Naombeni ufafanuzi wa kisheria

Democrasia

Member
Feb 1, 2008
79
3
Jamani naombeni kupata ufafanuzi kuhusu sheria za usalama barabarani, JE TRAFIKI ASIPOWEKA PLATE NAMBA KWA GARI YAKE NI HALALIHii naiona sana hapa Arusha kwa Police traffic mmoja anayeitwa Hemedi mwenye gari Aina ya Cortina lisilo na plate namba,Jana nilishuhudia polisi trafiki wakiwa wanakamata magari eneo la Tengeru na alipopita hemedi bila namba yeye aliruhusiwa kupita bila hata ya kusalimia, Je jamani ni sahihi? Naombeni ufafanuzi wa kisheria hapo, kama wao wako wako tofauti na wengine
 
Hakuna aliye juu ya sheria.Hemed ni mhalifu wa sheria za usalama wa barabarani tu kama mtuhumiwa mwingine yeyote yule.Uzoefu wake wa kazi au kuwa katika kitengo hicho hakumwekei kinga ya kisheria hata kidogo.Yeye anajaribu kutumia usemi wa kiswahili usemao "Mbuzi hula kwa urefu wa kamba yake"Hiyo siyo sheria.
 
Hakuna utawala wa sheria hapo. Mwenzao anavunja sheria lakini hakuna wa kumnyoshea kidole kwani 'zimwi likujualo halikuli likakwish"
 
Anavunja sheria! Whats the big deal? You sound like kwamba ni kitu kigeni sana kwako. Lakini kama wewe ni mtanzania unayeishi Tanzania hali hii ni ya kawaida kila mahali. Kuna kitu tunaita kubebana. Its our culture. Tukiwa tunafanya kazi idara moja, lazima tulindane.
 
Wajameni mnavyosema hivyo ni sawa kunakulindana, swali linakuja hivi nani awajibishwe?
 
Wajameni mnavyosema hivyo ni sawa kunakulindana, swali linakuja hivi nani awajibishwe?

Wote wanaohusika na wewe pia. Umechukua hatua za kumpigia simu mkuu wake wa kazi au hata RPC au IGP? Kama bado basi na wewe au yeyote yule ambaye ameshuhudia tukio hilo anahusika!
 
Zipo taratibu za kiusalama ambazo zinaweza kusababisha gari kuendeshwa bila ya plate number na kwa vile wenyewe wanalielewa na wanamuelewa muendeshaji sio kosa kabisa ni taratibu zipo ndani ya uwezo wao,sasa mbona wewe wanakukamata au mbona wengine wanawakamata.
Kwa kweli si polisi wote wanaendesha gari bila ya plate number wako polisi maalumu tu ambao wamepewa uwezo wa kufanya shughuli zao wakiwa na magari yasio na plate number ila unachotakiwa ni kutoiga tembo.
 
kweli kwa jinsi wanavyo tunyanyasa ningepata namba ya cm ya mh James Kombe au e mail yake ningemweleza yote haya, mwenye nayo jamani naiomba
 
Anavunja sheria! Whats the big deal? You sound like kwamba ni kitu kigeni sana kwako. Lakini kama wewe ni mtanzania unayeishi Tanzania hali hii ni ya kawaida kila mahali. Kuna kitu tunaita kubebana. Its our culture. Tukiwa tunafanya kazi idara moja, lazima tulindane.

Na huku kulindana ndiko kumetufikisha hapa tulipo! Tunaacha kuwajibishana tunakuta tumefika pabaya. Je askari wote wenye magari wakiamua kutembea bila plate number itakuwaje? Anatakiwa kuchukuliwa hatua za kisheria haraka sana!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Zipo taratibu za kiusalama ambazo zinaweza kusababisha gari kuendeshwa bila ya plate number na kwa vile wenyewe wanalielewa na wanamuelewa muendeshaji sio kosa kabisa ni taratibu zipo ndani ya uwezo wao,sasa mbona wewe wanakukamata au mbona wengine wanawakamata.
Kwa kweli si polisi wote wanaendesha gari bila ya plate number wako polisi maalumu tu ambao wamepewa uwezo wa kufanya shughuli zao wakiwa na magari yasio na plate number ila unachotakiwa ni kutoiga tembo.

Sikubaliani na hili. Hata kama ni kwa sababu za kiusalama unakuwa na namba bandia. Sijawahi kuona mahali popote gari ikiendeshwa bila plate number ila ninajua kuwa kunakuwa na namba bandia walizopewa na huzibandika kwenye magari yao. Ni uvunjaji wa sheria
 
nchi kibao utakuta watu wanaendesha bila ya numbaer plate ila wewe sasa unataka kuvaa jezi ya ubishi.
Mimi najua sababu ya baadhi ya gari kuwepo au kuendeshwa bila ya numberplate ,namba ya bandia ndio kuvunja sheria kwa maana unadanganya ,ndio maana yake.
 
Lengo la plate number ni moja tuu, utambulisho wa hilo gari wakati wa usajili. Kuwepo kwa kibao cha plate number au kutokuwepo kunaweza kutokana na sababu yoyote kati ya hizi.
1. Huyo ni Mh. Fulani hivyo gari yake inatumia cheo chake ama alama ya wadhifa wake kama ngao, CJ, CS, CAG, IGP, State Car or Just Married.
1. Gari haijasajiliwa humu nchini, ilikuwa imekufa kabla ya zoezi la number mpya, sasa imefufuliwa hakuna any documentation na anasubiri kufanya process.
3. Vibao vimeanguka na mmiliki ama kwa uzembe ama kwa kutingwa, hajaandika vibao vipya.
4. Gari maalum ya shughuli maalum katika eneo maalum linaloeleweka na wahusika. Na hapa ndipo pia hutumika namba bandia makusudically.
Nb demokrasia kama una biffu na huyo afande, hauwezi kuimaliza kwa issue ya plate number, ama inakuuma kwa nini ford cortina yake ya mwaka 47, haina usajili?. Kuna issue kubao muhimu zinazowahusu trafic wa A-Town, wewe umeona tuu hii ya plate number?.
 
kweli kwa jinsi wanavyo tunyanyasa ningepata namba ya cm ya mh James Kombe au e mail yake ningemweleza yote haya, mwenye nayo jamani naiomba

Kwa hiyo ungekuwa hunyanyaswi ila unapeteshwa peteshwa na hawa rogue law enforcers usingejali, usingetaka kuripoti kwa RPC Kombe. Nilifikiri hupendi uvunjaji sheria na ufisadi wa law enforcer yeyote.

Na wewe ni hao hao!
 
kweli kwa jinsi wanavyo tunyanyasa ningepata namba ya cm ya mh James Kombe au e mail yake ningemweleza yote haya, mwenye nayo jamani naiomba

IGP-0754 785557, Manumba-0754 206326, Kombe-0754 304514, Chagonja-0754 489567, Tossi 0754 016150. Kazi kwako Mkuu
 
Kutokuwa na plate number ni kosa, hata polisi wanaofanya kazi maalum wanpewa plate number tofauti na za kawaida, sio kuruhusiwa kuendesha pasipo plate number. Huo ni uozo na kulindana.
 
Na huku kulindana ndiko kumetufikisha hapa tulipo! Tunaacha kuwajibishana tunakuta tumefika pabaya. Je askari wote wenye magari wakiamua kutembea bila plate number itakuwaje? Anatakiwa kuchukuliwa hatua za kisheria haraka sana!!!!!!!!!!!!!!!!

Kuna post imeweka number za Kombe hapo. Huyo ndio kiongozi wao. You better call him right now.
 
Back
Top Bottom