Naombeni Msaada wa mawazo tafadhali

Pole SweetDada, mapenz yanaumiza sana, kaa nae umwambie hiyo tabia hukufurahishwa nayo na usikie atakuambia nini. By the way ukiona dalili za Moshi ujue moto upo.


Wapendwa wana JF nawasalimu wote, natumai mu wazima.

Kuna jambo lanitatiza nahitaji msaada wa mawazo, yawezekana kabisa muamuzi wa mwisho ni mimi mwenyewe ila nikipata mawazo tofauti itasaidia pia.

Nina mchumba wangu ambae tunatarajia kufunga ndoa hivi karibuni. Wiki iJuzi Jumanne niliibiwa simu so yeye akanipa simu yake nitumie.
Hamadi kwenye simu nikakuta texts kwenye inbox ambayo kutokana na flow ya zile texts alikuwa akichat na mwanamke, na ikaonyesha kabisa yule mwanamke waliwahi kuwa na mahusiano na kudo pia, ha hiyo imetokea akiwa na mimi, mana yule dada aliandika kabisa kuwa "bahati ulikuwa nayo wewe tu ya kukupa ....), na nyingine lukuki za kuonyesha mdada ana wivu kuwa amesikia jamaa ana mtu mwingine yani apart from me, na huyo dada anaonyesha kunifahamu mana kuna msg baada ya jamaa kumwambia kuwa hao anaowasema si watu zake hata mchumba wangu (yani mimi) anawajua, mdada akahamaki na kutaja jina langu..

Nilijaribu kuongea na huyo mume mtarajiwa lakini alikana katukatu hajawahi kuwa na uhusiano na mtu huyo ni jokes tu, kama nataka nijaribu kuchukua simu yake nione jinsi gani wanawake wanamchatisha mambo makubwa kuliko hayo. mimi sikubuy story yake kwa kweli hapa kichwa kinaniuma kwa mawazo. Na cha kushangaza yeye kutwa akiongea na simu ni kuita wanawake baby sasa hata akiniita mimi sioni kama kuna uniquness yoyote.

Naombeni msaada wa mawazo tafadhali, nina mawili nimuache au nibaki, na mahali keshatoa. nikimuacha je nitakayempata atakuwa na afadhali au atakuwa worse.nina maswali mwngi kichwani kuliko majibu.

Natanguliza shukrani.

Sweetdada
 
Ni kweli hakuna aliye perfect lkn hiyo isiwe kisingizio. Yaani nikute meseji kwa mchumba wangu anamsifia mwanaume mwingine kuwa alimtia vizuri, anajua kubembeleza nk bado unidanganye kuwa kuna watu wanapenda utani mara ooh hakuna mkamilifu na utumbo kibao...! Walah namtoa baru aende akafaidi huo 'utani' wake kwa uhuru zaidi. Hivi baada ya 'utani' wa kijinga hivo huwa mtu anapata sh. ngapi?! Huu ulimbukeni wa mawasiliano huu, utawacost wengi.
 
Ushauri wa maisha ndo huu. Hata bible imeandika mwanamke mpumbavu hubomoa nyumba yake kwa mikono yake mwenyewe, bali
mwanamke mwelevu huijenga nyumba yake kwa mikono yake mwenyewe. Cha msingi maisha tunayoishi sisi hakuna jipya, yote haya nia marudio na yatakuja makubwa zaid haya, mvumilie mpe nafasi na mkiwa ndani atatulia. Unajua hisia tofauti sana na matamanio. Kuwa mpole usikwazike wala usimuulize lolote akuone km mjinga siku ya kuja kujua thaman yako yeye atakuwa chizi zaidi yako atataka mpaka chooni akusindikize.
 
Haya maisha yanazidi kuwa kizungumkuti kabisa,

Nakushauri uyasikilize mapigo ya moyo wako.....Kama moyo bado unampenda basi usimdhulumu kwani mapenzi huvumilia kila karaha!!

Ila ufahamu tu kwamba huyo mchumba wako ni mtaalamu wa kuchombeza chombeza...Kama utayaweza basi banana naye, kwa sababu huwezi kuwa na uhakika mwingine utakayekutana naye atakuwaje!!!

Babu DC!!
 
baby,piga chini hiyo ndude,tena fasta,ukimlegezea atakuletea ukimwi! Mbwa takataka hiyo,achana nayo!
 
hao ndo opportunist wenyewe,kwanini usitafute mwingine mwaminifu na atakaekupenda kwa moyo wote???kwanini kuhangaika na jitu kama hilo ambalo halithamini utu wako??ungekuwa umefunga nae ndoa hapo kweli tungekuambia vumilia dada huna jinsi.sasa mtu hata ndoa bado anacheat,usidhani akikuoa ndo atabadilka.ndoa haimbadilishi mtu my dear.focus on your things una mambo mengi sana ya kufanya kujiendeleza badala ya kupotza muda na watu wa jinsi hiyo ukidhani one day watachenji.fikiria mara mbili.wanaume wako wengi sana tena wenye utu kuliko huyo.jijali tafadhali.
 
Watu wepesi kweli kushauri umuache,sio mwaminifu....hao waaminifu wako wangapi na probability ya kumpata aliye mwaminifu 100% ni kiasi gani?? Nakushauri, usikilize moyo wako na akili yako, wewe unamjua vizuri,binafsi nachukia cheating,ila ninavyozidi kukua naona kama uwezekano wa kumpata ambaye atakuwa mwaminifu kwangu kwa asilimia 100% ni mdogo, nasikiliza moyo wangu na akili yangu juu ya mwanaume. Kama nimempenda naye kanipenda,ananiheshimu na walio wangu,ananitunza na kunisaidia kuwa bora zaidi,nina furaha.....etc....natulizana hapo hapo....hadi ni-prove ni cheater wa kupitiliza hadi anashindwa majukumu yake ndo nitamuacha,sina muda wa kubadili wanaume kila kukicha,ni wale wale tu.....!
 
Watu wepesi kweli kushauri umuache,sio mwaminifu....hao waaminifu wako wangapi na probability ya kumpata aliye mwaminifu 100% ni kiasi gani?? Nakushauri, usikilize moyo wako na akili yako, wewe unamjua vizuri,binafsi nachukia cheating,ila ninavyozidi kukua naona kama uwezekano wa kumpata ambaye atakuwa mwaminifu kwangu kwa asilimia 100% ni mdogo, nasikiliza moyo wangu na akili yangu juu ya mwanaume. Kama nimempenda naye kanipenda,ananiheshimu na walio wangu,ananitunza na kunisaidia kuwa bora zaidi,nina furaha.....etc....natulizana hapo hapo....hadi ni-prove ni cheater wa kupitiliza hadi anashindwa majukumu yake ndo nitamuacha,sina muda wa kubadili wanaume kila kukicha,ni wale wale tu.....!

Huu ni aina ya ushauri tunautegemea kutoka kwa dada mkuu!!

Wakati mie niko mdogo, dada yangu alikuwa akija kushitaki nyumbani kila anapokuwa na ugomvi mkubwa na mume wake....Ilikuwa inaniudhi sana hadi namshauri aachane naye!! Leo siwezi kusema kitu kama hicho!

Babu DC!!
 
Huu ni aina ya ushauri tunautegemea kutoka kwa dada mkuu!!

Wakati mie niko mdogo, dada yangu alikuwa akija kushitaki nyumbani kila anapokuwa na ugomvi mkubwa na mume wake....Ilikuwa inaniudhi sana hadi namshauri aachane naye!! Leo siwezi kusema kitu kama hicho!

Babu DC!!

Asante Babu DC, mimi ni uzoefu wangu tu mdogo, wengi wa waliokimbia wapenzi wao kwa kosa moja au mawili ya cheating,wamejikuta wakiwa dissapointed zaidi na zaidi na kurudi nyuma inakuwa ngumu. Nimeshuhudia watu wanakuwa na wanaume zaidi ya ishirini na bado wanatafuta that perfect man that doesn't cheat...! Its not realistic and there will never be a guarantee that the next man won't cheat...ukimuacha uliye naye...usiwe na mtu tena,hapo hutakuwa na expectation na hutakuwa dissapointed.
 
Asante Babu DC, mimi ni uzoefu wangu tu mdogo, wengi wa waliokimbia wapenzi wao kwa kosa moja au mawili ya cheating,wamejikuta wakiwa dissapointed zaidi na zaidi na kurudi nyuma inakuwa ngumu. Nimeshuhudia watu wanakuwa na wanaume zaidi ya ishirini na bado wanatafuta that perfect man that doesn't cheat...! Its not realistic and there will never be a guarantee that the next man won't cheat...ukimuacha uliye naye...usiwe na mtu tena,hapo hutakuwa na expectation na hutakuwa dissapointed.

Kweli ndugu,

Watu wanatakiwa kujua kuwa maisha ni sadaka...lolote utakaloamua kufanya lazima utalipia gharama yake...

Hata akiamua kuishi peke yake (single) for life...si jambo rahisi kabisa!!

Anyway, ngoja tumwachie mwenyewe aamue!

Babu DC!!
 
Kuna watu wamekushauri vizuri na kuna watu wamekutisha sana, kwanza sio kweli kwamba wanaume wote wako hivyo hizo ni hulka tu. Lakini kuhusu suala la mumeo mtarajiwa bado mna nafasi ya kurekebisha uzuri ni kwamba umegundua mapema cha msingi kaeni chini mzungumze kweleze dukuduku lako la hatua ambazo utazichukua ikiwa utagundua kwamba ana mahusiano mengine kama yalikuwepo mwisho uwe hiyo siku ya mazungumzo kama yalikuwepo hapo awali mweleze hutaki kusikia anaendelea kukuletea stori za kwamba alikuwa ni xgf wake.
Usikimbilie kuvunja mahusiano, tatua tatizo dadangu.Mimi sioni ugumu wa suala lako hata kidogo.
 
unasemaje?
Yupo busy na simu kuwaita wanawake 'baby?' na wewe umetulia wenzio wana-bebi-wa?

Zungumza nae kwa herufi kubwa! Kama anakuonyesha ufirauni wake mapema akikuoa si ndo atakuletea wanawake ndani?
Mwanaume gani hana heshima kwako wala staha?

Eti kasema akupe cm yake? Kama una kifua Ichukue tena kwa kumsuprise kaa nayo masaa 4 tu utapata jibu.

Na umwambie huyo mwanaume awe na msimamo! Mahari kitu gani bwana,heshima kwanza! Mwambie Abadili Tabia, mchunguze ukiridhika ndo uende nae next step
 
kama tatizo ni hilo tu nashauri umueleze hisia zako na jinsi gani usivyopendezwa na tabia yake. Sio rahisi sana kumpata mtu ambae mtalandana na kushabihiana kiasi cha kufikia hatua za kutaka kufunga ndoa. Don't give up that easily like anything else in life go and fight for your love. Wanaume/wasichana wanaishi katika jamii yenye marafiki kazini, mashuleni gym etc ambao hutokea kuzoeana na kutaniana japo sio lazima kuwa na mpango wa kando, watu hatuishi katika kisiwa cha msingi mueleze jamaa on a serious note kwamba sasa anaoa hivyo aache mipango ya kando na marafiki wenye nia mbaya. Wazazi wa kale ukifuatilia wali-sacrifice sana ikiwa ni pamoja na kuvumilia kuendelea kuwa na mke/mume aliye-cheat na kuzaa na jirani. No one is perfect maranyingine watu hufunzwa na kubadilishwa na wapenzi wao. Ila kama haelekei kabisa kubadilika na haheshimu muafaka, it's never too late, you can always jump off the ship and looking for the next.
 
Kitendo cha kusema kakataa katu katu means kua bado anakupenda ama kukuhitaji na huyo dada hana maana yoyote. Kwa upande wangu mambo ya messaging hasa hizi za chatting hazina uzito saana kwangu for nisha ona na nisha experience kua katika chatting you go with flow na kusema mambo mengi ambayo mara nyingi wahusika wanakua hawaja maanisha kabisa... Mara nyingi walengwa hutuma messages ambazo mpokeaji kwa wakati huo angependa asikie....

Kupata mtu (hasa mwanamke ama mwanaume) alo bora na anafaa kua mwanandoa... imekua mtihani saana siku hizi na only God knows wapi hasa tunaenda with this. However kama ndio atarajia kua shemeji yetu kuna ya msingi maswali ya kujiuliza... Anakupenda? anakuheshimu? Does he take good care of you? Does he seem to be like he will be a good dad/hubby? Yupo responsible na reliable pia? If the answer is "YES" kwa maswali yoote haya... then he is a good Man na waweza mpa nafasi tokana na moyo wako utavo amua. All the Best katika maamuzi yako.
 
Don't Cry for Someone who Can't Cry for You!!:focus:nilikuwa na mpenzi wangu nilimpenda kwa moyo wangu wooote,nilimuamini saana nilikuwa muaminifu 100% enzi zake izo.yaani kila kitu changu kilikuwa chake.simu yangu nilikuwa naweza kumpa au hata kama nimeisahau kwake naiacha hadi aniletee sio sasa nikisahau mahali nipo radhi kukodi hata ndege niifate maana atazimia kama si kufa. ila simu yake ilikuwa ni marufuku kabisa kuishika kwa sababu ya ujinga na upofu wa mapenzi sikuona ni tatizo.one day hamada nikaipata iyo simu kama ya kwakoooo sms kibao nikapuuzia nikaja kumwagwa shosti lonely lonely nimebakia maweeeeeeeeee

You won't be lonely for long..............the Almighty God has better plans for you.........
 
Mara nyingi walengwa hutuma messages ambazo mpokeaji kwa wakati huo angependa asikie....

could be true...........but love is not about the past but rather is all about........"our future" for those who are stupid enough to fall into its maze of traps............
 
Asanteni wote mlionipa ushauri na mawazo yenu. Mbarikiwe sana.

Kusema ukweli mchumba huyu ana kila sifa za kuwa mume/baba, kasoro ni hiyo ya kuita ita wanawake baby na hizo texts nilizokumbana nazo, apart from that he is a good man.
Nasema tena asante kwa mawazo yenu, yananisaidia kwa namna moja ama nyingine kwenye kuona the other side of the coin.

Weekend njema wote.
 
mwe shosti pole, kumbe na wewe yalikukuta!!

simu hizi zina mambo, angefuta msg zake kabla hajanipa simu leo nisingekuwa najua mauzauza yake, ila pia nashukuru kuwa nimejua..sasa nipo njia panda looh sijui naanzaje kufanya nini[/QUOT

mtenda kosa mara ya kwanza simkosaji, kosa ni kurudia...so mkalishe chini hubby wako 2b mzungumze siriazly na umfungukie how u feel abt that ishu blah blah...utanote tu if waweza msamehe mkaendeleza mapenzi. usikimbilie kumwacha
 
Somo la leo: usikague simu ya mpenzi wako. Pressure tupu. (japo mimi nakagua, yan lazima nikague)

Sent from my Nokia Lumia using Tapatalk
 
Back
Top Bottom