuwa na mtoto wa kiume
 
Mara nyengine tunaona aibu kwa mabo yasiyohitaji kuonewa aibu. Hivi ulikuwa huoni aibu ulipokuwa mjamzito? Unafikiria hao wakwe zako na wazazi wako ulikuwa unawapa picha gani kujitokeza mbele yao na kitumbo? Mwache mtoto ajitambue!
 
Duh! Muwe mnamkataza kwa kutishia kumchapa.
Au anaonaga wewe unashka shka zako.
Mkataze kabla hajazoea hako katabia.

Hiyo siyo tabia mbaya,,, anajitambua..
akikuwa ataacha,, kwani wewe ulikuwa hujichokonoi?
hatafu hakuna cha ajabu hapo, wazazi wanaelewa.
 
Qg yupo sahihi jamani ila labda hamjamuelewa alichokisema hapo sio kuwa anamtamani mzazi wake kimapenzi ila anapokuwa na mama yake kama ni wa kiume anakuwa na hisia za kimapenzi, kwa kuthibitisha hili angalia mtoto wakiume akiwa ananyonya kwa mama yake wapo wengine huwa wanajishika nyeti zao wakati wa kunyonya, chunguza hili utaamini anachosema huyu qg, nawasilisha

nyengo usione aibu! hiyo ni kawaida sana Mwanasaikolojia SIGMUND FREUD kaeleza mengi sana ebu ingia mtandaoni ( sigmund Freud psychosexual stages) utacheki ni hatua mojawapo tu ktk ukuaji, ya kwanza inaitwa ORAL stage yaani wewe mpatie mtoto chini ya mwaka 1 utakuta kila kitu akikishika anaweka MDOMONI ..........na kuna stage akifika kama wa kiume anamtamani mama yake mzazi na wa kike anamtamani babayake kimapenzi!
 
Ndugu yangu Nyengo wala hata usione aibu katika stage za ukuaji wa mtoto hiyo hali ni kawaida sana, hii unaweza kuthibitisha pale unapomnyonyesha muangalie kwa makini sana utakuta anashika pia nyeti zake, wataalaam wanasema kuwa mtoto wa umri huo akiwa ananyonya kutoka kwa mama yake huwa anakuwa na hisia za kimapenzi bt hali hiyo automatically huja kupotea yenyewe na mtoto kutotambua aliyokuwa anayafanya hapo nyuma.

Tuna watoto wawili ktk famlia yetu, binti na wa mwisho ni mvulana. Mvulana ana mwaka mmoja na miezi sita. Sasa kinachonitia aibu ni kwamba huyu mtoto wa kiume tunapombadili nepi hua anashika nyeti zake na kuanza kucheka cheka kitu mbacho huwa naona aibu mbele ya mama mkwe ambae amekuja kututembela hivi karibuni.
Sijui ni kwa nini anafanya hiyvo na mnanis
hauri nifanyeje wanajamii
 
Du kama ni hivyo mtoto anaweza kuwatamani hata wazazi wake mimi nashauri ahamishwe kitandani mara moja kanaweza vunja ndoa hako katoto, au kafungie kwenye kitanda chake pekee cha grill hata za mbao. Mimi na wife huwa tunalala watupu kabisa
du tatizo
Ama kweli ukwaju ni mchachu! Nimecheka kweli, eti mtoto atavunja ndoa du!
 
tuna watoto wawili ktk famlia yetu, binti na wa mwisho ni mvulana. Mvulana ana mwaka mmoja na miezi sita. Sasa kinachonitia aibu ni kwamba huyu mtoto wa kiume tunapombadili nepi hua anashika nyeti zake na kuanza kucheka cheka kitu mbacho huwa naona aibu mbele ya mama mkwe ambae amekuja kututembela hivi karibuni.
sijui ni kwa nini anafanya hiyvo na mnanishauri nifanyeje wanajamii
pole ila cha msingi kama unaona aibu na mama mkwe yupo kamfungie nepi mwanao chumbani.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom