BelindaJacob
Platinum Member
- Nov 24, 2008
- 6,474
- 4,022
Wanajamii,
nakushukuruni sana kwa maoni yenu kwani kuna baadhi yamenifungua macho sana na baadhi yamenichanganya kabisa. Ukweli ni kwamba mimi malengo yangu ni kujiendeleza kitaaluma kwasasa. Mwenzangu yeye anasema anataka kuolewa MWAKA HUU HUU lakini pia yeye kitaaluma yeye amefanikiwa sana. Yeye anasema pia kwamba muda wake mwingi ulikua shuleni lakini pia nikijumuisha maelezo yake anasema kwamba alikua na mahusiano lakini hayakuwa na mafanikio. Aidha, kwa upande mwingine ni kwamba huyu dada ni mambo safi pia. Kiniacho nipa wasiwasi ni kwamba anasema yeye anataka kuolewa na anataka iwe mwaka huu huu, ukweli ni kwamba mimi mwaka huu siwezi kumuoa. Hata hivyo moyo naona umemuangukia kweli lakini kinachonisibu ni hio spidi anayotaka na haraka aliyonayo, inanifanya niogope kweli kweli.
Licha ya hayo suala linalokuja kichwani je ni sawa kuoa mwanamke mwenye miaka 30? Lakini pia huyu dada kwangu ni mkubwa wa umri kidogo kwa miezi kadhaa na usheehe hivi...! Swali ni je ni sawia kujitosa hapa wandugu...?
Ni sawa kuoa mwanamke mwenye miaka 30,au unaogopa kwavile amekupita miaka kidogo?Maana kupishana miezi kadhaa huwezi kusema mkubwa kwako,ni age mate!
Sasa wewe ndo unamfahamu na kumjua vizuri huyo binti,fuata moyo wako unavyokushauri. Na hivi umesema moyo wako umemwangukia pia,mweleze dhamira yako ya kujiendeleza kimasomo kwanza halafu muoane kumbuka mkioana au kuanza familia majukumu ni mengi pia na maisha yanabadilika(inategemea unataka ukasome wapi,mtakuwa pamoja au distance kidogo).
Huyo binti anaweza kuwa na wasiwasi maana ukimwambia asubiri, si unajua siku hizi hata uchumba huvunjika. Kifupi yupo tayari kwa ndoa maana kafanikiwa kama elimu anaona ni muda wa kuolewa na kuanza maisha ya ndoa wakati wewe bado unasita!
Muhimu ongea nae na umsikie mwenzio,unapokuwa na kitu moyoni ukamshirikisha anaweza kulipokea tofauti na wewe unavyomfikiria au mkapata wazo mbadala wote wawili. Kumbuka unapotaka kuoa ni uamuzi mkubwa unaufanya katika maisha yaani kuishi na mtu fulani na kuwa kitu kimoja katika hayo maisha. Haihitaji ukurupuke!
Kila la Kheri!..