Naombeni email address ya bwana NEHEMIA KYANDO MCHECHU nimpashe habari ya BOKO NHC

Vakwavwe

JF-Expert Member
May 16, 2009
503
100
kama kuna mambo magumu kuyameza hapa jijini basi ni hili la maji HAPA boko KWENYE Nyumba ZA mradi zilizojengwa na NHC kwa msaada wa mashirika ya kimataifa na kuziuza kwa wananchi kwa bei inayosadikika kuwa nafuu.....

kwa ufupi ni kwamba: nyumba hizi zilijengwa kisasa sana na mpango ulikuwa kuzijenga kitalaamu sana na kuweka huduma zote za kijamii....kama ilivyo hapa Tz rushwa kila kona,network ya maji ilitakiwa ijengwe chini ya usimamizi wa DAWASCO, lakini wakawafunika ikapewa kampuni moja na kutandaza network hiyo na cha kushangaza wakalipwa in full bila kuujaribu mfumo wenyewe. kilichotokea baada ya kumaliza ujenzi na kuziuza DAWASCO wamekataa kuupokea mradi huo wa maji ila wakaunda kagenge ka wahuni kanaitwa KAMATI YA MAJI...wakakubaliana kuweka flowmeter moja kubwa kupima maji yote yaingiayo kwenye nyumba zaidi ya 200 na kuweka mita ndogo kila nyumba ili waanze mavuno.

DAWASCO wanasoma hiyo mita kubwa na kuibili kamati ya maji na kamati inaanza kupita nyumba kwa nyumba kukusanya pesa za kuchangia....hawana utaalamu wowote wa masuala ya maji,hawana sheria yoyote inayowalinda kwa kuingia kwenye nyumba za watu....maji yalikuwa yanamwagika hovyo kwa ubovu wa kimfumo ila DAWASCO kwa unyang'anyi mkubwa wanaibili tu kamati ya maji....

Mtu utajiuliza DAWASCO wenye ujuzi mkubwa wameushindwa mradi ila kwa makusudi wakaamua kuwalang'ai kamati na kuiachia majukumu hayo mazito wao wanakuja kuvuna tu mwisho wa mwezi....hakuna service yoyote wanayotupa sisi wakazi ila wanatucharge pesa...tena nasikia wanacharge bei ya watuniaji wakubwa eti kwa kuwa tunashare mita....

kwa sababu ya shida ya maji wakazi wakarubunika nao wakaikubali kamati hiyo ila kilichoendelea ni vitendawil...kila baada ya muda mfupi kamati hii infukuzwa inawekwa mpya...mpaka sasa tupo na kamati ya tatu ambao wanaganga njaa zao tu na kuwakusanyia DAWASCO MAPATO WASIOSTAHILI.

....NASIKITIKA SANA KWA HAYA YAFUATAYO.

1. NHC wamekaa kimya kwa muda wote huu na hawana msaada kwa kuwa wanajua wao ndo waliohusika kwenye kuwadhulumu wananchi wasiona hatia(siku hizi wanaitwa wapiga kura). waliahidi kuwa kutakuwa na maji ndani na barabara za lami ila sasa maji hakuna yalishakatwa na wanyang'anyi fulani wanaitwa DAWASCO,barabara zina mashimo makubwa sana ukienda pembeni gari inaweza kuzama kabisa kwenye mashimo na kutoka mpaka msaada wa waokoaji...

2.Kwa nini DAWASCO wanakata maji wakati wao hakuna wanachotufanyia....uwekezaji mkubwa wa maji unafanywa na DAWASA,wao wanatakiwa watubill kwa kutupa service kwa mwezi. Nasikitika kwa kuwa wameiajili kamati ya maji ambayo inabidi imnyonye kwa bidii mwananchi ili mwisho wa mwezi walipe DAWASCO na wajikimu wao.

3.Kuna mamlaka moja inaitwa EWURA, nayo ndo walewaleee...wao wameruhusu ili kufanyika na kamati hii isiyo rasimi inachaji tZS2500 kwa unit ili kufanikisha mambo mambo mawili kujikimu wao na kulipia DAWASCO....na ukumbuke ukitembea kama KM moja tu wanalipa TZS725 kwa unit...linganisha utofauti huo!!EWURA wao wanasema hiyo ni miradi ya maji wao hawahusiki japokuwa hakuna sheria inayowaruhusu DAWASCO kuanzisha vidawasco vidogo bila ruhusa ya EWURA.

4. serikali imenyamaza,wananchi wanaendele kunyonywa maana maji yamekatwa na ukinunua ya boza wanauza TZS10,000/- kwa unit....hivi kweli nitalipa kodi kwa moyo mkunjufu wakati nanyonywa nyie mmenyamaza kimya??mbunge uko wapi weye?DIWANI upo kweli?....RAIS mstaafu aliwahi kuja akadanganywa na NHC kuhusu maji,alikuja waziri mkuu wa ZAMANI akadanganywa na NHC kuhusu maji,wamekuja kamati ya maji wakadanganywa pia na NHC.

5.Mheshimiwa NEHEMIA tusaidie tunaangamia sisi wapiga kura huku BOKO NHC,maji yapo hapa lakini tunanyimwa kuyapata..kwa nini usirekebishe hii na kuyarudisha kwa DAWASCO watuhudumie?...wengi wetu ni wastaafu tulitumia masalia yetu kununua nyumba hizi tukitegemea huduma zote zipo..leo maji tunanunua ghali kuliko chakula....
 
Back
Top Bottom