Naombeni ushauri

Usiogope Bro, kama una nia njema zungumza na huyo binti, lakini kama unataka kumchezea tu kwa tamaa zako, yanaweza kukupata matatizo makubwa, kama unampenda kweli mweleze, kama ni tamaa, muache mtoto wa watu.
 
Kwanza huna nia ya dhati na huyo mtoto, unataka uchape usepe, iyo mbaya kwa maisha yako ya kazi yako. Mwache mtoto wa boss endelea na uliye naye. Roger so far over.
 
Kama una nia ya dhati haina shida, lakini ka unataka kuleta zako zipi boss atakukata masikio nakwambia!
 
Kama hiyo interest ni ya kukupenda na unafikiri hicho unachotaka kufanya atakipenda poa, ila kinyume chake atakuharibia kazi Mkuu, achana naye.
 
kwanza unatakiwa ujiandae kuacha kazi kwani kiustaarabu huwezi kuwa chini ya baba / mama mkwe wako kikazi maana kwa vyoyote mtakuwa katika wakati mgumu wote wawili .. pia kumbuka boss wako anaweza akawa anakutumia masuala yake binafsi hivyo ukawa unamwelewa mapungufu yake , hili linaweza kusababisha mkawa hakuna maelewano kati yenu.. hivyo kama kweli unahitaji kuchukua hatua hiyo jiandae kwanza kwa kutafuta kazi sehemu nyingine ndo uanze utaratibu wa uoaji
 
uwe makini kumsoma boss wako km ni mtu wa kuchukizwa na hilo mpotezee, kazi ngumu bana. utapotezwa km Gaucho toka mchezaji bora wa dunia na klab bora ya ulaya hadi kwenda kuchezea kombe la kuku huko kwao Brazil, mapenzi hayaliwi kaka ila km una source zingne za income its ok.
 
siku boss wako akijua anaweza mind kichizi na mwisho wa siku ajira ukapoteza na mtoto ukamkosa siku hizi mapenzi ya kweli oveer sidhani kama huyo mtoto atakung'ang'ania kama tuonavyo kwenye movie za kihindi na tamthilia za kifilipino.

kukosa kazi! Mh, sidhan kama kuna uhusiano kati kazi na mapenzi! Namaanisha bosi atatumia kigezo gan kumfukuza mshkaji? Atamwoa yeye?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom