naombeni ushauri wenu wadau

Life has to go on with him or without him. Na uwe mwangalifu na wanaume wanaopenda ugomvi kwa vitu vidogo vidogo.
 
Kwa baadhi ya jamii kumpa mtoto jina ni suala/tukio kubwa kuliko tunavyoweza kuelezana hapa. Pamoja na hilo, huyo kaka hatumjui, wewe unamjua zaidi yawezekana kuna issue zaidi kati yenu. Jaribu kwa 'nguvu' zote kupata suluhu. WADADA, JARIBUNI SANA KUEPUKA MIMBA ZA KABLA YA NDOA. Japo kuna wale ambao hamtaki kusikia neno kuolewa!!
 
Nilionalo hapo ni kibri cha elimu ulonayo, tabia hiyo ni maarufu kwa wana-wake wenye elimu/kipato kikubwa kuliko mwanaume. Cjui ndo ubeijing?
 
Kama tatizo ni jina tu na wewe bado unamtaka mpe mtoto jina analo/alilotaka yeye!Kama kuna mengine hata ukibadili jina haitasaidia.Inawezekana umempa sababu/kisingizio tu ya kukuacha sasa hivi ila nia alikua nayo kabla!
 
hii kesi ni ya kitoto sana. acheni upumbav haraka sana. badala ya kutafta hela ya kumnunulia mtoto pampers ndio kwanza mnagombana kwa jina. nyambaaaf!. naomba mods waipeleke hii sredi jukwaa la wakubwa ili tusiione kabisa.

BTW: nawewe mleta sredi kwanini kutiana mimba mlishirikiana lakini kutoa jina hamkushirikiana? aaargh! niko na hasira kweli. naomba mdada mmoja anitumie PM ili nipungue mzuka kidogo.
 
mamie maybe hakuwa na nia na wewe, au anasababu ingine lakini sio jina tu liharibu mahusiano had kutotaka kujua mtoto anaendeleaje.
jus move on coz sidhan kama hapo kuna upendo.....!
 
Jamani, mie nikiperuzi na kudadisi, naona kuna kitu imefichika hapa. Mara nyingi watu tunapenda kueleza mabaya tuliyotendewa na vijimakosa vidogovidogo tulivyokosea hadi tukatendewa hayo mabaya. Hakuna aliye tayali kueleza makosa yake mabaya kwa uwazi ili asaiiwe. Mzazi mwenzie angeweza kupatikana huenda angeeleza yaliyojiri kwa uwazi. Huyu bint anatafuta msaada bila kuweka yote peupe, kwa tabia yetu wanaume huwa tukihisi jambo la kukosa uaminifu kwa wapenzi wetu huwa tunavuta subra kupata ukweli. Nionavyo mie, huyu bint alikua na mahusiano na mtu mwingine na jamaa alipata tetesi na inawezekana alipohoji akajibiwa mbaya sasa shule imeisha na huyo aliyemjaza kiburi hayupo na mzazi mwenzie amejiridhisha kwa kuona hata jina hajashirikishwa kutoa. Hapo dada ni DNA tu itakayo mrudisha jamaa vinginevyo sitarajii arudi. Weka yote hapo tukusaidie .
 
My dear,jiandae kwa lolote......sidhani kama jina ndo isssue ya yeye kufanya hayo anayoyafanya.....manake kinachoonekana si tu anakuadhibu wewe kwa kosa tusilolijua bali pia hata mtoto ambaye hana hatia na anastahili mapenzi yote ya baba yake bila kujali mapungufu au tofauti za baba na mama.......nakushauri muombe msamaha na jadili nae kuhusu kubadili jina,ukiona haelekei mwambie awe wazi tu,kama hakutaki tena aseme,napenda kukupa moyo tu,utayaweza yote kwa msaada wa Mungu anayetutia nguvu......jipe moyo mkuu.....mwanao kwanza,mengine yafuate....focus on your baby and do not let anything take that focus!!
hongera kwa mtoto,na Mungu awatunze.....akue aje kuwa kama Obama!!!
 
Ushauri wa kileo ni mwepesi kwa mambo mazito. Mtoto tayari ni historia mpya ya maisha Umegeuza page Dada taka usitake. Kabla ya kufanya chochote juu ya mtoto ushirikiano ni lazma. Wasichana Magraduate hapa ndipo wanapoachwa na wasio magraduate kwenye mambo ya kijamii.Kama jamaa aliilea mimba mpaka ukajifungua kuna swali kwa nini leo ajiweke pembeni? DADA TUPE JIBU. Nahisi ameshasikia story kuwa amebambikiwa ndo maana jina silo lake. Rudi kwa mumeo mlainishe mumlee mtoto ikiwezekana mtaoana tu ma be. NI MUMEO TUUUU HAITAFUTIKA. Halafu madada magraduate chungeni sana majukumu yenu ya kijamii na kinyumba mnayadharau ndo maana mnaongoza kuibiwa waume na mabeki tatu wenu.... NALIANZISHA.
 
hasira zako kali hadi PM yenyewe imeogopa kuja. PM inataka bodigadi eti.
wewe unanibeep sio? soon nitaelekeza mahasira yangu kwako. ok do ze needful haraka kabla sjachafua sredi la watu.
bek to ze topik: refer to my post no 25 for maelezo zaidi
 
hapana, huna haja ya kufeel guilty kisa ulimpa jina mtoto,any responsible father hawezi kununa bila sababu ya msingi kwa sababu anajua in the end anayekuwa victim ni mwanae.............mie nadhani mzazi mwenzio kampata mwingine, hivyo anakuona wewe na mwanao kama mzigo/obstacle kny relationship yake mpya!....cha kufanya jiandae kisaikolojia kulea mtoto mwenyewe!.......ila pia nahisi tutakachofanya hapa JF ni guess work mwenye majibu ni huyo mzazi mwenzio kwa nini usimuulize kwa upole nini future yenu na mtoto wenu?
 
Vijana mnakurupuka kumsema binti wa watu. Mnasahau kuwa hawa vijana hawakuoana. Pia mmoja yuko mikoani na mwingine Dar. Je mnafahamu mazingira ya kujifungulia ya huyu binti? Je mnafahamu mawasiliano yao yalikuwaje baada ya binti kubeba mimba? Msimshobokee binti kuwa na degree. Wapo watu ambao wanaringia degree zao na ni malimbukeni ila mfahamu ni wachache wa aina hiyo. Binti kujifungulia kwa wazazi wake mara zote unakuta ni rahisi sana jina la mtoto kutokea kwa upande wa mama maana kijana hajatoa mahari na wala katika maelezo ya binti haionyeshi waziwazi kama kijana alienda kujitambulisha kwao.
binti tulia na mwanao usimfikirie huyo mwanaume kwa sasa lea mtoto wako. Jina ni sababu tu ndogo anayoitafutia lukuacha na wala hakuwa na mpango na wewe tokea mwanzo. Kama jina limemkwaza basi angekuwa na subira na kusema mtoto ajaye atampa jina yeye maana alikuwa na mpango wa kukuoa au siyo? Pia kuna namna nyingi ya kubadili jina mtoto, je mumefikiria jina la ubatizo?

Hapa sijaona sababu ya watu kumrukia degree ya huyu binti unless otherwise huna wewe ndio maana unaona ndio sababu.
 
Vijana mnakurupuka kumsema binti wa watu. Mnasahau kuwa hawa vijana hawakuoana. Pia mmoja yuko mikoani na mwingine Dar. Je mnafahamu mazingira ya kujifungulia ya huyu binti? Je mnafahamu mawasiliano yao yalikuwaje baada ya binti kubeba mimba? Msimshobokee binti kuwa na degree. Wapo watu ambao wanaringia degree zao na ni malimbukeni ila mfahamu ni wachache wa aina hiyo. Binti kujifungulia kwa wazazi wake mara zote unakuta ni rahisi sana jina la mtoto kutokea kwa upande wa mama maana kijana hajatoa mahari na wala katika maelezo ya binti haionyeshi waziwazi kama kijana alienda kujitambulisha kwao.
binti tulia na mwanao usimfikirie huyo mwanaume kwa sasa lea mtoto wako. Jina ni sababu tu ndogo anayoitafutia lukuacha na wala hakuwa na mpango na wewe tokea mwanzo. Kama jina limemkwaza basi angekuwa na subira na kusema mtoto ajaye atampa jina yeye maana alikuwa na mpango wa kukuoa au siyo? Pia kuna namna nyingi ya kubadili jina mtoto, je mumefikiria jina la ubatizo?

Hapa sijaona sababu ya watu kumrukia degree ya huyu binti unless otherwise huna wewe ndio maana unaona ndio sababu.

huyu mdada na huyo mkaka ni watoto flani tu na nadhani wakipata hizi skendo watagrow up kidogo. tangu nimejiunga JF hii ndio sredi ya kwanza ambayo naiona haijabalehe. huyu mdada wenyewe stori anaibania bania utazani vocha ya sim. haelezi kama alimshirikisha jamaa kwenye kutoa jina? haelezi mazingira yake ya kujifungua? haelezi habari ya mimba jamaa aliipokeaje? acha niishie hapa
 
Pauline;1787411]hapana, huna haja ya kufeel guilty kisa ulimpa jina mtoto,any responsible father hawezi kununa bila sababu ya msingi kwa sababu anajua in the end anayekuwa victim ni mwanae.............mie nadhani mzazi mwenzio kampata mwingine, hivyo anakuona wewe na mwanao kama mzigo/obstacle kny relationship yake mpya!....cha kufanya jiandae kisaikolojia kulea mtoto mwenyewe!.......ila pia nahisi tutakachofanya hapa JF ni guess work mwenye majibu ni huyo mzazi mwenzio kwa nini usimuulize kwa upole nini future yenu na mtoto wenu?[/QUOTE]

Hivi dada Pauline kwako unaona ni sawa mama kumpa jina mwanae bila kumshirikisha mmewe na hasa mtoto wa Kwanza? Isitoshe sidhani kama ni jina tu ndo imekuwa issue kwa mme kumsusia huyu dada. Yawezekana kweli kama walivyosema wachangiaji hapo juu kuna jingine hapa limejificha. Katika hari ya kawaida kama walikuwa kwenye maelewano mazuri kipindi cha mimba hasingeweza kumpa mtoto jina bila kumshirikisha baba mtoto. Nikisoma ndani ya mistari naona huyu dada ana ugraduate kichwani wa kuona anaweza kufanya maamzi yoyote juu ya mtoto bila kumshirikisha baba ikiwemo kumtunza mtoto. Yawezekana pia kwa vile hawajaowana wazazi wa binti walishinikiza kumpa mtoto jina kutokana na maelewano yaliyokuwepo kati ya binti yao na baba wa mtoto. Inakuwa vigumu kujuwa ni nini kilijili hapo kwa vile hatujasikia kutoka kwa baba wa mtoto na hivyo tunabakia na labda...... labda vile... yote hiyo tujaribu kuangalia possible causes tha situation waliyomo kwa sasa.

Wakae chini watatue matatizo yao, mtoto siyo matumizi tu yanahitajika bali malezi yanayojumuisha baba na mama. Kuna raha jamani kwa mtoto kukuwa akiwaona baba na mama wapo pamoja wanapendana. Ni vema pia watoto wakazaliwa kwa baba mmoja na mama mmoja. Ni matatizo tu yanasababisha watoto kuwa na baba tofauti nadhani nao wao wangependa mama yao na baba yao awe ni mmoja.
 
jaribu kumuuliza angependa mtoto aitwe nani uone atasemaje.
ila ulitakiwa kumsikiliza tangu mwanzo
 
My dear, mwanaume akikuchoka anatafuta kila sababu ya kutokea. Kama nimekuelewa umeandika kuwa jina mlikubaliana kabla, ila baadae ndio amekuja geuka. Huyo amepata mwingine huko aliko ndio katafuta sababu ya kukuacha,,, Mpigie simu jaribu kuongea nae kuwa angependa mtoto aitwe nani, ukona hana mweleko achana nae, mtegemee Mungu, lea mtoto wako. Mwanaume ndio walivyo mdogo wangu
 
hellow everybody! Jamani hii ni mara yangu ya kwanza kuwa humu, so naombeni mnipokee,! Mimi ni msichana wa miaka 25,nimemaliza chuo kikuu mwaka jana. Tatizo nililonalo ni kwamba,nilipata boyfriend,ambaye tulipendana sana kufikia hatua ya mimi kubeba ujauzito nashkuru mungu nimejifungua salama mwez wa2, issue kubwa ni kwamba,jamaa kanisusia mtoto kisa,hajapenda jina nililompa mtoto! And so far, hatujaoana! Ila tulikua na plans hizo. Mimi nipo kwe2 dar na yeye anaishi nje ya mkoa akiendelea na mambo yake. Bynow,hatak mawasiliano yoyote na mimi,haulizi hata mtoto wake anaendeleaje! Amekua akintolea maneno ya kashfa and all that stuffs!jamani,au mimi ndiye mkosaji? And its nt that i ddnt tel him b4,nilimwambia! Lkn ni kigeugeu sana! Jamani nifanyeje?should i leave hm alone and live my own life?trully ameniharibu psychologically! Sidhani kama ntakuja kupenda tena maishani! Plz help me...

pole kwa yaliyokukuta ndugu yangu bt hapo kwenye red umeniacha njia panda
 
Back
Top Bottom