Naombeni msaada jamani

Yote inategemea na msimamo wenu wakati wa maisha yenu ya ndoa. Mwanzo mwanzo mnaweza msiwe na tatizo nyinyi wawili tu lakini matatizo yakaanza wakati mkipata watoto, kila mmoja kutaka kushinikiza watoto wafuate dini yake. Mkisema muwape watoto uhuru wa kuamua wenyewe mtakuwa hamwatendei haki katika malezi ya udogoni kwa kukosa mafunzo ya kiimani. Huwezi kumpeleka mtoto kanisani, msikitini, hekaluni...kwa wakati mmoja. Ili kuepusha hayo, ni bora mkajadiliana na kukubaliana kabla ya ndoa nini mtafanya katika malezi ya watoto wenu.

nimependa sn ushauri wako!maan ni kama umesoma mawazo yetu!asante
 
Kuishi pamoja kwa wenza kwa dini tofauti ni mtihani kwa watoto iwe mmeachana ama mnaishi pamoja hii kitu imevuruga sana familia yetu kwani watoto wengine hujiita mi mwislam mkristo. Nashauri kubalianeni kuwa na imani moja Mungu wetu ni yule yule ingawa njia za kufika kwake ndizo zenye tofauti.

na ugumu unaongezeka zaidi pale support ya wazazi inapokosekana!
 
ni makubaliano yenu nyie wawili mliopendana , mkikubaliana kuhusu izo iman zenu bs inatosha.
wazaz mnawaweka 2 sawa, me nadhan dini sio big deal kiivyo. kama mmependana u discus n then u conclude bs.

naomba unipe njia za kuwaweka sawa wazazi,utakuwa umenisaidia sn!
 
Inategemea na family of origin kwenu wote (mpendanao)

Kama ni nucleus hapo its all up to you
Kama ni extended type in which mpaka mume wa shangazi naye anapewa room ya kuchangia mahusiano yenu hapo kazi ni kubwa kuliko hiyo ndoa yenyewe

So angalia familia zenu kwanza then weigh out

halafu nilikuwa sijajua kama nimekuwa na xtended family,ndio umenizindua!
 
Sijui kama kuna faida zake, manake utofauti wa kiimani ni changamoto kubwa sana. Ninachokushauri,zungumzeni nyie wawili kwa upana sana,na katika yote hakikisheni mnawashirikisha wazazi wenu,manake nyie mnaweza kuwa hamna tatizo ila wazazi ambao ni kiungo muhimu wakawa na tatizo....haipendezi mwanaume aende msikitini na mwanamke aende kanisani, inahitaji hekima sana kuishi maisha yenu yote hivyo, jadilini hili kwa upana na uhalisia mapema kabisa,mkikubaliana na changamoto go ahead!1
 
Huwa sishauri mtu kubadili dini kwa sababu ya mume au mke,bali mafundisho ya imani husika tu.mfano unaenda dini ya mume ni mkristo ,je Unampenda Yesu? ,umewahi kusikia habari zake,siyo unanyanyuliwa tu na kupachikwa kwenye dini ambayo kwa zaidi ya miaka 20 huijui na huyo anayekupenda siyo pastor au sheikh atakulazimisha kufuata ya kwake wakati utayari wa kiroho haupo bali mpo pale kimwili tu na kila imani ina namna yake kutafsiri ndoa!ni bora ujifunze kwa ufupi imani ya huyo umpendaye na uone ktk mahusiano utaathirika vipi.Ziko imani zinaruhusu wake wengi (talaka)uko tayari kumpokea mwenzako mbeleni.?Dini inatoa picha aina ya uhusiano wa ndoa utakavyokuwa ,sasa kama mwingine anaomba kwa Jina La Yesu na mwingine la Mtume,mtaleta machafuko kwenye uhusiano na unaweza ujute maisha yako yote!sio kwamba wenye imani mfanano hawana shida ,ila ugumu unapungua.
 
Sijui kama kuna faida zake, manake utofauti wa kiimani ni changamoto kubwa sana. Ninachokushauri,zungumzeni nyie wawili kwa upana sana,na katika yote hakikisheni mnawashirikisha wazazi wenu,manake nyie mnaweza kuwa hamna tatizo ila wazazi ambao ni kiungo muhimu wakawa na tatizo....haipendezi mwanaume aende msikitini na mwanamke aende kanisani, inahitaji hekima sana kuishi maisha yenu yote hivyo, jadilini hili kwa upana na uhalisia mapema kabisa,mkikubaliana na changamoto go ahead!1

Nashukuru sana kwa ushauri jamani,maana naona wotemko positive sana asanteni.
 
Back
Top Bottom