Naombeni Msaada wenu!!!!

KakaKiiza

JF-Expert Member
Feb 16, 2010
11,578
8,600
Ninaombeni msaada wenu wana jf hususani Jukwaa la JF Doctor,Mimi nina mgonjwa ana limonia kali nimempeleka TMJ akapewa Rocephin certriaxone,na benzylpenicillin amemaliza dose lakini bado maumivu makali anayasikia na zaidi alikunywa mafuta ya taa bila kufahamu!!akidhani nimaji ya kilimanjaro kwakuwa yaliwekwa kwenye chupa tumepiga xray ilionyesha pafu kwa chini kidogo kolaps!!
 
Mafuta ya taa alikunywa kabla ya Pneumonia/wakati wa matibabu/baada ya matibabu?

Anyway, ukinywa mafuta ya taa yakaingia tumboni, madhara yake yanaweza yasiwe makubwa kama hayo mafuta yakiingia kwenye mapafu (kupaliwa). Mafuta ya taa yana sababisha muwasho (irritation) na hata mchubuko (corrosion), kisha 'inflammation' (sijui kwa kiswahili inaitwaje) ya njia ya hewa na kusababisha kitu kinachoitwa 'chemical pneumonitis', yaani mfano wa Nimonia inayosababishwa na kemikali. Inflammation ya njia ya hewa inaongeza uwezekano wa bacteria kushambulia njia ya hewa na kusababisha Nimonia kali.

Nimeona mgonjwa wako alipewa Rocephin (ceftriaxone) na Benzylpenicillin..hiyo combination ni ya antibitics zenye wigo mpana sana wa kuua bacteria (ni sawa na kuua inzi kwa bomu la mkono) hivyo nategemea zitakuwa zimemsaidia kuua bacteria wote waliosababisha hiyo Nimonia. Pia mafuta ya taa (paraffin) ni rahisi kuwa mvuke (volatile) na hivyo kuitoa kwa njia ya hewa, hivyo sitegemei kama bado ana mafuta ya taa kwenye njia ya hewa. Lung collapse itapona kadri anavyoendelea kupumua basi atakuwa analipanua pafu lililo'collapse' taratibu mpaka lirudi kwenye hali yake ya kawaida.

Maumivu hukusema ni ya wapi...kama ni ya kifua basi ni kwa sababu ya hiyo inflammation ya njia ya hewa, kadri inavyopona na kurudi katika hali yake ya kawaida na maumivu yatakuwa yanapungua. Anaweza kutumia dawa za kupunguza maumivu, Ila yakizidi arudi kwa daktari wake kwa ajili ya uchunguzi zaidi!
 
Ukweli nikwamba bado anaumwa japo anaendelea na tiba maumivu niyakifua upande kulia kifua anasema hata akipumua bado manasikia maumivu makali hata wakati wakugeuka napenyewe anasikia maumivu lakini kabla ya kunywa mafuta nakumbukz alikuwa akisema nasikia maumivu kifuani inazwezekana limonia alikuwa nayo kabla ya mafuta!!Sasa baada ya maelezo yako unanishauri vipi??Nawengine nisaidieni huyu mgonjwa ni Mama yangu Mzazi!!
 
Pole Kaka Kiiza...wakati mwingine ni vigumu kidogo kutoa ushauri wa kitabibu kupitia forums, kwa sababu kuna maswali meengi ninayotamani kukuuliza na kupata majibu papo hapo ili niweze kukushauri vizuri lakini inashindikana. Kama mafuta ya taa yalifuata wakati tatizo la Nimonia lipo tayari, nachelea kusema kuwa tatizo hilo la kifua limesababushwa na hayo mafuta ya taa, japo inawezekana likawa limekuzwa.

Kama mgonjwa ni mama yako, na wewe ni kaka yangu tayari...nafikiri umri wa mama utakuwa mkubwa na hivyo nafikiri anahitaji uchunguzi toka kwa Dr aliyebobea kwa masuala ya vifua. Nakushauri uende Tumaini Hospital Upanga opposite makao makuu ya jeshi umuulizie Dr Mabula Mchembe. Nadhani akimuona mama atatoa ushauri wa kitaalamu zaidi.
 
Asante nitaenda japo nimemuanzishia matibabu TMJ ila nitaenda kumwona!
 
Back
Top Bottom