Naombeni ushauri jamani ktk hili

JATELO1

JF-Expert Member
Oct 31, 2011
1,230
301
Wanajamii,
mimi nina mdogo wangu wa kiume na kwasasa ana miaka 27. Huyu mdogo wangu alifanya CSEE mwaka 2010 na kupata division IV. Akarudia mwaka 2011 kama Private Candidate na kupata alama zifuatazo;
History C
Geogr D
Kiswah D
English D
Civics D
Liter Eng. F
Mathem. F

Jumla anakuwa na Division 4 ya Point 29.

Kumbuka kwamba kabla ya kjiunga QT alisomea Udereva na Machenical kwa mwaka 1 pale FUTURE WOLRD DRIVING COLLEGE pale Buguruni na kupata Driving Licence na Umakenika Grade B baada ya kufanya mtihani wa Veta. Sasa alipomaliza Hapo ndiyo akaamua kujiunga na QT Programme na hatimaye kupata hayo matokeo. Huyu dogo alikuwa akisoma ili aweze kujiunga Ualimu Grade A, lkn sasa imeshindikana kwani Ualimu Grade A nasikia wanatakiwa wenye Division 4 ya Point 28 mwisho. Sasa nimeongea na dogo na inaelekea amekata tamaa, kwani alitamani sana kwenda Ualimu, ukizingatia miaka nayo inazidi kusogea.

Sasa ndugu zangu naomba ushauri wenu namna ya kumsaidia huyu mdogo wangu. Je kwa matokeo hayo anaweza akafanya nini? na je nimshauri afanye nini jamani?

Natanguliza shukrani.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom