Naombeni mnipokee kijana wenu!

Mgaya D.W

JF-Expert Member
Jan 20, 2012
965
475
naitwa Mgaya D.W,mwanajf mgeni wenu.nimechagua jf kuwa darasa na mwalimu wangu.nimewachagua wanajf kuwa walimu na viongozi wangu ktk kujadili,kudadisi,kuibua,kutafakari na hata kutafiti mambo mambo mbalimbali yanayohusu jamii. jf limekuwa darasa na jukwaa mahususi kwa great thinkers,nami nimeona si dhambi wala dhihaka kuwa sehemu ya familia hii. nitafuata sheria,kanuni,miongozo na taratibu ili nipate kujifunza na kulelewa kwa mujibu wa sera za jf. nahitaji wenu ushirikiano wa dhati,nipo tayari kurekebishwa na nitarekebika pale nitakapokwenda tofauti pia nipo tayari kuchangia mawazo yangu pale nitakapoona nastahili kufanya hivyo. tuwe pamoja nyakati zote. wenu mgaya d.w!
 
Back
Top Bottom