Naombeni kujua, hapa Tanzania ISP yupi ni bora katika Huduma ya Internet services na Email!

MLINGANO

Member
Nov 26, 2013
15
2
Jaman Naombeni kufahamu ISP gani Hapa Tanzania yupo vizuri kwenye huduma ya Internet services na Emails? Me binafsi Niliwatumia SimbaNet Siwaelewi vizuri Nataka kuwapiga chini na kutafuta wengine so nimekuja kwa wadau kuomba msaada!
 
simbanet huwaelewi au huna hela? unatumia huduma yao ya internet za waya?

unaweza cheki hawa jamaa wa 4g kama internet yako ipo mjini, Kuna tigo, smile, smart, voda na TTCL
Mzee Mkwawa Mimi naishi Kimara Temboni, kwa miaka nimekuwa natumia Smile ila nimeshawachoka kabisa, Nimejaribu kufunga mkonga wa Vodacom Supakasi ila eneo ninaloishi halina network, Hivyo naomba ushauri ni huduma gani Nyingine ambayo itanifaa.
 
Kuna mtu alisema TTCL mbezi hawajafika, jaribu kuuliza eneo lako kama wapo.

Kama hawapo ni hizi internet za mitandao ya simu zilizobakia. Vodacom 50,000 kwa mwezi ama Tigo postpaid.
 
Nilienda ttcl offices mlimani city waliniambia fiber yao imefika mbezi mwisho, lakini gharama za kuleta most areas nje ya mbezi mwisho ni around 2-3M
 
Adsl mkuu, maana siku hizi wameshusha bei mpaka 25,000 ndio sisi walalahoi tunaponea humo.
 
Unaweza kufafanua zaidi? I'm unfamiliar with this. I'm also looking for option ya internet huku mkuu acha tu
Kuna uzi upo hapa

Baada ya comments mbalimbali tukaja tukajua ni Adsl, internet ya kizamani ile ya dial up tulikuwa tunatumia hata kwa Modem,

Si mbaya 4mbps kwa 25,000 hata kama ping ni mbovu inaweza kamilisha basic task za hapa na pale, so far hakuna mjuzi alieleta feedback ya maana ila watu wanatumia.
 
Bado naona changamoto hapo
 
Kuna mtu alisema TTCL mbezi hawajafika, jaribu kuuliza eneo lako kama wapo.

Kama hawapo ni hizi internet za mitandao ya simu zilizobakia. Vodacom 50,000 kwa mwezi ama Tigo postpaid.
TTCL speed yao ni ya kobe mzee, Upload speed yao ni mb 1 per sec wakati vod ni mb 20, Una experience na jamaa wanajiita simbanet
 
Simbanet nawafahamu mkuu, ila bei zao si za kitoto. 1mbps upload na 4mbps download si mbaya kwa 25,000 kwa mwezi, Hata kama utapata nusu ya Hio, kuweza kustream 480p ama 720p Netflix ama youtube ikakaa nyumbani TV na vitu vidogo vidogo vikatumia ni nzuri. Inapunguza pia makali ya Bando kwa Familia nzima.
 
Nilikuwa nawazia kuweka kile cha 50k kwa 8mbps ila kuna mdau amenipa feedback kuwa anatumia hicho cha 25k kwa ajili ya office yake yenye watu takribani 10+ na bado anaweza stream HD plus download movies. So nadhani kwa wengine tulio peke yetu au familia ndogo kitatufaa uzuri tu.
 
Nilienda kuulizia office kwao kwa eneo langu natakiwa tu kulipa 25000 bila installation fee yoyote. Pia modem wameniambia ninunue mwenyewe.

Hivyo naplan kuitest.

Pia nina wasiwasi kama Adsl inaweza sustain 8mbps. Imagine situation una 8mbps halafu unapata 3mbps sawa na mwenye 4mbps.
 
Nilipewa option hiyo pia kwenye modem ndo nasubiria soon nijionee mwenyewe.

Sina experience na ADSL ila kwa jinsi nilivyoelezwa sidhani kama inaweza sustain muda mrefu, labda from time to time.
 
Nikiwa kama mdau, TTCL copper iko vizuri na bei ni sawa na bure. Sogea ofisi yoyote iliyo karibu na wewe.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom