Naombeni msaada sijui pa kuanzia Wakuu!

Bosco Ntaganda

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
710
288
Wakuu, mimi ni mwalimu wa leseni tangu mwaka 2006, sasa nimehitimu Higher Diploma ya IT hivi karibuni. Nimerudi kuendelea kufundisha kwenye shule niliyo kuwa nimepangiwa kufundisha. Sasa kwa kuwa sikusomea taaluma ya ualimu, na nipo kwenye payroll tangu mwaka huo wa 2006, huku nikiendelea kupandishwa madaraja kama kawaida.
Naombeni mnipatie taratibu za kufanya ili niweze kuhamia kwenye kazi ya taaluma yangu (IT) hapa halimashauri ya jiji ninapofanyia kazi.
 
watakuja hapa watu wa halimashauri wakuelekeze cha kufanya dogo, vuta subra tu!
 
Tatizo ni hawa watu wa jiji, idara ya elimu ndiyo wanaonipa vitisho, wanadai eti kwakuwa sikusomea ualimu hawanitambui, hivyo sitaweza kupatiwa barua ya kuthibitishwa kazini na kuendelea kupanda vyeo, nimechanganyikiwa wakuu!
 
Umekuwa kwenye payroll tangia 2006? Una pesa kidogo kama TZS 500,000 nikusaidie? Unataka Halmashauri gani?
 
Umekuwa kwenye payroll tangia 2006? Una pesa kidogo kama TZS 500,000 nikusaidie? Unataka Halmashauri gani?
mkuu hadi sasa bado nipo kwenye hii halimashauri ya jiji la hapa mbeya. Tatizo ni hii taaluma niliyo nayo kwa sasa (IT) haitambuliki kwenye idara yangu ya elimu sekondari. Msaada ninao uhitaji ni namna gani naweza kuhama kwenye hii idara ya elimu pasipo kuathiri ka-mshahara kangu. Sikwamba nahitaji ajira mpya mkuu, nahitaji kujua jinsi gani nitaweza kuhamia idara watakayo nitambua mkuu.
Nipo tayari kufuata masharti yako mkuu, tunaweza kuwasiliana tu
 
Kiwango changu cha mshahara hadi sasa ni TGTS D8, sina barua ya ajira, ninayo leseni tu, niliyopewa mwaka 2006. Vilevile sina TSD namba, kwa hivi nipo nipo tu wakuu wangu, mwalimu si mwalimu, yaani si eleweki. Baada ya kupewa hiyo leseni sikusomea tena taaluma yeyote ya ualimu, badala yake nilisomea Higher Diploma ya IT, sasa nipo njia panda, sijui nifanyaje ili niweze kuendelea na utumishi wa serikali, kwa taaluma niliyonayo sasa (IT), kwenye hii halimashauri yangu ya jiji. Nahitaji msaada wenu tafadhali
 
dogo hapa naona kama hautaweza kupata mawazo mazuri, jukwaa hili wamejazana waalimu wakilalamikia mara malimbikizo, mara mishahara, mara sijui nini.
vile vile sidhani kama wanafurahishwa na jitihada zako za kutaka kuwakimbia kwenye viboko vya sisiemu, hahahaa.
Ushauri wangu kwako kijana ni huu, andika barua kwa mkurugenzi wako wa jiji, ukimuelezea wasifu wako kwasasa, ambatanisha na nakala za vyeti vyako vya sasa, halafu sikilizia..
 
haaaah haaaah haaah ww kweli Jimbi.
hahahaaa, mkuu si umewasikia mwenyewe, mara wamelala sakafuni kwenye ukumbi wa jiji, mara mkurugenzi amewanyima posho zao, unategemea watatoa mawazo ya msaada hapo? NEVER
 
hahahaaa, mkuu si umewasikia mwenyewe, mara wamelala sakafuni kwenye ukumbi wa jiji, mara mkurugenzi amewanyima posho zao, unategemea watatoa mawazo ya msaada hapo? NEVER
kaka punguza ukali aisee
 
dogo hapa naona kama hautaweza kupata mawazo mazuri, jukwaa hili wamejazana waalimu wakilalamikia mara malimbikizo, mara mishahara, mara sijui nini.
vile vile sidhani kama wanafurahishwa na jitihada zako za kutaka kuwakimbia kwenye viboko vya sisiemu, hahahaa.
Ushauri wangu kwako kijana ni huu, andika barua kwa mkurugenzi wako wa jiji, ukimuelezea wasifu wako kwasasa, ambatanisha na nakala za vyeti vyako vya sasa, halafu sikilizia..
nashukuru sana kaka, naona nimepata pa kuanzia sasa
 
2006-2012-7yrs exp..aisee najiuliza umepataje kazi wakati kila kazi nikisoma inaitaji 10yrs exp

ongeza 3 watakurekebishia 10 yrs ndio full exp mpwa komaa
 
Mi naona uendelee kufanya kazi yako ya ualimu
huku unaandika barua za maombi ya kazi yako mpya
ukiitwa kwenye interview na kufanikiwa ajira ya IT
itakubidi uandike barua ya kuacha kazi kufuatana na taratibu za ajira yako ya ualimu.
 
2006-2012-7yrs exp..aisee najiuliza umepataje kazi wakati kila kazi nikisoma inaitaji 10yrs exp

ongeza 3 watakurekebishia 10 yrs ndio full exp mpwa komaa
kaka ulisoma vizuri maelezo yangu pale juu? rudia utanielewa
 
Mi naona uendelee kufanya kazi yako ya ualimu
huku unaandika barua za maombi ya kazi yako mpya
ukiitwa kwenye interview na kufanikiwa ajira ya IT
itakubidi uandike barua ya kuacha kazi kufuatana na taratibu za ajira yako ya ualimu.
ahsante dada kwa ushauri wako mzuri. lakini tatizo langu mie siyo kuacha kazi halafu nitafute nyingine. ninachohitaji ni kuhamia idara nyingine ili nisipoteze haki zangu, nimeingia kwenye ualimu tangu 2006 dada, you can imagine!
 
2006-2012-7yrs exp..aisee najiuliza umepataje kazi wakati kila kazi nikisoma inaitaji 10yrs exp

ongeza 3 watakurekebishia 10 yrs ndio full exp mpwa komaa
wewe kijana wakati unaandika hapa ulikuwa umelewa, sivyo?
 
wewe kijana wakati unaandika hapa ulikuwa umelewa, sivyo?
Duh, kumbe huu mjadala ulifikia hatua hii? Ndugu zanguni samahanini sana, nilichelewa kuwapa feedback, nilikwisha fanya maamuzi magumu. Wale maafisa utumishi walijifanya kama miungu watu, basi nikaamua kuwaachia kazi yao kimya-kimya
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom