Naombeni ushauri

TihZ

Senior Member
Jul 31, 2012
158
26
Habari zenu wanaJf naomba ushauri wenu,nimechaguliwa UDSM sasa nafikiria kukaa nyumbani au hostel kipi kitakuwa bora na mimi nyumbani ni Sinza(kwa wanaopafahamu)....naombeni ushauri wenu
 
Kaa hostel kama ukipata nafasi ili iwe rahisi kusoma na wenzio usiku
 
ni vyema kwanza ungepata ushauri kutoka kwa familia yako,hatujui unajiweza kwa ada ya hostel au la,ila kama unajiweza haujiwezi sinza si mbali na chuoni,kwa nini usikae nyumbani
 
ukipangiwa Mabibo itakuwa vizuri ukikaa home b'se no diff.with Sinza.ila hosteli ni bora zaidi kwani hakuna usumbufu,yaani home mara movie,kutumwa dukani n.k.pia kisaikolojia home hakuna anayesoma hivyo hakuna atakaye kufanya ushtuke na kuanza kusoma tofauti na hosteli ambapo ukiwaona wenzako wanaposoma na wewe lazima usome kwani roho itakuwa inakusuta.

Pamoja sana Mkuu tutakuwa wote UD.
 
Mkuu mtoa mada kama unauwezo kaa hostel coz kule utakutana na wenzako na kujifunza mengi na pia changamoto nyingi..kama mdau alivyosema hapo juu utapata changamoto nyingi za kusoma ukiwaona wenzako wanavyosoma..!
 
Ahsanteni sana ndugu ila kwa upande wa familia yangu naona nitawadidimiza kwa gharama ila nataman kutobaki nyumbani ili nijifunze maisha ila kwa upande wa pili naona bora niwe natokea nyumbani....ahsanteni sana
 
Back
Top Bottom