Habari zetu wana JF;
Naombeni msaada wenu katika suala zima la sheria za jinai.
Ninasikia kwamba sheria huwa zinabadilishwa kutokana na sababu moja ama nyingine. Kwamba kitendo fulani huenda kilikuwa kosa la kisheria kipindi flani, na hukumu yake ilikuwa hivi ama vile. Baada ya mabadiliko ya sheria kutokana na sababu kadha wa kadha, kitendo hicho endapo kitatendwa hakitakuwa kosa tena ama basi kitaendelea kuwa kosa, LAKINI hukumu yake itakuwa hivi ama vile (tofauti na ilivyokuwa mwanzo).
Swali langu; MFANO:
Kwa kipindi flani labda kosa la wizi (wa kawaida) kwa sheria za jinai za kipindi flani hukumu yake ilikuwa Miaka mitano gerezani. Wakati huo, A alitenda kosa la wizi na akahukumiwa kwenda gerezani kutumikia kifungo cha Miaka mitano. A, akiwa gerezani na amekwishatumikia miaka mitatu tayari, hukumu ya sheria hiyo ya wizi ikabadilika, kwamba endapo mtu atapatikana na hatia, hukumu yake itakuwa kifungo cha miaka miwili gerezani.
Swali; Je A ambaye alihukumiwa kwenda jela miaka mitano kipindi hicho, na tayari amekwisha tumikia miaka mitatu gerezani, atakuwa affected kwa namna yoyote na sheria mpya au vile alihukumiwa kabla ya mabadiliko ya sheria itabidi atumikie kifungo chake cha miaka mitano?
Kama jibu ni NDIO kwa swali la kwanza, kwamba atumikie vile alihukumiwa kabla ya badiliko la sheria. Vipi kuhusu kosa la Mauaji ya kukusudia, ambapo B (muuaji) alihukumiwa kifungo cha Kunyongwa mpaka kufa kwa kosa la Mauaji ya kukusudia. Then B akiwa kifungoni kusubiri kunyongwa mpaka kufa, sheria ya Haki za binadamu ikaingilia kati kwamba 'Kila mwanadamu ana haki ya kuishi, na kwamba sheria ya kunyonga mpaka kufa ni batili', kwa pressure kutoka haki za binadamu, Sheria ya kunyongwa mpaka kufa ikafutwa/badilishwa kuwa kifungo cha maisha ama vinginevyo.
Swali; Je, B kama alivyokuwa A kwenye kesi ya wizi hapo juu, ataangukia kwenye sheria mpya au vile alishahukumiwa kunyongwa mpaka kufa kabla ya sheria kufutwa/badilishwa, itabadi akamilishe kifungo chake (anyongwe mpaka kufa)?
Nawashukuru kwa muda wenu, naombeni ufafanuzi tafadhali.
LizY.