Naombeni msaada wenu wakimawazo wanajf wenzangu....... Ndugu hawa

last three months nilipatwa na msiba baba yangu kipenzi, tukazika salama na kila kitu kimeenda vizuri hakukuwa na tatizo lolote..about two weeks sasa yamenza kubumburuka mambo ya nani mrithi wa marehemu...mzee ameacha mtoto mmoja ambaye ndio mimi ninaye andika hii thread na mke ambaye ndio mama yangu mzazi, kiukweli mzee hakuwa na mali za hivyo amecha nyumba yake moja ya kawaida tu na shamba moja na kagari ...sasa kuna baba yangu mkubwa mmoja amenza kusema kwakuwa marehemu ameacha mtoto wa kike basi lazima arithi na ndugu mmoja wa kiume na akapendekeza mwanawe ndio awe mrithi na blaa blaa kibao ...sasa jamani wanaJf wenzangu hii imekaaje
Ni pm nikupe mwongozo
 
...Kwa faida ya wengi, sheria za mirathi zinasemaje hapa?

  • kidini
  • kiserikali
  • kimila (kama itahusika na kabila la Sharobaby)
 
ahsante nshapoa ndugu yangu ntajitahidi kufuata mawazo yenu
anatumia mila za kabila gani huyo babako mkubwa?... ukinitajia kabila nitafuatilia mila ila navyojua mie ..MILA NYINGI ZA KIAFRIKA mama yako angerithiwa na babako mdogo/mkubwa kisha "kama watazaa" mtoto wa kiume then hilo tunda la ndoa ya urithi ndio atakuwa mrithi...hiyo ilikuwa ikitumika sanaa enzi za ujima ila sikuhizi imekwisha...

mwambie huyo dingi yako kuwa marehemu mshua wako nilikuwa namdai tshs 1billion kwa hiyo auze mali za marehemu babako na mali zake yeye na ndugu wengine "WANILIPE PESA ZANGU NISEPE"...wakikubali hilo deni langu waambie na wewe umekubali mwanae arithi jasho la babako...

UMENIELEWA?...MWISHO NAKUPA POLE YA KUPOTELEWA NA MSHUA WAKO...MAAANA NAJUA ANGEKUWEPO PANGECHIMBIKA.
 
dina thank you a lot my dia yaani haya mawazo yenu ni faraja kubwa sana kwangu mimi....laiti mngejua hali nliyonayo sasa na jinsi nnavomuwazia mama yangu anamawazo kupita kiasi, ndugu hawa kweli huwa nlkiuwa nasikia watu yamewakuta na sasa ni zamu yangu
Hilo jina nalo kiboko...................

Umenikumbusha kisa kimoja cha mali za marehemu shem wangu alifariki akaacha nyumba, gari na mashamba (mkewe pia alikuwa ameshafariki) hata kuzikwa alikuwa bado Baba mdogo akaanza kusema gari nitachukua mimi na nyumba nachukua mimi ili nilee watoto wa marehemu (wawili) bwana wewe ule msemo wa kuwa kuna watu huondoka na vitu vyao duniani ulitimia baada ya kuzika na kuanza vikao vya mali hamadi wakati wanachukua nguo za kwenda kumaliza msiba home (kijijini) walichokiona walikoma nacho kila kitu kauza ndani ya wiki mbili walichoambulia ni milioni sita tu ndo walikuta ndani.

Pole sana haya mambo yapo sana ila kuwa ngangari kama vipi mshauri mama uza gari nunua lingine
 
the finest nashkuru kwa mawazo yako na nitajitahidi nifike huko pia...
Sharobaby nakushauri kitu kimoja cha msingi tena fanya haraka wala usifanye mzaha nenda kawaone TAMWA uwaeleze kila kitu ukihitaji msaada wa jinsi ya kufika huko nishtue i will direct you ili ukawaone
 
yaani mngejua how much michango yenu yamawazo inavonipa faraja mungu pekee ndiye anajua..ntakomaa na kutetea haki yangu na ya mama yangu mpaka mwisho na ntaendelea kuhitaji mssada kwenu pia
1st of all POLE SANA,
Ukikomaa kama wachangiaji walivyosema hawatagusa chochote,
Kitu cha kufanya nenda mahakamani uwe msimamizi wa mali za babako.
Hadi lini sisi wabongo tuataacha haka ka mchezo, pindi nduguyo anapokufa unakimbilia mali Wakati anazitafuta ulikuwa wapi?
Kila mtu akarithi vya babake, tena ni baba mkubwa inasikitisha sana.
Wakati mwingine ukikaa na kufikiri unaweza kudhani watu huwa wanaombea mtu afe ili aje warithi.
NCHI INAKUWA MASIKINI KWA TABIA YA KUPENDA VYA ULAINI.
MWENZENU APINDE MGONGO, TENA YAWEZEKANA ALIWASAIDIA LAKINI HAMSAIDIKIKI, ILA MACHO KODO KWENYE MALI ZAKE.
YALISHANIKUTA, SO NINAUJUA UCHUNGU ULIONAO BUT AT THE END OF DAY UTAWASHIDA NA UTAMJUA NANI NI NDUGU WA KWELI.
POLE SANA
 
Pole sana kwa msiba huyo baba ako mkubwa bila shaka atakuwa chizi,yaani mwanae ndio aridhi mali zenu?mvalie miwani ya mbao kama na undugu ufe kabisa,tena mwambie asiguse hata kijiko akikuzingua mpeleke mahakamani,hana chake hapo.
 
Pole sana kwa msiba wa baba yako,
kuhusu urithi wa mali ,, wewe na mama yako ndiyo warithi peke yenu,
uwe mtoto wa kike au wa kiume bado wewe ni mrithi halali tu wa hizo mali,
huyo baba yako mdogo aache uroho wa mali, kifo hakikuumbwa kwa ajili ya baba yako tu,
hata yeye atakufa, je wanaye wakinyanyaswa hivyo atafurahia??,
komaa hakikisha hapati hata thumuni,
akizidisha usumbufu nenda kawaone tamwa, ndiyo watamkata maini kabisa.
Haya ndiyo madhara ya kutokufanya kazi kwa bidii na kusubiri mali ya marehemu.
 
kwanza kabisa tafuta mwanasheria....

na kama una boyfriend ambae ni taff basi awe karibu kwa mapambano

hiii ndo dunia,nenda kwenye viyuo vya watoto yatima utalia ukisikia yaliyowakuta
mpaka wakafika kwenye vituo hivyo...
 
kwanza kabisa tafuta mwanasheria....

na kama una boyfriend ambae ni taff basi awe karibu kwa mapambano

hiii ndo dunia,nenda kwenye viyuo vya watoto yatima utalia ukisikia yaliyowakuta
mpaka wakafika kwenye vituo hivyo...
Namuonea huruma nahisi kama keshakubaliana na hali vile
 
last three months nilipatwa na msiba baba yangu kipenzi, tukazika salama na kila kitu kimeenda vizuri hakukuwa na tatizo lolote..about two weeks sasa yamenza kubumburuka mambo ya nani mrithi wa marehemu...mzee ameacha mtoto mmoja ambaye ndio mimi ninaye andika hii thread na mke ambaye ndio mama yangu mzazi, kiukweli mzee hakuwa na mali za hivyo amecha nyumba yake moja ya kawaida tu na shamba moja na kagari ...sasa kuna baba yangu mkubwa mmoja amenza kusema kwakuwa marehemu ameacha mtoto wa kike basi lazima arithi na ndugu mmoja wa kiume na akapendekeza mwanawe ndio awe mrithi na blaa blaa kibao ...sasa jamani wanaJf wenzangu hii imekaaje

Dada yangu Sharobaby
Kisheria kuna vitu 2 hapa vinahusika. Kwa kuanzia inategemea mambo 2 makubwa:
(i) Kama baba alifariki akaacha wosia (if he died testate)
(ii) Kama hakuacha wosia (if he died intestate).
Kama aliacha wosia wa namna mali zigawanywe basi huo utafuatwa kama ulivyo na kama baba mdogo anakwenda kinyume anabanwa na sheria. Wosia humtaja msimamizi wa mirathi ambaye LAZIMA afuate matakwa ya marehemu kama yalivyo. Akikiuka anashtakiwa mahakamani. Hii ni njia rahisi sana ya kuepusha migogoro baada ya kifo. Lakini sidhani kwa case yako kama mzee aliacha wosia.

Kama hakuacha wosia mahakama ndiyo inayohusika na kumthibitisha msimamizi wa mirathi (administrator au administratix kulingana na jinsia yake). Hufanya hivi baada ya kikao cha ukoo (ndugu) kukaa na kufikia makubaliano nani awe msimamizi wa mirathi. Kumbukumbu (minutes) za kikao hiki LAZIMA hupelekwa mahakamani ambayo humthibitisha au kutengua uteuzi huo. Kwa kawaida kama wewe au mama hamkuridhika na uteuzi wa kikao cha ndugu mnaweka pingamizi mahakama isimthibitishe huyo aliyeteuliwa. Mathalani, mama au watoto ndiye ana haki ya kwanza kuwa msimamizi wa mirathi hiyo kama wameshafikia umri wa utu uzima kisheria. Hivyo kama wewe ni mkubwa unaweza kuwa msimamizi au mama. Lakini ukiwa wewe kumbuka utabanwa na sheria kuhusu namna ya kutumia hizo mali kwa ajili ya mama -mjane wa marehemu. Sio unaanza kutapanya. Baba mkubwa pia anaweza kuteuliwa kulingana na mazingira ya familia yenu na kama nyie mmeridhika. Akishathibitishwa mahakama hutoa maelekezo ya namna ya kusimamia mali hizi (hapa ni pamoja na kupewa jukumu la kuainisha na kubainisha mali zote, mahali zilipo na thamani yake). Haruhusiwi msimamizi wa mirathi kufanya kinyume na hayo au kuzitumia mali hizo kwa ajili yake. Ni kosa na akifanya hivyo mahakama itatengua usimamizi wake pamoja na kuchukuliwa hatua za kisheria.
Kama baba alikuwa anaishi maisha ya kiislamu kuna pia taratibu za kiislamu kuhusu mirathi ambazo zinafuatwa na sheria inazitambua. NB Kuwa tu muislamu kwa dini au jina haitoshi kuwa aliishi kiislamu. Hii inategemea namna "alivyoendesha maisha yake"-je aliincline kwa mirathi ya uislamu au la? Mara nyingi watu ni waislamu lkn mfumo wa maisha yao unaathiria kuwa walipenda mirathi ya sheria ya nchi itumike.
Pia kama aliishi maisha ya kitamaduni sana (ambayo sidhani kama tz wapo tena wengi) basi utaratibu wa customary succession utatumika. NB Utaratibu huu lazima uwe hauvunji sheria za nchi-hasa katiba. Kama kimila mwanamke haruhusiwi kabisa kurithi mali hiyo haiwezi kukubaliwa.
Conclusion.
Kwa maelezo yako nadhani zile namna 2 nilizoeleza pale juu ndio zinaapply kwenu. Kuhusu testate or intestate succession. So, cha msingi muende mahakamani (mahakama ya mwanzo tu inatosha) mfungue shauri la mirathi. NB Hii sio kesi bali ni maombi ya mahakama iwatangaze mmoja wenu (mama hususan) kama msimamizi wa mirathi. Msiogope kwani hapa sio kwamba mnamshtaki baba mkubwa. Mkishampata huyo mtakuwa mmeshakwepa huyo mroho. Huko TAMWA na kwingine hata ukienda watakupaleka ktk utaratibu huu.

Natumaini nimekupa mwanga.
Asante.
 
dada yangu sharobaby
kisheria kuna vitu 2 hapa vinahusika. Kwa kuanzia inategemea mambo 2 makubwa:
(i) kama baba alifariki akaacha wosia (if he died testate)
(ii) kama hakuacha wosia (if he died intestate).
Kama aliacha wosia wa namna mali zigawanywe basi huo utafuatwa kama ulivyo na kama baba mdogo anakwenda kinyume anabanwa na sheria. Wosia humtaja msimamizi wa mirathi ambaye lazima afuate matakwa ya marehemu kama yalivyo. Akikiuka anashtakiwa mahakamani. Hii ni njia rahisi sana ya kuepusha migogoro baada ya kifo. Lakini sidhani kwa case yako kama mzee aliacha wosia.

Kama hakuacha wosia mahakama ndiyo inayohusika na kumthibitisha msimamizi wa mirathi (administrator au administratix kulingana na jinsia yake). Hufanya hivi baada ya kikao cha ukoo (ndugu) kukaa na kufikia makubaliano nani awe msimamizi wa mirathi. Kumbukumbu (minutes) za kikao hiki lazima hupelekwa mahakamani ambayo humthibitisha au kutengua uteuzi huo. Kwa kawaida kama wewe au mama hamkuridhika na uteuzi wa kikao cha ndugu mnaweka pingamizi mahakama isimthibitishe huyo aliyeteuliwa. Mathalani, mama au watoto ndiye ana haki ya kwanza kuwa msimamizi wa mirathi hiyo kama wameshafikia umri wa utu uzima kisheria. Hivyo kama wewe ni mkubwa unaweza kuwa msimamizi au mama. Lakini ukiwa wewe kumbuka utabanwa na sheria kuhusu namna ya kutumia hizo mali kwa ajili ya mama -mjane wa marehemu. Sio unaanza kutapanya. Baba mkubwa pia anaweza kuteuliwa kulingana na mazingira ya familia yenu na kama nyie mmeridhika. Akishathibitishwa mahakama hutoa maelekezo ya namna ya kusimamia mali hizi (hapa ni pamoja na kupewa jukumu la kuainisha na kubainisha mali zote, mahali zilipo na thamani yake). Haruhusiwi msimamizi wa mirathi kufanya kinyume na hayo au kuzitumia mali hizo kwa ajili yake. Ni kosa na akifanya hivyo mahakama itatengua usimamizi wake pamoja na kuchukuliwa hatua za kisheria.
Kama baba alikuwa anaishi maisha ya kiislamu kuna pia taratibu za kiislamu kuhusu mirathi ambazo zinafuatwa na sheria inazitambua. Nb kuwa tu muislamu kwa dini au jina haitoshi kuwa aliishi kiislamu. Hii inategemea namna "alivyoendesha maisha yake"-je aliincline kwa mirathi ya uislamu au la? Mara nyingi watu ni waislamu lkn mfumo wa maisha yao unaathiria kuwa walipenda mirathi ya sheria ya nchi itumike.
Pia kama aliishi maisha ya kitamaduni sana (ambayo sidhani kama tz wapo tena wengi) basi utaratibu wa customary succession utatumika. Nb utaratibu huu lazima uwe hauvunji sheria za nchi-hasa katiba. Kama kimila mwanamke haruhusiwi kabisa kurithi mali hiyo haiwezi kukubaliwa.
Conclusion.
Kwa maelezo yako nadhani zile namna 2 nilizoeleza pale juu ndio zinaapply kwenu. Kuhusu testate or intestate succession. So, cha msingi muende mahakamani (mahakama ya mwanzo tu inatosha) mfungue shauri la mirathi. Nb hii sio kesi bali ni maombi ya mahakama iwatangaze mmoja wenu (mama hususan) kama msimamizi wa mirathi. Msiogope kwani hapa sio kwamba mnamshtaki baba mkubwa. Mkishampata huyo mtakuwa mmeshakwepa huyo mroho. Huko tamwa na kwingine hata ukienda watakupaleka ktk utaratibu huu.

Natumaini nimekupa mwanga.
Asante.

umeongea ila mengi halafu mazito...kama lecture darasani..... Pata picha somo lote unampatia dogo alefiliwa na mshua wake na anataka kunyanganywa mali zake.... Mpe njia mbele aka wayforward na ikipendeza at ziro cost or very minimal one.... Sio aende kwa wanasheria aishie kupigiwa hesabu za asilimia ya mali ya marehemu kumlipa wakili...ni sooo
 
sharobaby, je ninyi ni dini gani?
maana kwa sheria ya kiislamu, kama hakuna wosia (will) ya marehemu kusema urithi ugawanywe vipi, hapo ni shida kubwa sana, kwani kama ndugu za marehemu baba yako (siblings) watatumia sharia/sheria za kiislamu basi ni kweli mtoto wa kike si mrithi pekee wa baba yake na mke pia si mrithi pekee, mali hurithiwa kwa mafungu yaani mtoto/watoto wa kike wana percent yao, mama naye/nao wana percent yao na percent pia ipo kwa siblings (ndugu wa kiume na kike wa marehemu) ambayo kwa experince niliyopata katika familia yetu ni kubwa zaidi.
Sasa mkitaka kupinga ugawaji wa jinsi hii inabidi mfungue kesi mahakamani ya kupinga ugawaji wa mali kufuata sheria za kiislamu. kesi za hivi huwa haziishi, na mtakuwa mnaendelea kufaidika kutumia mali za baba yenu hadi forever! nina ndugu zangu wana kesi ya aina hii tangu 1982. Hata kama kesi itachukua forever kuamuliwa, it will be to your advantage,
cheers!
 
ninavosoma michango yane i feel like crying nashkuru sana kwa maneno yako na mawazo yako
Pole sana kwa msiba wa baba yako,
kuhusu urithi wa mali ,, wewe na mama yako ndiyo warithi peke yenu,
uwe mtoto wa kike au wa kiume bado wewe ni mrithi halali tu wa hizo mali,
huyo baba yako mdogo aache uroho wa mali, kifo hakikuumbwa kwa ajili ya baba yako tu,
hata yeye atakufa, je wanaye wakinyanyaswa hivyo atafurahia??,
komaa hakikisha hapati hata thumuni,
akizidisha usumbufu nenda kawaone tamwa, ndiyo watamkata maini kabisa.
Haya ndiyo madhara ya kutokufanya kazi kwa bidii na kusubiri mali ya marehemu.
 
yap ni muislam na nitajitahidi kufata mawazo yako naona anataka kutumia dini kama njia ya kujipatia mana nashangaa kwanini yeye achague mwanawe??na ndugu wako wengi???
sharobaby, je ninyi ni dini gani?
maana kwa sheria ya kiislamu, kama hakuna wosia (will) ya marehemu kusema urithi ugawanywe vipi, hapo ni shida kubwa sana, kwani kama ndugu za marehemu baba yako (siblings) watatumia sharia/sheria za kiislamu basi ni kweli mtoto wa kike si mrithi pekee wa baba yake na mke pia si mrithi pekee, mali hurithiwa kwa mafungu yaani mtoto/watoto wa kike wana percent yao, mama naye/nao wana percent yao na percent pia ipo kwa siblings (ndugu wa kiume na kike wa marehemu) ambayo kwa experince niliyopata katika familia yetu ni kubwa zaidi.
Sasa mkitaka kupinga ugawaji wa jinsi hii inabidi mfungue kesi mahakamani ya kupinga ugawaji wa mali kufuata sheria za kiislamu. kesi za hivi huwa haziishi, na mtakuwa mnaendelea kufaidika kutumia mali za baba yenu hadi forever! nina ndugu zangu wana kesi ya aina hii tangu 1982. Hata kama kesi itachukua forever kuamuliwa, it will be to your advantage,
cheers!
 
gaga nashkuru kwa kunionea huruma..nimelileta suala hili Jf ili nipate mwanga wapi nianzie na nashkuru mungu kwa mawazo yenu najua ntashinda ntaendelea kuwapa habari jinsi gani issue inavyoenda
Namuonea huruma nahisi kama keshakubaliana na hali vile
 
Kuna sheria za kimila pia na mahakama inazitambua. Kwa hiyo inategemea nyie ni kabila gani na baba na mama yako walikuwa wanafuata mambo ya kimila au la. Kuna makabila nilishasemaga hapa si ya kuolewa ni noma when it comes to mirathi. Sasa tunakutana kimjini mjini hivyo vitu hatuvizingatii. Linapotokea tatizo ndo utajua mila zote za upande wa mumeo.
 
Na kama ni waislamu, mtoto kama alizaliwa nje ya ndoa hana chake. Na nje ya ndoa kiislamu ni complicated kwani nina jirani yangu alikuwa na mtoto mmoja tu. Alipokufa ndio nikajua yule mtoto alizaliwa kabla baba na mama yake hawajafunga ndoa. Na mtoto akaambiwa regardless wale wote walikuwa wazazi wake, yeye ni wa nje ya ndoa na hana chake. Nilichoka kabisa
 
umeongea ila mengi halafu mazito...kama lecture darasani..... Pata picha somo lote unampatia dogo alefiliwa na mshua wake na anataka kunyanganywa mali zake.... Mpe njia mbele aka wayforward na ikipendeza at ziro cost or very minimal one.... Sio aende kwa wanasheria aishie kupigiwa hesabu za asilimia ya mali ya marehemu kumlipa wakili...ni sooo

Ndugu Who Cares,
Sijui way forward gani unataka nimpe tena. That is the best and most secure way ya yeye kuhakikisha usalama wa mali zake. Sijamwambia aende kwa wanasheria (mawakili) bali nimemuelekeza aende mahakamani athibitishwe kama msimamizi wa mirathi. Hii haina gharama yoyote. Ni utaratibu uliowekwa. Sasa maelekezo ya usimamizi itatolewaje na mahakama bila mtu kuiomba? Kumbuka nimesema hii ya kwenda mahakamani sio kesi per se. Kwa hiyo hahitaji kuargue chochote.Anapeleka tu uthibitisho wa kifo na maombi yake (anasaidiwa namna ya kuweka hayo maombi kwa njia ya fomu ya mahakama). Mahakama itatoa siku kama sijakosea za mtu yeyete kupeleka pingamizi kama lipo na baada ya hizo siku anatangazwa (yeye au mama kulingana na nani ameomba) kuwa msimamizi wa mirathi. So, sioni hizi cost implications unazoona wewe zimetoka wapi. Au nauli ya kwenda mahakamni? au lunch wakati akienda?. Shida ni kuwa watu wengi mkishatajiwa mahakamani kwa jambo lolote mnafikiria gharama za mawakili etc. Sio ktk hili.
Anyway, I gave my professional advice. Kama is costly kuufuata sawa ila kutoufuata will prove more costly.

Asante.
 
Back
Top Bottom